Wewe usiye na mtoto pitia hapa upate ukweli

Wewe usiye na mtoto pitia hapa upate ukweli

Ok9

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2013
Posts
4,554
Reaction score
4,171
Kwamfano;

Unapata mtoto ukiwa na miaka 30, mtoto baada ya miaka 6 anaanza darasa la 1, wewe una miaka 37.

Anamaliza darasa la 7, wewe una miaka 44. Anamaliza kidato cha 4, wewe una miaka 48. Anamaliza kidato cha 6, wewe una miaka 50. Anajiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, wewe una miaka 51. Anamaliza Chuo kikuu 4years, wewe una miaka 55

Anatafuta kazi na kuanza kujitegemea mwaka mzima, wewe una miaka 56.Hapo mtoto hajafeli wala kurudia Vidato.Huyo ndio first born wako hapo tumeasume umempata ukiwa na miaka 30.Life expectancy ya Tanzania ni miaka 52.

ZAENI MAPEMA ACHENI UBISHOO copy & paste
 
Mushi92, umezungumza jambo la maana sana, tatizo watu wengi wanogopa maisha, na wadada wao wanasubiri Mr right. As if yeye yuko right....
 
Last edited by a moderator:
Mushi92 hii ipo humu muda kwa heading ya Life expectance ya Tanzania; Asume unapata mtoto ukiwa na miaka 30
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
poor calculation haijajumuisha factors nyingine za kimaisha
 
Kwa wengine maisha sio freestyle, kila move inakuwa calculated. Siku nikijiskia kuwa m'dingi ntajipima kama nastahili kwanza, hiyo number hata nikiifikia bila copy sidhani kama ntapagawa.

Almost every man can be a daddy, but very few can be fathers.
 
Mi wangu wakifuata hizo process zote wataajiriwa nikiwa on my early 40s. . .Angalau hata nikipata mjukuu kipindi hicho bado ntakuwa na nguvu ya kucheza cheza nae.

Ila kabla ya kuzaa ni muhimu mtu ajiangalie kama yuko tayari kubeba jukumu la kuwa mzazi au la. Maana kuwa mzazi sio kazi ndogo, inahitaji kujitoa sana.
 
poor calculation haijajumuisha factors nyingine za kimaisha

Sisi tunaosoma economics ili theory ifanye kazi kuna kitu inaitwa 'ceteris peribus' mtoa post ndiyo katumia. Akiwa na maana 'other things remain constant'
 
Mi wangu wakifuata hizo process zote wataajiriwa nikiwa on my early 40s. . .Angalau hata nikipata mjukuu kipindi hicho bado ntakuwa na nguvu ya kucheza cheza nae.

Ila kabla ya kuzaa ni muhimu mtu ajiangalie kama yuko tayari kubeba jukumu la kuwa mzazi au la. Maana kuwa mzazi sio kazi ndogo, inahitaji kujitoa sana.
usiogope kuzaa haijalishi una kitu au hauna kitu mfukoni, maisha ni mzunguko unaweza kuzaa wakati una kitu halafu kitu ikapotea wakati mtoto bado yupo kwenye makuzi, ina mana utamuua ?
 
Huu ukweli unauma, but too late for me. Ngoja nikomae ivo ivo
 
usiogope kuzaa haijalishi una kitu au hauna kitu mfukoni, maisha ni mzunguko unaweza kuzaa wakati una kitu halafu kitu ikapotea wakati mtoto bado yupo kwenye makuzi, ina mana utamuua ?

"KUWA TAYARI" hakumaanishi kuwa na pesa. Kuna kuwa tayari kiakili na kihisia pia. Watu kibao uwezo wa kununua pampers na maziwa wanao lakini mwisho wa siku wanishia kufungia watoto wadogo ndani ili waende club na sehemu nyingine za starehe. Ndio maana nikasema kuwa mzazi ni kujitoa, meaning kuna mambo mtu atalazimika kupunguza au hata kuacha kabisa ili aweze kutimiza majukumu yake kama mzazi. Kama mtu hayuko tayari kwa hilo ataishia kuwa mama/baba ambae irresponsible. Na kuliko mtoto apate shida kwa kuwa na mzazi/wazazi irresponsible ni bora mtu akawie kuzaa.
 
Mtoto ni zawadi toka kwa mwenyezi mungu.unaweza ukaoa mapema ikaisha miaka 7 bila kupata mtoto.pia inategemea uchumi na uwezo wa kumudu maisha ya familia.wasichana wa siku hizi akila dagaa siku 3 anakupa talaka.
 
Wewe unaejaza mimba watu wazae kwann unaikimbia majukum ya familia je utakua umefundsha nin kwa kizaz hicho?
 
mi first born wangu akifuata mpangilio huo wa shule atahitimu chuo nikiwa na 38 mdogo wake atakuwa o-level
 
Mtoto ni zawadi toka kwa mwenyezi mungu.unaweza ukaoa mapema ikaisha miaka 7 bila kupata mtoto.pia inategemea uchumi na uwezo wa kumudu maisha ya familia.wasichana wa siku hizi akila dagaa siku 3 anakupa talaka.

Tatizo.... Mnapenda kuishi maisha ya bongo movie wakati mkiwa wachumba...... Anategemea mambo saf kumbe hakuna kila ki2
 
Back
Top Bottom