Baija Bolobi
JF-Expert Member
- Feb 25, 2009
- 1,093
- 1,727
Wasomi wa Sayansi ya Siasa wanaweza kutuelimisha juu ya kashfa ya Watergate miaka ya 1970 huko Marekani. Ofisi ya chama cha Democratic ilivunjwa na nyaraka kuibiwa. Ofisi hizo zilikuwa katika hotel iliyoitwa Watergate.
Bunge liliunda tume ya uchunguzi na ikakutana na vikwazo mbalimbali kutoka kwa serikali iliyoongozwa na Rais Richard Nixon. Watendaji wa serikali waliwaangaisha sana wajumbe wa tume na kuwanyima ushirikiano.
Hatimaye suala zima lilipofikishwa mbele ya Seneti, swali kuu lilikuwa ni :RAIS NIXON ALIJUA NINI KUHUSU UVUNJAJI HUO, NA ALIUJUA LINI? Majibu yaliyotolewa bila kupima, yaliashiria kuwa Rais alijua na alishiriki katika mpango wa kuvunja ofisi hiyo ili kuiba nyaraka na hatimaye kuanzisha vitisho dhidi ya wabunge walioonekana ni wapinzani kwa serikali yake. Kabla ya seneti haijapiga kura ya kukosa imani naye (Impeachment), Rais Nixon alijiuzuru akiwa na miaka miwili ofisini.
Je kuna mfanano kati ya Watergate na hiki kinachoendelea nchini kwetu? Je rais wetu JPM anajua kuwa kumekuwa na utekaji na vitisho kwa wabunge na mtuhumiwa mkuu ni idara nyeti iliyo chini yake? Je kama anajua, amejua lini? Na kama anajua amechukua hatua gani? Kama hajui na hakushiriki katika mpango huo mchafu, amechukua hatua gani?
Kama anajua, ni vema akachukua haraka hatua stahiki zinazolingana na uzito wa tatizo hili kwa yeye kushiriki katika jambo zito na chafu namna hii. Kama hajui, basi achukue hatua za kuwawajibisha IGP, DGI na mawaziri wao. Kwa nini? Kwa kusababisha yeye aeleweke vibaya na idara nyeti isemwe katika namna inayoiondolea heshima yake. Msingi wa utendaji wa idara hii huwa ni kuaminika na uadilifu wake - si usiri wake tu.
Wakati wa utawala wa Bill Clinton kulikuwa na kashfa ya Monica Lewisky. Mwendesha mashtaka maalum Keneth Starr aliwaita walinzi wa Rais (secret service) kuja mbele yake kuhojiwa kwa kiapo. Baadhi yao waliapa na kujiuzuru kumlinda Rais baada ya kuapa kwa sababu, baada ya kuapa na kulazimika kusema siri za Rais wasingeweza kuaminika tena hata kama yeye angewaamini.
Kitendo cha kusikika tu, kuwa walinzi wa rais wetu, wanahusishwa na vitendo vya jinai (kuteka, kutesa, kuvamia studio, kutisha watu, tena watunga sheria), wanautia usalama wa rais wetu mashakani sana. Usalama wa rais ni usalama wa nchi. Tusifanye mchezo katika suala hili.
Mimi nalazimika kupendekeza, hata kama kuna kutia chumvi katika suala hili; kwa kuwa kuna mazingira yanayoashiria hali hiyo ya kuhusika kwa kikosi hiki, hatua kubwa na za wazi zichukuliwe kurudisha heshima na imani juu ya taasisi yetu ya urais na ile nyingine ninayoiheshimu sana hata kuitaja jina nasita.