What if Mombasa ingekuwa sehemu ya Tanzania?


Heligoland Treaty ilifanyika kati ya ujerumani na Uingereza. Mkataba huu uliweka makubaliano kwamba Zanzibar iwe nchi huru baina ya mataifa haya mawili. Kwamba mwingereza au mjerumani ana uhuru na haki sawa ya kuingia Zanzibar na kufanya chochote. Na hii waliifikia sababu ya kiulinzi zaidi. Zanzibar iko sehemu ya kimkakati baina ya mwingereza kenya na mjerumani Tanganyika. Na hapo kupitia hiyo treaty tunaweza kujifunza kwanini Mwalimu alipambana sana ili kufanikisha muungano. Ni historia ndefu toka zamani huko.
 
Vip kuhusu Morserby treaty mkuu..
 
Naomba uisome vizuri Heligoland Treaty
 
Tanzania ndio ingekuwa sehemu kuu ya Bata Africa Mashariki
 
Mombasa ilikuwa sehemu ya Tanganyika ndio.maana kuna makabila kama wadigo wapo mombasa na Tanga na Kilimanjaro ilikuwa sehemu ya Kenya.
Ni kweli kenya waliwahi kuidai Kilimanjaro lakini rais wa kwanza wa Tanganyika akawaambia wairudishe mombasa kwa kuona watakosa bandari wakafyata mkia.
 
Ndio hivyo mkuu, mjerumani alimuachia mwingereza Zanzibar ili aweze kutawala vizuri pwani ya kenya na kenya in general. Ila bado mjerumani alikuwa na access ya kuingia Zanzibar.
Asante mkuu, kama ndivyo ilivyo nimeweza kuhisi ni kwanini Mwalimu aliungana na Zanzibar. Lakini ikikupendeza hapo tafadhali funguka zaidi tuelimike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…