Wezi wa kura wawajibike kwa nani?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Kuanzia mawaziri na sasa JWTZ wamekuwa wakijigamba ya kuwa hawawezi kujiuzulu kwa misingi ya uwajibikaji kutokana na utendaji mbovu wa taasisi wanazozisimamia.........

Huu ugonjwa unaanzia pale tunapopiga kura na watawala wanazichakachua na kujitangazia matokeo ya kura wayatakayo wenyewe...................hivyo kufuta aina yoyote ile ya wao kuwajibika kwa wapigakura na ndiyo maana watawala waliomo ndani ya Baraza la Mawaziri au ndani ya taasisi za umma kama JWTZ hawaoni sababu ya kuwajibika kwa sababu hata kama hatuwataki hatuna uwezo wa kuwafukuza kazi kupitia nguvu ya ballot box.............................................kwetu sasa kilichobakia ni nguvu ya umma....................kupitia maandamano yasiyo na ukomo kuwalazimisha waachie ngazi..............................hatuna njia nyingine kwa sababu maovu dhidi yetu yamezidi kipimo.....................tukisubiri uchaguzi tuandike maumivu kwa sababu hakuna uhusiano kati ya kura zilizopigwa na matokeo ambayo watawala huyatangaza...................

unapoona serikali inaua watu kila mara na hakuna kiongozi yeyote ambaye yupo tayari kuwajibika na hata waathirika na wahanga hawapewi fidia kulingana na madhara waliyoyapata ujue hilo taifa linaongozwa na viongozi ambao siyo wacha Mungu..........................huwezi ukaua raia halafu udai unawapa kifuta chozi......kwani haya majanga ambayo ni man-made kwa nini tuyachukulie ni natural disaster????????????????????????????

let us learn to be serious on serious issue of national profundity....................
 
Mkuu, wanajeshi wako sahihi kabisa kwamba hawatakiwi kujiuzulu kama wanasiasa.
Ni jukumu la Amiri Jeshi Mkuu kuwawajibisha kwa kuwabadilishia kazi au kuwastaafisha. Juzi juzi yule mkuu wa majeshi ya Marekani kule Afghanistan aliropoka maneno tu Obama akamwondoa

Sasa ukiwa na jeshi ambalo linachukua majukumu ya Rais kuamua kwamba watajiuzulu au la, ina dalili kwamba hatuna Amiri Jeshi Mkuu hapa. Ile kauli aliyotoa yule meja jenerali ilitosha kabisa kumfukuza kazi kama Amiri Jeshi Mkuu angekuwa mtendaji makini. Alichotakiwa kufanya yule meja jenerali ni kusema kwamba hilo ni jukumu la Amiri Jeshi Mkuu kuamua
 
PHP:

Mwanajeshi ni mtumishi wa umma na anapaswa kuwa na maadili ya kumwongoza kwenye shughuli zake..............................hapaswi kutumia udhaifu wa Raisi kama kichaka cha kuficha maovu yake..................................................

Hakuna tofauti ya mwanasiasa na mwanajeshi kweye dhana nzima ya uwajibikaji........................................
 
Kichwa cha habari hakifanani na habari husika. Pili mwizi ni yule aliyekamatwa na kuthibitika pasipo shaka kuwa kweli kaiba. Wengine wote ni watuhumiwa. Tupo wote mkuu?
 
Back
Top Bottom