Werrason Ngiama Vs Fally Ipupa nani zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Werrason Ngiama Vs Fally Ipupa nani zaidi?

Discussion in 'Entertainment' started by Losambo, Apr 29, 2012.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wadau wa masebene nadhani mtakubaliana nami kuwa katika kizazi cha muziki wa Congo saizi huwezi kuzungumza bila kumtaja Werrason au Fally Ipupa.

  Hawa wote ni wakali mbaya, ukianza na Werrasson album yake ya Techno Malewa imewapagaisha wengi.

  Fally Ipupa nae ni kitisho ukichukua baadhi ya nyimbo zake kama Sopeka n.k zinazidi kumuweka juu.

  Watu hawa wanafanana kitu kimoja, wote ni wakali wa live perfomance.

  Hapo ndipo napenda tujikite zaidi. Licha ya kuwa na nyimbo nzuri lakini wanapokuwa live hutisha zaidi.

  Baada ya kuwapamba kila mmoja nani zaidi kati yao?

  Ni Werrasson Ngiama au Fally Ipupa?

  Karibuni wadau wa masebene.

  Nawasilisha.
   
 2. m

  mareche JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  fally ipupa bana du
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mareche kumbe kwako Fally Ipupa mkali. Noted.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Huyo ipupa ni mpiga makelele kama beberu, hampati werason ngiama, tena hawatii pua kwa jb mpiana mukulu!!
   
 5. ZENITH

  ZENITH JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 732
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Kweli kabisa,fally ipupa akapambanishwe na akina felix wazekwa huko,huyu werrason yupo level za akina gola,olomide na JB Mpiana.
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hakika haujamndea haki Noel Ngiama Makanda 'Werrason' kwa kumlinganisha na bwana mdogo Fally Ipupa....

  Kiukweli Werrason sio size ya Fally Ipupa,Werrason size yake ni Jean-Bedel Mpiana, Adolphe Dominguez, Paschal Poba, Felix Wazekwa, Charles Antoine 'Koffi Olomide' na wengine..Kumbuka kwamba Werrason ni mmojawapo wa waanzilishi wa bendi machahari ya Wenge Musica BCBG ambayo waliianzisha mwaka 1981 na imetamba mpaka iliposambaratika mwaka 1997...Pia kumbuka kwamba Werrason ni mtunzi wa nyimbo ambazo miaka nenda rudi haziishi utamu/hazichuji...Nyimbo kama Kala Yi Boeing,Solola Bien, Force D'Intervention Rapide, Opearation Dragon, Kibuisa Mpimpa na bila kuvisahau vibao vitamu vilivyopo kwenye albamu yake ya Techno Malewa Suit En Fin....Kwa ujumla Werrason na Fally Ipupa ni sawa na Mbingu na Ardhi mkuu ama Yanga na Barca.......

  Fally Ipupa yeye size yake(wa kuwalinganisha/kuwapambanisha naye) ni akina Ferre Gola, Bill Clinton Kalodji ,Montana Kamengana wengine....Kumbuka kwamba Fally ni bwa'mdogo ambaye ameibuliwa na Le Grand Mopao Charles Antoine Koffi Ollomide ambapo alikuwa ni mmojawapo wa wanamuzii waliounda Quartier Latin International(ambayo ilianza tangu mwaka 1986 na bwana mdogo Fally amejiunga mwaka 1999)...Alikuwa akiimba na vijana kama Montana Kamenga,Geco Mpela, Ferre Gola(baadae alihamia kwa Werrason).......Hii inaonesha ni jinsi gani Fally alivyo bwana mdogo kwa Koffi kimuziki na kiumri na pia kuheshimika kimataifa....
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakubaliana na wewe kabisa lakini Fally Ipupa kwa sasa nae kidogo anakuja kuja na wapo baadhi ya watu wanamuona yupo juu.

  Koffi kwa sasa ni kama kafulia vile, kuna kibao kimoja Cindy alikiimba ndiyo nakiona kimenyanyua kidogo. Kesho nitaweka link yake.
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mkuu umeiweka kama nilivyotaka kusema ...
  Tena hata Bill Clinton na Tutu Kalodji sio size yake bado, sema tu ho majembe nyota zao ni za kawaida pia ni ma team player...
  Fally Ipupa anaangukia huko kwa akina Ferre Golla na wakina CNN ( yule repa wa Koffi baada ya kuondoka wale Quatterettin ya wakina Suzuki) amerap kwenye ile nyimbo ya Artentant (nismehe matamshi ila kama ni mfutiliaji wa Koffi najua umeipata hiyo nyimbo)....

  Nasikitika kusema inapokuja kwenye bolingo Fally Ipupa kwangu anapata marks za chini sana....

  Ahsante mkuu kwa kunipa hizo kumbukumbu za wakongwe.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ... mie hapa nasikiliza Orchestra VEVE kibao kinaitwa yanini. huu mziki wa Kavasha ni mtamu ajabu! Akina Fally Ipupa dah just cant comment!! lkn ukiwa na time sikiliza mziki wa akina Verckys, Kiamangwana mateta, Mombasa vata, Nzaya Nzayadio! oh roho inataka kuniruka hapa nikikumbuka enzi za Kavasha!
   
 10. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Pazmanian

  Pazmanian JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 832
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 180
  werason
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Tunachanganya mambo hapa..........kuna swala la ukongwe na kuna swala la nani anafanya vizuri kwa sasa

  Kwa ukongwe wa sikunyingi na kutunga nyimbo nyingi zilizofanya vizuro ofkozi Ngiama Makanda ataukuwa juu
  Swala la nani anafanya vizuri kwa sasa ni debatable

  Kwa maoni yangu Fally Ipupa yupo vizuri zaidi kwa sasa, Fally ana management iiliyokwenda shule na anaangalia zaidi masoko ya kimataifa zaidi ya Condo na Paris
  Fally anakubalika zaidi hata nje ya Congo hasa baada ya kufanya makolabo ya kufa mtu almost all over the world.
  Fally yupo flexible ku adapt aina mbali mbali za musiki kama alivyokuwa Papa Wemba tofauti na Werrason aliyejikita kwenye bolingo original na kumfanya akubalike zaidi Congo na nchi zinazopenda miziki ya kikongo tu.
  Fally anakubalika zaidi na kizazi kipya cha dot com

  Lakini hii yote haiondoi ubora na umahiri wa Werrason isipokuwa kwa sasa Fally Ipupa ni zaidi.....maoni ynagu tu
   
 13. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nakubali uchambuzi wako sana tu,
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Narudia tena, Fally ipupa anapiga makelele jukwaani, Werason anaimba kwa ustadi mkubwa, hata kama huelewi lugha anayotumia, ustadi wa sauti yake utakuburudisha.
  Werason usipime!!!!!!
   
 15. princess ariana

  princess ariana JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2017
  Joined: Aug 19, 2016
  Messages: 4,434
  Likes Received: 5,966
  Trophy Points: 280
  fally ipupa
  lavi est belle
   
Loading...