Wewe binafsi unaionaje JF mtu akiomba umueleze?

mzado

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
1,013
1,483
Kwema wadau,

Sio kwa lengo la kupima kukubalika au ubora wa JF bali kama passive member wa muda mrefu kidogo nimeona niulize, labda kuna namna naweza itumia kwa manufaa zaidi.

Binafsi JF kwangu ni sehemu ya kupumzikia nikitaka kukimbia uhalisia, nikiingia huwa najihisi nipo ulimwengu wa uhuru wakutoa maoni na kushiriki mijadala ni mdau mkubwa wa Habari na Hoja mchanganyiko na MMU. Kwa majira ya mchana huwa ni jukwaa la habari na hoja mchanganyiko na jioni ni MMU na hii huwa inatokea automaticaly, marachache sana huwa nahudhuria majukwaa mengine.

Jinsi naichukulia sasa ni kama vile kijiwe/maskani flani hivi yenye wadau wa kila aina, wataalam, wasomi, wajanja wajanja, na wajuaji lakini wazee wa fix na wakurupukaji hawa ndio wengi. Ni maskani ambayo ukikuta wanastori za kujenga, basi unatulia unamskiliza mtoa mada kwa makini lakini kwa tahadhari, na wadau wakianzia kuchangia tu basi kwa zaidi ya asilimia 90 kunauwezekano wakutoka nje ya mada na kuweka data za uongo kwa sifa l, labda iwe mada juu ya mapenzi na kunyanduana angalau wanaweza stick kwenye point kwa asilimia kubwa,

JF kama kijiwe chochote kina characters wake wakubwa, ambao ukikaa kwa muda kuna baadhi unaweza watambua na kujua tabiazao na kuna wafuasi wao, pia kuna wale ma-star wa msimu wanakuja wana-hit na kupotea.

JF ni sehemu bora ya kujifunza ukikutana na nyuzi makini, ambazo kwa binafsi yangu zimekua za kumulika kwa tochi. Nisehemu ya burudani na kupotezea mawazo hususani kwenye comments na kubwa zaidi si sehemu sahihi ya kuomba ushauri hususani ukiwa kwenye kipindi kigumu, asilimia kubwa ya wadau wanao comment hawajafahamu nguvu ya kile wanacho andika.

Binafsi nakipenda hiki kijiwe, lakini kama wasemavyo wadau ukiwa na akili za kushikiwa JF inaweza ikakupoteza kabisa.

Karibuni kwa maoni.
 
Jf inanifanya nijihisi nipo nyumbani hasa nikiwa huku maporini nachoma mkaa,

Sijabeba watu Jf na kuwapeleka kwenye maisha yangu halisi, yanayotokea Jf hubaki huku huku,

Napenda majukwaa ya Habari Mchanganyiko, Chitchat, Siasa, Celebrities, Ujenzi, Jf Chef, MUM na Teknolojia, naweza nisichangie ila hua nasoma,

Siwezi kuacha kuchangia mada yoyote inayohusu LGBTQI+ sababu mimi ni Mwanaharakati wa upinde wa Mvua na mada za humu hua nazitumia kama reference kwenye kazi zangu (exclusive hiyo natoa)

Miaka mi5 nyuma ningeweza kui recommend kwa watu wazima wenye akili na busara zao ila kwa sasa siweziii sababu kumejaa wajinga, matusi na wagonjwa wa akili.
 
2b102012-77d0-46d6-87cb-128265c44eb7.jpg
 
Jf inanifanya nijihisi nipo nyumbani hasa nikiwa huku maporini nachoma mkaa,

Sijabeba watu Jf na kuwapeleka kwenye maisha yangu halisi, yanayotokea Jf hubaki huku huku...
Imekaa vizuri mkuu, sema hapo kwenye uanaharakati wa upinde wa mvua sijaelewa, yaani unawaunga mkono hao wadau?

Kama ndivyo, kwanini?
 
Jf inanifanya nijihisi nipo nyumbani hasa nikiwa huku maporini nachoma mkaa,

Sijabeba watu Jf na kuwapeleka kwenye maisha yangu halisi, yanayotokea Jf hubaki huku huku...
Mumeeee wanguuuu,

JF Imejaza wagonjwa wa akili na wajinga, nimecheka mie.

Mic u sanaaaaa mume wanguu.
 
Ila upande wa App JF wamekua wazembe sana kuipa updates.. Imekua rahisi sana kuitumia JF kwenye WEBSITE au ndani ya Tapatalk kuliko app yenyewe naona bado imekaa kilocal sana imetelekezwaa..
 
Kwema wadau,

Sio kwa lengo la kupima kukubalika au ubora wa JF bali kama passive member wa muda mrefu kidogo nimeona niulize, labda kuna namna naweza itumia kwa manufaa zaidi...
Huku stendi naogopeka balaa maana natoaga nondo humu nasimulia basi naonekana bonge la wale watuuu!!!
 
Binafsi
jf Ni sehemu yangu kufunguka Yamoyoni nisiyoweza kufunguka kwa watu Baki.

Ndo maana sipendi watu wangu wa karibu waijue jf au wajue Kama Niko humu jf
 
Cha msingi humu mtu Akikukwaza hata kwenye comments.

Take it easy chukuliana kama mna have fun tu.tuseme humu.

Ni sehemu ambayo 79% ya watu wa waliomo humu tabia zao

Za kiuhalisia wanazionyesha humu ndio maana Kuna kaugumu.
Flani Jf member kukutana live ni ngumu..Jf ni sehemu poa Sana nimejifunza si kila mada itakayo anzishwa uchangie.

Nyingine kausha.

All in all ni sehemu nzuri ya kujifunza,kupata burudani, Over.
 
Kwema wadau,

Sio kwa lengo la kupima kukubalika au ubora wa JF bali kama passive member wa muda mrefu kidogo nimeona niulize, labda kuna namna naweza itumia kwa manufaa zaidi..
vijana anawatoki nje ya mada wakisoma uzi wa kula tunda kimasihara wanatoa comments ambazo zipo ndani ya mada.

lakini kwenye thread nyingine wanakucomment hii picha 👇👇👇👇

2756823_JamiiForums-1851313687.gif
 
Cha msingi humu mtu Akikukwaza hata kwenye comments..
Take it easy chukuliana kama mna have fun tu.tuseme humu..
Ni sehemu ambayo 79% ya watu wa waliomo humu tabia zao

Za kiuhalisia wanazionyesha humu ndio maana Kuna kaugumu.
Flani Jf member kukutana live ni ngumu..Jf ni sehemu poa Sana nimejifunza si kila mada itakayo anzishwa uchangie..
Nyingine kausha....!

All in all ni sehemu nzuri ya kujifunza,kupata burudani, Over.
Umeiweka vizuri sana
 
Back
Top Bottom