......Bwana Magoti, mrefu kiasi na mweusi, anakuja kutupokea akiwa ameambatana na watoto wake watatu, wadogo; Happy, Eliza na Witi.
Tulipofika nyumbani kwake, alitukaribisha kwenye banda la uani ambalo baadaye alitueleza kuwa lilikuwa likitumika kufugia kuku lakini kutokana na ugumu wa maisha, sasa ndiyo makazi ya familia hiyo.
Robo ya banda hilo imejengwa kwa matofali na robo tatu iliyosalia ni maboksi (ceiling board).
Tulipowasili nyumbani kwake, mke wa sasa wa Magoti, Naomi Samson alikuwa akijiandaa kwenda kuuza ufuta katika Shule ya Msingi Buguruni na alipotukaribisha, tuliuliza bei ya ufuta naye alitujibu: “Huu ni Sh100, una Bluetooth, Whatssap na Memory card.”
Baada ya kununua ufuta wa Sh500, tulianza mazungumzo yetu na Magoti ambaye alifukuzwa kazi BOT Machi, 29, 1993.
“Nilikaa na mke wangu wa kwanza katika kipindi cha mwanzo tu wakati nina hela za mafao, baada ya hapo hali ilianza kubadilika naye akabadilika,” alisema.
Alisema miaka mitatu tu, baada ya kufukuzwa kazi, migogoro ilianza kwenye ndoa yake, mkewe alibadilika naye akawa hana sauti ndani ya nyumba.
“Kama huna kazi unakuwa mnyonge, huna sauti, kwa sababu kila unalomwambia atakujibu atakavyo na atasingizia anatafuta hela na wewe kweli huna.” Baada ya migogoro hiyo, mke wake aliondoka na kumuachia watoto watatu.
NILICHOJIFUNZA: Akina dada wote mliomo humu, nawapenda sana, story hii ya kweli ikapate kuwafumbua macho zaidi. Sisemi ya kwamba wote mpo kama huyo mwanamke(mke wa 1) aliemuacha Bwana Magoti wakati ameanguka.
Lakini nasema kwa wale ambao wanakuaga na dharau haswa kwa wenza wao wakiishiwa ama kupata matatizo, huezi jua ya kesho,ya Mungu mengi.
Sasa embu fikiria baada ya miaka 22, huyo mke mwingine wa Bwana Magoti ambae alimvumilia katika shida nyingi sasa ataaenjoi matunda ya uvumilivu wake kwa mumewe. Fikiria fidia na hio mishahara ya miaka 22 watakayolipwa na pia na job juu(tena BOT).
Sasa embu labda tungejiuliza yule mke wa kwanza aliekimbia yupo wapi sasa hivi ama kuna lipi la maana alilofanya...tena si ajabu Mungu kamueka hai ili aje ashuhudie then aanze kumpa mapigo matakatifu.
WHAT GOES AROUND ALWAYS COMES AROUND!!!