Hujawahi kufikiria na hutaweza kuamini, lakini ukweli ndio huu. Wewe unaweza kuwa sababu kubwa sana ya mpenzi wako kuonekana ana kasoro kibao,hawezi kuwa mpenzi sahihi kwako henda ni kwasababu ya umakini ulionao na tabia yako kwake ambayo inasababisha kuzalisha ubaya kutoka kwake yani kuonekana hafai hata kidogo.
Na utakuja kushangaa mtu yuleyule ambaye alionekana mbaya kwako, mwenye mapungufu mengi, na hafai anakuja kuwa mzuri sana na kufaa pindi tu atakapooa au kuolewa na mtu mwingine atakayemthamini, muheshimu na kumtunza vizuri inavyotakikana.Kuna kazi kubwa ya kufanya unapokuwa na mwenzi wako. Ulishawahi kulifikiria hilo?
Je ni yapi utakayoweza kufanya kuuonyesha uzuri wa mwenza wako uliojificha?