Tetra kama nilivyosema mwanzo,upendo hauna uhusiano na ngono,halafu kupenda hakuna limit,kwamba unampenda mmoja kuliko mwingine
'
Ukishaingia kwenye hali kama hiyo ujue hauko kwenye upendo,hauko kwenye upendo kwa kuwa kanuni ya upendo haielekezi kubagua,huyu umpende kwa kiasi hiki huyu kile
'
Huyo anaejiua na yule anang'ang'ania kwenye ndoa au uhusiano unaomuumiza na kumdhalilisha,ambae ni katili kwa mwenza wake,au anavunja mahusiano hovyohovyo hawana tofauti,ni wagonjwa
'
Ukikagua utagundua kwenye malez yao kuna tatizo la upendo
'
Binadamu yoyote anahitaji upendo,akiukosa either atakuwa katili sana au atakua zezeta sana kwenye suala la mahusiano na maisha kwa ujumla
'
Ukatili utakuja pale mtu huyu atakapokua anafanya ukatili huo kwa kulipiza kisasi kwa kunyimwa upendo na wazazi au walezi wake
'
Uzezeta unakuja pale mtu huyu atakaponyimwa upendo kwenye malezi kitendo kilichomfanya akose kujiamini na ajione bila mpenzi hajakamilika na ndipo kujiua kunapokuja
'
Kumbuka aina zote za watu hao hufanya hayo huku wakiamini wako sahihi!