Wewe ungefanyaje?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,353
Reaction score
26,194
Habari zenu waungwana!

Huu ni mkasa wa kweli. Ilikuwa hivi:

Jamaa mmoja ambaye ana tabia fulani fulani za ukware,alikuwa nafanya kazi shirika fulani la umma. Jamaa huyu ameoa na mkewe anajulikana kazini kwake hasa kwa bosi wake(ambaye yeye anamwendesha garini).Kudhihirisha hilo,hata nambari ya simu ya mkewe inajulikana na bosi wake.

Kuna siku jamaa alikumbuka kimada wake.Akamhaidi kwenda kulala huko.Kwa mkewe akaaga kuwa atasafiri kwenda Bagamoyo na bosi wake hivyobasi hatarudi nyumbani siku hiyo na itakayofuata. Lakini,siku iliyotangulia bosi wake alipatana na jamaa kuwa atamwaisha Ikulu kwa mazungumzo na wakuu wa nchi hii. Wakakubaliana kuwa safari ya kuanzia shirikani hapo hadi Ikulu itaanza saa mbili asubuhi kwakuwa kikao ni saa nne kamili asubuhi.

Kweli siku ya siku jamaa akalala kwa kimada. Hakumwambia kimada wake kuwa asubuhi atawahi kazini.Alisahau. Usingizi ukamteka. Kushtuka,ni saa nne kasoro. Ile kuwasha simu tu,bosi anapiga. Huku akitetemeka,akamwambia kimada ajifanye kuwa ni mkewe na amwambie kuwa yeye(jamaa) hakuamka vyema.Ana homa kali sana.

Kimada akapokea simu. Alipoeleza vile,bosi kwa sauti ya upole akasema mpe pole. Vilevile akasema 'nitakupigia kwenye simu yako baada ya dakika mbili tuongee vizuri kwakuwa simu hiyo inakoroma kidogo'.Bosi alimaanisha kuwa punde angepiga kwenye simu ya mke wa jamaa. Basi,akakata simu tayari kumpigia mkewe amwulize vyema ugonjwa wa mumewe.Balaa!

Ikumbukwe kuwa ikipigwa simu ya mkewe,itapokelewa nyumbani kwa jamaa ambaye ameaga kusafiri na bosi huyo huyo. Na bosi huyo anasifika kwa ukali hasa anapoongopewa kama ilivyo kwa mke wa jamaa. Wafanyakazi wengi walishafukuzwa kwa makosa ya uongo kama hayo.

Simu ya bosi ilipokatwa,jamaa akaanza kuumwa kweli...akachanganyikiwa asijue la kufanya. Akawa anatetemeka kisawasawa. Alimchukia hata kimada aliyekuwanaye. Aokoe kazi au ndoa? Apoteze kazi au ndoa? Au vyote? Njia panda!

Yeye aliamua kuokoa ndoa kwa kwenda kutubu na kujuta kwa mkewe aliyemkuta amefura kwelikweli siku hiyo na karibu mwezi mzima. Kazini hakwenda tena.

Wewe ungefanyaje?

cc Kaunga The Boss snowhite,@FP Mtambuzi, Bujibuji mzabzab mwaJ et al
 
Amefanya vizuri kuokoa ndoa, ila bado angeweza kuokoa na kazi kama angefanya kama odg alivyoshauri.
 
Last edited by a moderator:
Mi fasta ningempigia wife ili akipigiwa aseme kweli naumwa.... Then baadae ningekaa nae na kumuomba msamaha.... Ingawa guys sio poa kuchezea kazi, mshahara ndo unaweza kuuchezea....
Labda kuchanganyikiwa kungekuchelewesha
 
ngoja aje The Boss hapa ndo utapata majibu mazuri!
wengine tunagwaya gwaya tu hapa!
unajua atakwambia nini?
mmmmhhhhhh!sasa we utajiongeza mwenywe atakuwa anamaanisha nini!lol
mimi :tape2:
 
Last edited by a moderator:
Kwanini unadhani amefanya vyema kuokoa ndoa kuliko kazi?

Rafiki yangu ndoa ni scared thing, ikimess nayo ni laana hata kazi inaweza isizae matunda stahiki.
Unaposaliti ndoa, unajikosea mwenyewe (mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu), unamkosea Mungu, unamkosea mkeo, unamkosea ulozini naye, watoto, wasimamizi wa ndoa na jamii nzima.

Hivyo ukitubu na kuacha basi unajitakasa na kujiosha na milaana iloambatana na uzinzi wako.
Mungu atamsaidia for the sake of mkewe na watoto apate kazi nyingine kwani alichagua fungu jema (la kumkataa shetani na kumrudia Mungu).
 
Haya wale wakware, swali la kipima joto hilo limerushwa kwenu....baadaye nitapita kuchua matokeo na kuyarusha ITVVVVVV!!!!
 
Hahahahahaaaaa.vere simpo!!!

Anakata tu na mimi nampigia wife...


Tunabonga weeee such that by the time boss anapiga anakuta line iko engaged!!!

ataghairi na kwenda kikaoni Ikulu...sasa mpaka kikao kiishe nadhani akili itakuwa imerudi poa!!!
 
Nikisema ntafanya nini si itabidi nizini nje ya ndoa ili niwalk the talk{ni aply utetezi niliosema}?
 
Ah... mis sio dereva wa Bosi siwezi fanya upuuzi huo...
 
Hahahahahaaaaa.vere simpo!!!

Anakata tu na mimi nampigia wife...


Tunabonga weeee such that by the time boss anapiga anakuta line iko engaged!!!

ataghairi na kwenda kikaoni Ikulu...sasa mpaka kikao kiishe nadhani akili itakuwa imerudi poa!!!
Inategemea na uwepo wa vocha Mkuu Mentor
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…