Hapa ni siasa zinachezwa kwa gharama ya kodi zetu. Mtakumbuka siku zile za kikao cha bunge alipojiuzulu Lowasa, Spika alikuwa tayari keshapata trip ya nje ili kukwepa kile kikombe kilichokuwa mbele yake. Jk alifanya jitihada za kumzuia asisafiri ili akabiliane na Lowasa. Na sasa hivi baada ya Lowasa kuunguruma bungeni na kushangiliwa na zaidi ya three qouter ya bunge, jambo hilo limemshitua Jk. Ndio maana amemtafutia safari haraka Pinda na kumkaimisha Sitta kile cheo ili amkumbushe EL kuwa kisu kilichomchinja bado kinashikiliwa na Jk. Kwa habari ya gharama kipesa, hiyo haimhofishi Jk, maana anatambua fika kuwa waTz hawajafikia uwezo wa kuhoji maamuzi ya mkuu wa nchi
.