Hili ni neno pana lakini nitajaribu kulielezea niwezavyo...
Mental strength au wengine wanita mental toughness
ni uwezo wa kuweza kuhimili mikikimiki ya maisha. Ni
ku-control
inner-world (how you feel) bila kujali
outside-world (circumstances).
Nipale unapo endelea kufanya kile unachokitaka kufanya
bila ya kujali kama utafanikiwa au la (courage). Mfano
kama umeanzisha biashara na hukufanikiwa badala ya
kuanza kujiona huwezi biashara, (ukiwa na mental strength)
utajaribu kutafuta njia nyingine bila kujali yaliyo tokea.
Pia kama umepata matatizo "
mental strength" ni uwezo
wa kutafuta jinsi ya kuyaondoa.Mfano kama umefukuzwa
kazi badala ya kuanza kutwanga maji ili kupunguza
mawazo mwenye "
mental strength" hukaa chini na kupanga
jinsi ya kupata kazi nyingine.
Mental strength inaweza kuwa ni uwezo wa kukubali hali
halizi ya mambo yaliyo tokea na kuyakabili. Mfano kama
umempa binti fulani mimba badala ya kumkana unakaa nae
na kuanza kupanga jinsi mtakavyo mlea mtoto.
Mental strength pia ni kuwa na "
emotional intelligence"
nikimaanisha uwezo wa ku-control emotions wakati wa
maamuzi. Mfano
nimesoma hapa JF kuwa Shayrose
alimrushia simu mgombea mwezake mtarajiwa kwasababu
aliambiwa anagombea ili kutafuta mume.
Yeye hakuweza kufanya maamuzi sahihi na kuacha emotions
zake kum-control. kama angekuwa na "
emotional intelligence"
wakati ule angeweza kujua kusudi la yule aliye mdhihaki
na angetakiwa kutabasamu (japokuwa inauma).