Wewe ni Mchepuko tu, wivu wa nini?

Wewe ni Mchepuko tu, wivu wa nini?

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Ukishajijua wewe ni mchepuko hutakiwi kuwa na wivu hata kidogo, tambua umepewa hisani tu! Mambo ya kumfuatilia mtu wakati ushajua ana mtu wake wa permanent ya nini! Unampigia simu usiku wa manane ili iweje? Unapekua simu yake ili iweje?
Jiangalie!
 
Michepuko mingine kama utendaji ni bomba huweza kupewa bonge la promotion na kuwa nyumba kubwa, hili si jambo la ajabu.
 
With emotions even heroes can act like i.d.i.o.t.s .....
 
Mchepuko ni hisani???? hujui kuwa mwanaume hunyenyekea kwa mchepuko kuliko nyumba kubwa. Acha kabisa hayo maneno, mchepuko ni malkia, kwa hyo hauombi unapewa.
michepuko inajua sehemu zote za starehe, nyumba kubwa yake kumbi za sherehe
Michepuko inajua mapozi ya private car, nyumba kubwa zake daladala
Michepuko inazujua shopping mall, nyumba kubwa kwake kariakoo.
Nimekusaidia tu maelezo kidogoooo.
 
Je, ni sahihi mchepuko kumfuatilia sana kwa wivu mtu ana njia kuu yake? Kumpigia simu usiku wa manane? Kupekua inbox za simu kwa nini?
 
Anakupigia anakuwa kakumiss!anapekuwa cm ili ajue kama kuna mchepuko mwingine zaidi yake!

Ndo kupiga simu usiku wa manane? Wivu kwa michepuko mingine wa nini wakati we mwenyewe ni mchepuko tu na si njia kuu yako! Mmiliki mwenye haki yake katulia nyumbani kwanini michepuko mgombane?
 
Michepuko mingine kama utendaji ni bomba huweza kupewa bonge la promotion na kuwa nyumba kubwa, hili si jambo la ajabu.

Unazungumziaje mchepuko kuwa na wivu?
 
tatizo wanaume mmeshashindwa kuwa wakweli sasa kama unajua unanitongoz niwe mchepuko kwann usiniambie mapema unasubir penz limenoga ndo unaanza visa, aseee yani nikigundua umenifany mchepuko wakati uliniambia mimi njia kuuu nahakikisha nimekuvulugia iyo njia kuu yako ili tuumie wote.
 
Kwani mchepuko hauna moyo?Wakati unamuona mchepuko labda wewe kwake ni njia kuu inabidi akabe!
 
tatizo wanaume mmeshashindwa kuwa wakweli sasa kama unajua unanitongoz niwe mchepuko kwann usiniambie mapema unasubir penz limenoga ndo unaanza visa, aseee yani nikigundua umenifany mchepuko wakati uliniambia mimi njia kuuu nahakikisha nimekuvulugia iyo njia kuu yako ili tuumie wote.

Ninayemzungumzia hapa ni yule ambaye alishaambiwa mapema na anajua kuwa yeye ni mchepuko!
 
tatizo wanaume mmeshashindwa kuwa wakweli sasa kama unajua unanitongoz niwe mchepuko kwann usiniambie mapema unasubir penz limenoga ndo unaanza visa, aseee yani nikigundua umenifany mchepuko wakati uliniambia mimi njia kuuu nahakikisha nimekuvulugia iyo njia kuu yako ili tuumie wote.

utatulia tu. namm nahakikisha huvurugi ila utalia kidogo na utakubali matokeo tu. Hivi unafikir kaz rahisi kunivurugia ndoa?
Ukiniletea vurugu zaidi nyumban utakumbana na vitasa
 
😀:thumbup:
 
Je, ni sahihi mchepuko kumfuatilia sana kwa wivu mtu ana njia kuu yake? Kumpigia simu usiku wa manane? Kupekua inbox za simu kwa nini?

Si sahihi kabasa, lakin kawaida kama mtu mnazoeana ni rahisi kujua sim anazopigiwa na mkewe, na si ruhusa kabisa kupiga sim akiwa nyumbani kwake hadi akupige yeye, na unapiga sim ya nin wakati kwa kawaida huwa anakuacha huna shida hadi awe kwake anakuwa amemaliza matatizo yako kwa siku hiyo.
Wanasema ukitaka kula na kipofu, usimshike mkono.
 
Mstari wako wa mwisho unahusika sana!
 
Back
Top Bottom