Wenzetu wameweza... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenzetu wameweza...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mpenda pombe, Oct 1, 2012.

 1. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Wenye simu ghushi mashakani Kenya

  1 Oktoba, 2012 - Saa 09:50 GMT

  Simu ya rununu
  Wateja milioni 2.5 wa Simu za rununu leo wamejipata mashakani baada ya Tume ya Mawasiliano nchini Kenya kuzimasimu ghushi.

  Zoezi hilo la kuzima simu lilianza kutekelezwa usiku wa manane na linalenga kukabiliana na uingizaji wa simu bandia, suala linalohujumu juhudi za kuimarisha usalama.

  Hatua ya kuzima simu ghushi na ambayo imethibitishwa na kampuninne za huduma za simu nchini humo, inafuatia agizo la tume ya wasiliano nchini humo ambayo inataka kukabiliana na biashara haramu, wizi wa haki miliki na tisho la usalama.

  Afisaa mkuu mtendaji wa tume hiyo,Francis Wangusi, alielezea kuwa hatua ya kuzima simu hizo, ambayo ilikuwa imeakhirishwa mara tatu iliweza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo.

  Tume hiyo haijashirikiana na kampuni za huduma za simu kuzimasimu ghushi tu bali pia simu ambazowateja wake hawajasajiliwa.
  Hatua hii imesababisha hasare kubwa kwa kampuni za simu.

  Hata hivyo tume ya CCK, imetenga bajeti ya pesa itakazotumia kugharamia hasara ya kampuni za simu ingawa wateja wa simu hizo hawatapata fidia yoyote.

  Kampuni ya Safaricom, ambayo ina wateja wengi zaidi ya kampuni zoteza huduma za simu za rununu nchiniKenya, imezima simughushi, 670,000 katika masaa 15 pekee.

  Kampuni ya Airtel Kenya nayo imezima simu 100,000 huku yuMobile ikizima takriban simu 45,000. Kampuni ya Telkom Orange imezima takriban simu 20,000.

  Nani wa kulaumiwa kwa kuingiza nchini simu bandia?
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono ili na wateja nao waone uchungu.
   
Loading...