‘wewe ndiye mwanamke halisi’

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443

Mwaka 1990 wakati nafunga ndoa na mume wangu sikutarajia kwamba , ningekuja siku moja kumfumania na mwanamke yeyote. Alianza kunisimulia mama huyu, ambaye hapa ningependa mumfahamu kama mama Sikuzani. Alishusha pumzi na kisha kuendelea na simulizi yake ya mkasa uliompata muongo mmoja uliopita……………………

Huyu mwanamke alikuwa ni mama wa mtoto mmoja. Hakuwa na ndoa na kazi yake ilikuwa ni kutumwa kufanya kazi za watu pale mtaani na kulipwa kidogo. Kazi kama kuchota maji, kulimia bustani na nyingine za aina hiyo. Alikuwa ni mwanamke ambaye amejipiga mahuru, yaani hakuwa anajali sana kuhusu mwili wake wala nguo.Sifa yake kubwa ni makalio makubwa tu, lakini hakuwa na sura wala kitu kingine ambacho mtu anaweza kusema kwamba, kinaweza kumbabaisha sana mwanaume.

Mimi ni mwanmke, hivyo sijui mwanaume anavutiwa na kitu gani kwa mwanamke linapokuja suala la kujaamiana. Nakumbuka ilikuwa ni
Mwaka 2000, nikiwa nimetoka kazini kwenye muda wa saa kumi siku ya jumamosi, niliamua kutoingia ndani kwanza. Niliona nipite hadi kwenye mabanda yangu ya kuku, ili kuona kama kijana anayenisaidia kazi alikuwa amefanya kazi zake vizuri. Nilipofika kwenye banda kubwa nilikuta mlango ukiwa wazi na nilijua ni yule kijana wangu wa kazi. Sikutaka kumsumbua, nilijua yuko kazini, hivyo niliona nikabadilishe nguo na kula kwanza ndio nirudi mabandani.Lakini wakati nataka kugeuza ili nirudi, nilisikia minong’ono.

Niliamua kurudi nione ni akina nani wanaonong’ona. Nilifika mlangoni na kuchungulia bandani. Niliona nilichokuwa nataka kukiona, lakini hakikuwa nilichokuwa nimekitarajia. Hakuwa mtumishi wetu bali mume wangu wa ndoa. Alikuwa amemkumbatia yule mwanamke mchafu wa mtaa. Alikuwa anamng’ang’aniza kumvua nguo na yule mwanamke alikuwa hataki. Halafu badala ya kunong’ona, yule mwanamke aliongea kwa nguvu. ‘Hebu mheshimu mkeo we baba, ndio nini unataka kufanya. Halafu wewe afisa mzima utatembeaje na mimi. Kwanza siamini..’
Mume wangu naye aliongea kwa sauti kidogo. ‘wewe ndiye mwanamke halisi, hujipodoi, huna nywele za bandia, hunukii pafyum, unanukia harufu halisi ya mwanamke... Tunaita kuku wa kienyeji, usijali, maofisa wengi wanapenda wanawake kama wewe...’ Halafu niliona yule mwanamke akitupa kanga zake pembeni na mume wangu alianza kuhangaika kuvua shati.

Nilijihisi kama vile nimenaswa na umeme na pumzi zilisimama na nilipotaka kuwakemea nilijikuta nimekwama. Nilipojitahidi kutaka kuwafuata nilijikuta sina nguvu kabisa.
Bahati nzuri, yule mwanamke alitupa jicho mlangoni na kuniona. Alishtuka sana na kuinama na kukusanya nguo zake. Sijui zilitoka wapi nguvu zile.nilikurupuka na kwenda kumvaa yule mwanamke na kumwangusha chini, halafu nilimpiga hasa, huku mume wangu akiwa amesimama asijue la kufanya. Yule mwanamke alikuwa kipiga mayowe ya kuomba msaada, na ndipo mume wangu alipopata ujasiri wa kunishika ili nisiendelee kumtia adabu yule mwanamke hayawani.

Nilimgeuzia mume wangu kibao na kuanza kumvurumishia mangumi mfululizo, hakumudu kujibu mapigo zaidi ya kujitahidi kujikinga uso nisimtie ngeu. Kumbe siku zote nilikuwa sijui kwamba nina nguvu kiasi kile. Ilibidi kijana wetu wa kazi ambaye ndio kwanza alikuwa anarudi kutoka mjini alikokuwa ametumwa na mume wangu ili ampe nafasi ya kufanya uibilisi wake aingilie ule ugomvi na kuamua.Yule mwanamke mchafu wa mtaa alishakimbia zake na kutokomea kusikojulikana, na hata kijana wetu wa kazi hakuweza kujua chanzo cha ugomvi wetu.

Tukio lile lilikuwa ni chungu sana kwangu na sitakuja kulisahau kamwe. Bado niko na mume wangu, lakini tangu siku hiyo, amebadilika sana.

Wanaume hawajui wanacho kitaka... natural or not akiamua kukugeuka atageuka tu. Hapo alikua anamwambia yule mama hivo kwa sababu kuna kitu alikitaka kwake!

 
umenikumbusha ile story ya harufu ya fenesi! watu mna mambo nyie!
 
You have made your point Mtambuzi, ulianzia kwenye V scent sasa naona umetunga supporting story.

Girls vipara mtindo mmoja sasa! LOL
 
Last edited by a moderator:
umenikumbusha ile story ya harufu ya fenesi! watu mna mambo nyie!
snowhite
Kula fenesi kwahitaji nafasi, mchuzi wa ndimu wanitia wazimu mie............................
 
Last edited by a moderator:
Badili abia usipende ku-generalize, si wanaume wote wako hivyo. Hayo ni mawazo ya kukata tamaa na kuonyesha hujui usemacho mwanangu. Si mwanamke wala mwanaume haya mambo hutokea hasa ikizingatiwa kuwa it take two to tango.
 
snowhite
Kula fenesi kwahitaji nafasi, mchuzi wa ndimu wanitia wazimu mie............................
hahahahahhaahh mara mwataka ndimu mara asali mara barafu mara chai ya moto,mara uvuguvugu mara inukie hiliki mara iwe haijakoshwa!mwe!
mna sifa za mdudu fulani hivi ana macho makuuubwa na ulimi mreeefu!
 
Lakini Graca alisema ukiwa mjuvi kwenye 6*6 unamweka kwenye kumi na nane na hachomoki, kumbe kuna harufu ya heat tena lol....
ndo wanaume hao.......hata hawajitambui wanataka nini....headache tupu.....
 
Last edited by a moderator:
Hakuna cha harufu wala nini hapo, ni hulka tu ya binadamu kutaka kujaribu kila kitu, kwani hamjaona mke wa bosi tena mwenye cheo kikubwa serikalini anatembea na kijana anayelisha mifugo? Mbona hiki ni kitu cha kawaida sana. Hizo ndiyo weakness alizonazo binadamu, ndiyo maana akawekewa na amri ya usizini, maana hata Mungu alijua kwamba control ya binadamu ni ndogo linapokuja suala la ngono.
 

Samahani lakini!
Ila nakuona unatumia nguvu sana kujiconvise kuwa unapenda kitu natural. Why do l think that?
Apart of kuongelea sana, matendo hayaoneshi hivyo. Picha almost zote unazoziattach ni za wadada ambao wako heavily made up na studio make ups.
Ungekuwa unaweka hao natural, ningeamini kweli u r for real, na hii ni kwa wanaume wengi; nyumbani anapiga mkwala extensions lkn akimuona mdada mitaani na fake everything mimacho inamtoka.

Samahani lakini!
 
mmh! yangu macho...wanaume wengi Kipochi manyoya tu mengine ya ziada..mbishe, mkatae ila fikra yote mara nyingi ni hapo!!
 
Huyu baba ni kahaba mzoefu CD la kiume, hana cha kumsifia yule mwanamke ni alitaka tu haja zake zitimilike. Na anauzoefu wa kuhadaa wanawake, hawa ndio wale wanao tembea na watoto wao.mh!
 
There is no natural until natural is there.
Natural is not objective but rather subjective.
So everybody is natural according to his/her standards.
​

Bazazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…