What is this? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What is this?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by UZEE MVI, Sep 17, 2011.

 1. U

  UZEE MVI Senior Member

  #1
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Muda mfupi uliopita nimepita karibu na viwanja vya shule ya sekondari ya kinyerezi iliyopo manispaa ya ilala jijini dar.
  Nimeona watu waume kwa wake vijana wazee na watoto wote kwa ujumla wao wakiwa wamevalia mavazi mazuri ninayoyapenda ya kiislam(mimi ni mkristo).

  Kwa kuwa nafahamu kuwa shule ya sekondari ya kinyerezi ni ya serikali, nikalazimika kumwuliza mwenyeji wangu(yeye ni muislam) kulikoni?
  Amenijibu kwa masikitiko makubwa kwamba siku hizi baadhi ya shule zinafanya mahafali mbili tofauti. Moja kwa ajili ya wakristo na nyingine kwa ajili ya waislam. Na hao watoto wamekuwa wakisoma pamoja kwa miaka kadhaa. Mwenyekiti ameendelea kuonyesha masikito makubwa juu ya mbegu hii mbaya ya ubaguzi inayopandwa kwenye udongo mzuri wa watoto wetu.

  Nimebaki najiuliza maswali mengi bila majibu.

  1. Haya yameanza lini?

  2. Je serikali yetu(inayajua haya na imeyaruhusu)

  3. Aliyeanzisha haya anajua madhara yake?

  4. Vipi kwa watoto ambao ni waumini wadini zingine tofauti na ukristo na uislam au wapagani, je hawana haki ya kushiriki mahafali?
  Naomba kutoa hoja. Nadhani hili ni jambo la kukemewa.

  Niko tayari kusahihishwa au kupata maelezo sahihi pale ambapo maelezo yangu yataonekana kuwa yana mapungufu.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. M

  MAKAKI Senior Member

  #2
  Sep 17, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umeuliza vzuri lakini labda ni mahafari ya kidini au hujuag hilo. kama ni mahafar ya dini ni sawa na ni sahihi kabisa ila kama ni la kishule ni makosa makubwa!
   
 3. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mkuu hayo yawza kuwa mahafali ya dini ya kiislamu...................huh
   
 4. m

  maoniyangu Member

  #4
  Sep 17, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu hujaenda shule au? kama hujui ni kwamba huwa kuna vyama vya kidini vya wanafunzi mashuleni na hata vyuoni. kwaio huwa kunakuwa na mahafali ya vyama hivyo ambayo huwa hayaandaliwi na shule ila wanafunzi wenyewe na walezi wao. baadae ndipo hufanyika mahafali ya shule ambayo ni kwa wote bila kujali dini.
   
Loading...