Wewe unataka hiki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wewe unataka hiki!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 20, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Haya.. mapumziko time!

  Wewe unataka hiki, naye anataka kile,
  Mkononi unachaki, ubao wake ni ule,
  Mwaitana marafiki, tangu nyie mko shule,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mwaringiana?

  Wajua anakitaka, anajua wakitaka,
  Wote mwajua mwataka, mmebaki na mashaka,
  Mmebaki na dhihaka, na kicheko mnacheka,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mnazungushana?

  Cha kwake unakipenda, cha kwako anakipenda,
  Sasa wote mmekonda, zinawadondoka denda,
  Kwa wenzako wamponda, kwa wenzake akuponda,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mnategeana?

  Usiku unapolala, ndotoni unakiota,
  Naye anashindwa kula, kutwa anaona nyota,
  Wawacheka wenye hila, kwa jinsi mnavyosota,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mnaumizana?

  Unasubiri aombe, anasubiri uombe
  Sasa mmeota pembe, za kiburi na kimbembe,
  Ati hutaki atambe, naye hivyo hivyo kumbe,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mnangojeana?

  Sasa nenda utamke, uwe wa kwanza kunena,
  Fanya hima mualike, hilo ungefanya jana,
  Cha kwako ukipeleke, anakungoja kijana,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mwachelewashana?

  Umpe kilichojaa, si kibaba bali pishi,
  Umpe kama kichaa, mfike Kapirimposhi
  Na umpe kwa ridhaa, akupe bila ubishi,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mwakodoleana?

  Ushauri nawapeni, msipende kutegana,
  Mkitaka peaneni, vile mnavyoombana,
  Msinyimane jamani, ni vizuri kugawana,
  Ulichonacho ataka, alichonacho wataka
  Mbona mnakubaliana?

  Wewe unayo sukari, na yeye ana kikombe
  shirikianeni kutengeneza chai..

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
   
  Last edited by a moderator: Mar 22, 2009
 2. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,698
  Likes Received: 8,238
  Trophy Points: 280
  ndiyo mimi nakitaka, naye pia akitaka,
  ila shida ukipata, mara moja jatosheka,
  ningependa kukipata, naogopa nikipata,
  nilichonacho ataka, alichonacho nataka
  ilA TUNAVUMILIA.

  muda bado hujafika, japo sana twatakana,
  mwili unababaika, nimwonapo huyu mwana,
  twajua siku tafika, tutapeana kwa sana,
  nilichonacho ataka, alichonacho nataka
  ilA TUNAVUMILIA.

  mvumilivu huvuna, na hulia kivulini,
  mda mrefu hakuna, ingawa hatujui lini,
  kwa upendo tutaona, matunda ya kujijali,
  nilichonacho ataka, alichonacho nataka
  ilA TUNAVUMILIA.

  Mimi ninayo sukari, na yeye ana kikombe,
  lakini chai bora yahitaji maandalizi zaidi!??
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2009
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,698
  Likes Received: 8,238
  Trophy Points: 280
  Mvumilivu Hula Mbivu!
   
Loading...