Tetesi: WEWE MWANADAMU JARIBU KUJIULIZA

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
14,834
2,000
We mwanadamu jaribu kujiuliza
Ungekuwa Mungu ni nani ungemsiikiza?
Polisi wa doria au kibaka ndani ya giza?
Je ni nani angepokea miujiza?
Mlevi wa gongo au mama anayeuza?
Yote tisa ungemponya mgonjwa ndani ya machela?
Papii Kocha, Seya wangegeuka Paulo, Sila?
Au ungelala na kuzuga hutuoni mafukara?
Simba anakuomba wewe kabla ya kumuwinda swala
Swala anafanya sala umuepushe na misala
Je, ungekumbuka kuwa mbu hajala?
Ungemkumbuka Mwanaidd wa Mbagala?
Tuma anakuomba wewe kabla ya kulala
Wakati jambazi sugu huko nje anafanya sala
Anaomba Tuma alale fofofo usiwe msala
Je, ungenipa mke mwenye upendo kama Wastara?
Au ungenisakizia changu mwenye penzi la biashara?
Ungekuwa Mungu ungeshameza sumu?
Au ungeshatuchoma moto kuyakwepaa majukumu?Chorus – Mary Lucos
Jaribu kujiuliza, jaribu kujiuliza
Je, ungekuwa Mungu wooh uwooh
Je, ungekuwa Mungu wee
Je, ungelisha ndege wa angani wee?
Je. ungetupa pumzi bure wee?
Oooh wooh


Verse 2 – Kala Jeremiah
Ungeijua kesho na kesho kutwa
Ungeshuhudia mkono wa albino ukikatwa
Na mkataji akikulilia asije kukamatwa?
Ungekuwa Mungu nahisi ungeshadata
Kuna kina Mariam na Lamata
Wanataka ndoa na wachumba hawajapata
Mungu sina kazi na nataka kula bata
Je kweli ungemkumbuka yule ndege wa Tabata?
Wajane, yatima wasingechoka kukufuata
Wacheza kamari, maimamu na mapasta
Mgonjwa anaomba apone mapema
Wakati muuza jeneza alikulilia mapema
Muuguzi anasema baba huyu mgonjwa usimponye mapema
Nina shida na kiasi cha hela kwa ajili ya mama
Nahisi ungehisi tunakusakama
Kina sisi tunaotaka riziki kwa kuchana
Mwanafunzi analia mimba itolewe
Wakati mgumba anakesha macho na mumewe
Vipi sasa Mungu ndo ungekuwa wewe?
Kifaranga anatembea akikuomba wewe
Sikia maombi juu ya mwembe chakula anataka mwewe
Ungeyasikia maombi ya kichaa?
Au ungekomba pesa zote halafu ukakesha bar?


Chorus – Mary Lucos
Jaribu kujiuliza, jaribu kujiuliza
Je, ungekuwa Mungu wooh uwooh
Je, ungekuwa Mungu wee
Je, ungelisha ndege wa angani wee?
Je. ungetupa pumzi bure wee?
Oooh woohVerse 3 – Kala Jeremiah
Ungeficha siri zako kama nguo za ndani?
Au tungeona kila kitu ka daktari wa labour?
Je, ungeyasikia maombi ya kahaba
Anayesali kabla ya tendo umuepushe na miwaya?
Au mwasherati anayezuga mwanakwaya?
Ungetupa shavu kama Mungu wa Isaya?
Maana bila wewe hakuna Kala wala Jeremiah
Ungesema haya, ungewakumbuka wasukumaa na wahaya?
Vipi lugha zao zingepanda hawa wala kaya?
Vipofu wangeona? Au ungedili na vigogo?
Vipi mademu wa mjini wenye nyodo na mikogo?
Je, ungeichoma Sodoma na Gomola?
Au ndo kwanza ungenogewa na ishu za mduara?
Mamba ana njaa anataka nyumbu
Nyumbu anakuomba umuongoze mto usio na mamba
Wakulima wanalia lete mvua juu ya shamba
Dobi ndo katoka kuanika nguo juu ya kamba
Bila Mungu we siyo kitu achaa ushamba
Chorus – Mary Lucos
Jaribu kujiuliza, jaribu kujiuliza
Je, ungekuwa Mungu wooh uwooh
Je, ungekuwa Mungu wee
Je, ungelisha ndege wa angani wee?
Je. ungetupa pumzi bure wee?
Oooh wooh
Outro – Kala Jeremiah
Yeah, think twice
Natokea Mwanza
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,106
2,000
Leta na wimbo wa yule jamaa wa Mbeya sijui Abiud unaosemea "MUNGU SI ASUMANI"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom