Salaam jf.
Jamani nashindwa kuelewa hawa wezi ni watu aina gani katika maisha haya ya kila siku tunayoishi, kwa sababu nashindwa kushangaa! manake napigwa na butwaa pale nilipo muona jamaa fulani ambaye anafanya kazi katika wizara ya mambo ya ndani, kumuona anaogopa wezi imefika mahali mpaka gari yake kaitia security system kwa ajiri ya kuwaogopa hawa jamaa. Wakati katika hali ya kawaida wao ndio wanatakiwa wasiwe na hofu yeyote kuhusu uhalifu, kwa sababu wao ndio wanao husika katika maskhala ya ulinzi wa ndani ya nchi yaani wanafahamu system inside out. Sasa kama afisa katika wizara anaogopa wezi, vipi sisi raia wa kawaida? Kwa maana hiyo inaonyesha wezi wanaishi maisha ya amani kuliko hata baadhi ya maafisa, manake huku kwetu kuna wazito lakini kila siku wanalizwa maskrini ya mamilioni na upelelezi unagonga mwamba anabaki kusema ''hakya mama nitaua mtu'' lakini wapi.