Elly Andrew
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 410
- 174
Je, ni kweli kuwa unachukia sana watu wanapokuwa na mtazamo tofauti na ulionao? Ni kweli unatamani na hata umewashughulikia wote walio kinyume na wewe kimtazamo?
Ngoja nikufikirishe. Hivi umewahi kuwaza uumbaji wote wa Mungu kwa nini unadhihirisha kuwepo kwa uwili unaosigana/kupingana? Kama hujauelewa uwili unaosigana fikiria kuhusu mwanaume/mwanamke, usiku/mchana, mwanga/giza, utamu/uchungu, uzuri/ubaya, wema/ubaya.
Hivi umewahi kufikiria thamani ya elementi yeyote katika uwili huo unaosigana bila kuwepo kwa elementi ile nyingine ya pili? Kama hujaelewa jiulize kuwa hivi ungeelewa thamani ya mwanaume bila kuwepo mwanamke? Hivi ungeelewa thamani ya mwanamke bila kuwepo kwa mwanaume?
Hivi leo ungejua thamani ya mchana bila kuwapo kwa usiku? Ungejua thamani ya mwanga bila kuwepo kwa giza?
Kwa hakika uwili unaosigana ni suala la Kiuungu (kwa wanaoamini kuwepo kwa Mungu) na suala la kiasili (kwa wanaoamini katika asili).
Sio ajabu licha ya uwezo wote alionao Mungu bado aliuuacha utawala wa shetani nao uendelee kuwepo. Kwani ni kwa kupitia shetani ndipo uwezo na ukuu wa Mungu unadhihirika kuwa juu ya nguvu na mamlaka zote.
Sasa wewe ni nani unayetaka kusiwepo na uwili unaosigana katika kufikiri? Watu wote wawaze kwa namna moja? Kwamba ni kosa ukikosolewa? Wote waione dunia kama unavyoiona? Kwa hakika unafanya kinyume kabisa na Misingi ya Uumbaji. Umejiinua mno kuliko inavyostahili.
Jifunze kuufurahia uwili unaosigana. Katika uwili huo ndipo ubora wako utadhihirika. Tofauti na hapo ni sawa na kuwa na utamu pasipo uchungu. Utamu hautakuwa na maana yeyote.
c & p