Wezi ni watu wabaya sana, wameniibia masufuria yangu yote kwenye kamgahawa, nimerudishwa jalalani

Tamati

JF-Expert Member
May 15, 2017
1,085
1,956
Nikiwa hata bado sijamaliza mwezi mmoja na hata bado sijaanza kuona faida ya haka kabiashara kangu cha mgahawa.

Nimerudishwa jalalani kuibuka tena hadi nitumie nguvu za ziada. Wezi wamevamia kakibanda wamefyatua kufuli likafunguka na kuiba masufuria yangu yote, chupa ya chai na hotport vyenye thamani ya jumla ya Tsh 82,200/=

Daahh, katika maisha tunategemeana, ukipitia njia ya halali mwenzio anapitia njia ya haramu kukurudisha nyuma.

Mungu ni mwenza ngoja nianze kujichanga tena ili nijinasue jalalani kidogo kidogo.
 
Aisee pole sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Pole mkuu utainuka tena, ondoa mawazo ya kushindwa, mshukuru Mungu kwa uhai maana bado iko fursa ya kuinuka tena na kuanza upya. Nafasi bado ipo.

Dedication

Kimbia faster toka nduki we kimbia ukianguka ukiumia inuka vumilia
 
pole aise wezi dawa yao petroli
Petrol sio dawa,kwa Jinsi ambavyo walivyonifanyia sebuleni kwangu, kufanya sebuleni kwangu kuwa uwanja wa mpira(kuiba kila kitu).mm mwizi huwa sihangaiki kuwachoma Moto,huwa nachukua bisbis nawatoboa macho,kuua ni dhambi kubwa.

Kuna mmoja aliiba nyumba ya jirani hasira zangu nilimtoboatoboa macho,huko alipo haiwezi kunisahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom