Werema: Contracts flawed

Wakati wa Awamu ya Mwalimu Nyerere mikataba kuhusu uwekezaji katika madini iliiga misimamo ya Botswana, ambapo tulisisitiza mwekezaji awe na 50% katika mradi na serikali iwe na 50%.

Mwalimu alisisitiza kuwa madini hayaozi na yaliwekwa katika ardhi yetu na Mwenyenzi Mungu kwa manufaa ya Watanzania. Kama wawekezaji wakubwa hawataki au hawatosheki na hiyo 50%, basi tuwaachie artisanal miners waendelee na miradi yao.

Mauzo ya hawa wadogo wadogo yanakuja nchini yote, bila kubakiza asilimia yoyote ng'ambo. Hatimaye Serikali yetu iwawezeshe hawa ili tufaidike kweli kweli na maliasili yetu.

Mtindo wa kumiliki siyo chini ya 50% ya miradi ya madini unafuatwa kwa makini sana huko Botswana, na inavyofahamika, nchi hiyo imepiga hatua kiuchumi sana. Hakuna sababu sisi tusiige mtindo huo. Madini, mafuta ya petroleum au gesi haviozi.


Ndugu zangu,

Haya tunayoyasikia kutoka kwa wale waliokuwepo na kuhusika kama Mzee Mtei tuyahifadhi na kuyaweka moyoni. Ni muhimu mno!

Ardhi ni yetu, MADINI NI yetu. Mwekezaji anayo fedha. Hizo fedha zinampa 50% ya hisa, na sisi ardhi na madini yetu yanatupa 50% ya hisa zote. Lina shida gani hilo kueleweka? Na linakubalika, kama lilivyokubalika Botswana. Mengine yote ni ulaghai wa watawala wanaopokea rushwa kuidhinisha mikataba ya kiwizi.
 
Kwani Hata tulivyoingia kumekuwa na Madhara Gani kwa Watanzania? Neno Changamoto linatosheleza Mkuu!!

Mtu akichukua mali yako bila malipo hakuna madhara? Mali imechukuliwa, mazingira yamechafuliwa, malipo hakuna, kisha useme hakuna madhara? give me a break!
 
BAK: Maneneo ya Werema yanaudhi hadi basi. Anataka kuaminisha umma wa Tanzania kwamba taaluma ya sheria hapa kwetu iko nyuma sana na kwamba hakuna wanasheria wenye uwezo wa kushughulikia mikataba ikiwa ni pamoja na yeye? Mbona anashindwa hata kutoa maelezo ya nini kifanyike kurekebisha uozo huu? Atuambie basi uwezo wa wanasheria wa bongo uko wapi kwa sababu kuna manung'uniko mengi mno kuhusu nyanja hii. I hate this reasoning to the bone!!!!
 
Mtu akichukua mali yako bila malipo hakuna madhara? Mali imechukuliwa, mazingira yamechafuliwa, malipo hakuna, kisha useme hakuna madhara? give me a break!

Ndio maana Mkuu Nikasema kwa Tanzania lolote linawezekana!! na neno changamoto (Changa la Macho) wanalichukulia kama ndio solution ya kuwahadaa watu!! Naona tupo Pamoja!!
 
Back
Top Bottom