What drives you?

Mbagala stendi

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2020
Posts
343
Reaction score
407
Asalam allaykum, Bwana yesu asifiwe,
Habarini nyote mnaoendelea kupigania katika ndoto zenu.
Ungana nami katika maada fupi isemayo ni "kitu gani kina kudrive katika maisha yako"

"Driving force" ni msukumo wa kasi ambao kitu fulani kinavutwa kwa speed tofauti tofauti kutegemeana na mazingira na muda wa msukumo katika kitu hicho.

Kila Mwanadamu yuko na msukumo huo katika maisha yake... tofauti ni mwendokasi (Speed) ya msukumo huo kwani utofautiana.

Nguvu ya msukumo yawezakuwa ni kwasabbu ya matatizo unayokumbana nayo kila siku hukufanya huendelee kupambana kuondoa tatizo hilo.

"Tafuta pesa" huu ni msemo wenye maana kubwa kwa wenye malengo matokeo yake kwa sasa wengi uichukulia ni lugha ya mitandaoni hasa Tiktok & instagram


Leo napenda nikupe hizi 5 Tips
naweza sema ni nguvu za misukumo katika maisha.

Driven by Fear (Uwoga)

Wanadamu wengi tumekuwa tukiogopa kufanya jambo fulani kwa sababu ya uoga wetu binafsi katika nafsi zetu hii inatokana na traumatic exprience, unrealistic expectations,growing up in a high control home, even genetic prediposition mfano ulemavu wowote, Shortness & tallness statue. Watu hawa wanaoendeshwa na mshukumo wa UOGA katika maisha wanajikuta katika dimbwi la kukosa fursa na maarifa mbalimbali kwa sababu ya kuhofia kitu fulani mwishoe hujikuta kushindwa kufikia mafanikio katika maisha yao. Hii utokana na ukosefu wa mitazamo chanya na yenye kuleta tija baadala ujikuta waki play safe na kuendelea ku maintain their status. Vijana wengi wanalalamika kuhusu mapenzi wengi ni waoga wa kumove on au kuanzisha mahusiano mapya, Uoga wa kuangalia fursa nyingine za kusaka ajira na biashara.

Driven by Materialism (tangible)

Wengi wamebeba fikra finyu ya kuwa na matamanio katika mafanikio yao yamebebwa na mitazamo ya kuwa na vitu au kitu fulan cha thamani. Kijana wa leo akipata simu inayoitwa Iphone wanahisi maisha yenyewe ndio haya
hii hutokana na ukosefu wa misconception katika mawazo wanadhani kuwa na vitu vingi au kitu fulan cha thaman ndio chanzo cha kuwa n furaha, kuwa muhimu zaidi katika jamaii au Kuwa more secure but hizi zote ideas tatu hazina mashiko. Kwa sababu Possesion only provide temporary happiness lakin vitu hubadirika kila majira and eventually we become bored🄹 with them then we want somthing bigger, newly and better version
than old one , hii itasababisha upotevu wa resources kwa ajiri ya kuendana na fashion. katika dunia ya leo hauwez kuendana na fashion kila kukicha new version is inovated.

Driven by Resentment and anger

Some resentment-driven people "clam up" and internalize their anger while others "blow up" and exploide it onto others.

Those who have hurt u in the past cannot continue to hurt you now unless u hold them... your past is past nothing will change accept and move on unajiumiza wewe mwenyewe with your bitterness accept and learn from it.

Driven by Guilt

Most spend their entire lives running from regrets and hiding their shame which manipulated by their memories... continue to handle their past to control their future mara nyingi hizi huwa panikisha
na kujikuta kushindwa kuyafikia malengo, hii tumeona wengi hujitoa uhai na kupoteza maisha.

Driven by the need for approval

They allow their expectation from others to control their lives. Most vijana husukumwa na peer pressure na kujikuta wakiingia katika maisha yasiofaa au yenye ushindani usio na sababu ya msingi always they worried about what others they might think about them... kwa bahati mbaya those who follow crowd they get lost.

Hitimisho: Misikumo huleta hamasha katika maisha na kuyafanya maisha yawe yenye kuleta maana na yenye kuwa na point A to point B yaani direction, without purpose life is trivial and pointless.
 

elimu ya hizi mambo jinsi ya kuishi nazo na kuzikabili zingefundishwa tangu elimu ya msingi huko mashuleni ingetengeneza vijana na vizazi vizuri sana,

imebaki kwetu tu sasa wazazi kuwapa elimu hii watoto wetu....dunia nayo inabadirika kila sekunde,
asante chief kwa kumbusho hili.
 
Elimu hizi haziwezi kufundishwa katika elimu ya msingi, binanadamu dunia nzima anatawaliwa na anatawalaiwa kupitia akile zake mwenyewe na elimu zetu zote zimejengwa ili kumtaarisha mwanadamu atawaliwe milele, kimsingi watu wote dunia nzima mwisho wao wa akili ni za mtoto wa miaka 12, hata mtu awe na umri gani au na elimu gani au awe na cheo gani akili zinazomtawala ni si zaidi ya mtoto wa miaka 12,akili hizi za mtoto wa miaka 12 ni lazima kila mtu aelekezwe kila kitu ni lazima apate msaada kila anapotata shida akiumwa lazima mtu mwengine amshughulikie na atibiwe na mtu mwengine,yeye Mwenyewe Hana uwezo wa kijitibu hata awe na elimu gani, yaani elimu zetu zinatujenga tuwe tegemezi na tuelekezwe kila kitu maisha yote tunayoishi duniani,na ukiwa tegemezi na ukiwa unahitaji maelekekezi maana yake wewe sio mtu mzima au matured.

Nirudi kwenye mada
Tukianza kufikiria nini kinamdrive binadamu, kinacho mdrive mwanadamu ni akili zake wala binadamu Hana uhuru juu ya akili zake,binadamu yeyote anaendeshwa na kutawaliwa na akili zake si zaidi ya hapo.
Kama akili zina khofu binadamu atatawaliwa na khofu, kama akili zina ujasiri binadamu atatawaliwa na ujasiri na vyote hivyo khofu na ujasiri vinaweza kuwa vitu vizuri au vitu vya kijinga kwa wakati na mazingira tafauti,

Kuna mambo mawili Yanampa tabu sana mwanadamu ndani ya uwezo wetu Wakiakili ulojengwa na elimu zetu za skuli na maisha, mambo hayo ni kuwa mwanadamu yeyote ana hamu kubwa sana ya kukubalika na kuheshimika, kiuhalisia vitu hivi sio muhimu lakini akili zetu zimejengwa kuviona vina umuhimu mkubwa sana,
Mambo yote tunayofanya kimasha na harakati zote tunafanya ili tupate heshima na tukubalike katika jamii zetu na familia zetu, tunataka tuwe wa mwanzo katika kila kitu ili sie ndio tukubalike zaidi na tuheshimike zaidi, tunataka tuwe maraisi,tunataka tuwe matajiri wakubwa kuliko wote,tunataka kuwa na elimu zaidi ya wengine katika jamii au familia, kwa ufupi katika kila kitu tunataka tuwe wa mwanzo

Mfano mzuri wa maisha ya mwanadamu ni mbio za mbwa(dog race) kwa walipata bahati ya kuziona mbio za mbwa wanaweza kunifahamu

Katika mbio za mbwa mbwa wanafunzwa wawafukuze mfupa na mfupa huwa hata sio mfupa wa kweli lakini mbwa hajui wala hajali kutaka kujua,shebaha ya mbwa ni kuutafuna mfupa tu bila ya kujali chochote na Hana uwezo wa kufikiria kitu chengine, uwanjani kunakuwa na mbwa wengine tafauti na wote wamefunzwa hivyo hivyo,pia kunakuwa na watazamaji wengi sana na mazogo ya kila aina lakini mbwa hawajali yote hayo,wanachojali ni mfunzo yao ambayo yamewajengea ari na hamu kubwa ya kuwa wa mwanzo kunasa mfupa tu, tatizo la hii dog race ni kuwa mfupa wenyewe umeungwanishwa na mashine ambayo ina kwenda kasi kubwa sana hakuna mbwa nayeweza kuufikia mfupa sababu Machine ina kasi sana, kwa maana hio dhana ya kuufikia mfupa ni illusion(ndoto) tu hata mbwa awe na mafunzo (elimu) kiasi gani au na nguvu kiasi gani mfupa ni ndoto unapoteza nguvu bure hicho anachokimbilia hakipo au hakifikiki na hata ikitokea mbwa akaufika mfupa atakuta ni plastic tu sio mfupa kweli kama alivyo Amini au alivyo aminishwa.

Sisi binadamu tunaishi ndani ya mfumo wa mbio za mbwa hata tukiyafika hayo tunayoyaona ni muhimu si lolote si chochote, unakuwa na hamu ya kuyafikia kama ikiwa bado hujayapata tu ukifika na kuyaona kwa macho na kuyagusa kwa mikono utagundua ulichokua ukidhani ni mfupa mnono ni plastic halina maana au thamani yeyote
 

Attachments

  • 78B18AC1-DBB3-48C3-ACE3-E4C02609A1B6.jpeg
    278.3 KB · Views: 13
  • 152BA114-3ADA-435E-82FE-630BC175FCB8.jpeg
    50.4 KB · Views: 13
Sisi binadamu tunaishi ndani ya mfumo wa mbio za mbwa hata tukiyafika hayo tunayoyaona ni muhimu si lolote si chochote, unakuwa na hamu ya kuyafikia kama ikiwa bado hujayapata tu ukifika na kuyaona kwa macho na kuyagusa kwa mikono utagundua ulichokua ukidhani ni mfupa mnono ni plastic halina maana au thamani yeyote[/QUOTE]







Hapo nimepapenda sana. Ni kweli wakati mwingine tunahangaikia mambo ambayo ukishayapata unaugundua bora ungeacha tu and at that time there's no turning back.
 
Mi nlijua driven na kitu unachopendelea kufanya...
Mfano force driven me is on Hard ware and so on and so on bro...!!!
 
Mi nlijua driven na kitu unachopendelea kufanya...
Mfano force driven me is on Hard ware and so on and so on bro...!!!

Zipo concepts mbalimbali za misukumo katika maisha kuna zile za level ya chini concepts, katikati na juu zaidi. Hiyo life based interest naweza sem iko level ya chini primary level ambayo asilimia kubwa kila mtu ukimface atakujibu ni kitu gan kina msukuma mfano mzur ukimuhuliza mwanafunz atajibu kitu kinacho msukuma ni Kufaulu vizuri katika masomo yake kwahyo muda mwingi atakuwa akiwaza katika masomo kwahyo huyu mtu kitu kinachomsukuma ni kupata Elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…