Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Mbunge wa Jimbo la Msalala mkoani Shinyanga, Iddi Kasimu amewapatia usafiri wa baiskeli bure wenyeviti wa serikali za vijiji 92 vya halmashauri ya Msalala, utakaowasaidia kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao zenye thamani ya TSh. Milioni 23.
Baiskeli hizo zimekabidhiwa leo Mei 4, 2025 na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Kawaida, baada ya kuwahutubia wananchi wa kata ya Bugarama halmashauri ya Msalala na kuwaeleza namna serikali inavyotekeleza miradi inayogusa maisha ya wananchi huku akiwasisitiza kuilinda na kuitunza ili iwanufaishe.
Amempongeza mbunge kwa kuona umuhimu wa kuwapatia usafiri wenyeviti wote wa serikali za mitaa kwa lengo moja la kufautilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwataka wengine kuiga mfano huo ili kuwa pamoja na viongozi wao ambao kwa asilimia kubwa wako karibu na wananchi.
"Ninakupongeza sana kwa hatua hii ya kuwafikia wenyeviti wa serikali za mitaa na kuwapatia usafiri, tangu nimeanza ziara yangu ya siku 10 sijakutana na tukio la namna hii; Wenyeviti tumieni baiskeli hizo kwa malengo yaliyokusudiwa" ameongeza Ali.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025