Wenyeviti wa serikali za mitaa nchini wametoa masaa 24 kwa katibu mkuu wa TAMISEMI kuwaomba radhi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Wenyeviti wa serikali za mitaa nchini wametoa masaa 24 kwa katibu mkuu wa TAMISEMI kuwaomba radhi na kutengua agizo la kuwataka kukabidhi mihuri kwa watendaji wa mitaa na kumtaka Waziri mwenye dhamana kutoa kauli ndani ya siku saba kuhusu mgogoro huo.

 
Wenyeviti wa serikali za mitaa nchini wametoa masaa 24 kwa katibu mkuu wa TAMISEMI kuwaomba radhi na kutengua agizo la kuwataka kukabidhi mihuri kwa watendaji wa mitaa na kumtaka Waziri mwenye dhamana kutoa kauli ndani ya siku saba kuhusu mgogoro huo.


wanahamaki nini sasa kama sio wamegeuza mihuri dili. warudishe mihuri mambo ya ovyo na mihuri hiyo ndio mengi. hizo shughuli wanazodai kufanya ni kazi za mtendaji. wanatoa mimacho tu. watakaogoma wapo watendaji. lazima wabakie kama wenyeviti sio kuingilia kazi za mtendaji. watendaji wengi wanazurura au kufanya shughuli binafsi huku wanakula mshahara wa serikali. sehemu nyingi hakuna cordination mw'kiti na mtendaji kila mtu anapika dili zake wanaotaabika ni wananchi.
 
Hapo sasa ndiyo ngoma inogile......

Siri ya CCM kupata ushindi mbalimbali hapa nchini unatokana na hao wenyeviti wa serikali za mitaa katika kile kinachoitwa kampeni ya nyumba hadi nyumba.

Sasa kama kawaida yake serikali ya awamu ya 5 ni kutoa matamko ya kukurupuka bila kuzingatia impact ya hayo matamko hayo.

Ni dhahiri wakati TAMISEMI wakati wanatoa tamko hilo kwa 'maagizo' toka juu, walikuwa wanadhani wanawakomoa wapinzani.........

Sasa hata wenyeviti wa mitaa wa CCM nchi nzima nao wamekuwa kitu kimoja na wenyeviti wa mitaa wa vyama vya upinzani, kuitaka TAMISEMI iwaonbe radhi ndani ya saa 24 kwa kuwaambia wao wenyeviti wa serikali za mitaa wanafanyia dili hiyo mihuri......

Sasa kazi kwao wakubwa wa TAMISEMI, waamue kusuka au kunyoa.......
 
Rdishen bwana mmefnya ndio dli hyo mhur unamkt mwkit ana ktamb mtnda modo kw kla hla za mgumash
 
Kama hawana maslahi binafsi na hiyo mihuri wana ing'ang'ania ya nini? warudishe wananchi wakikosa huduma ya huo muhuri kwa muda muafaka basi watailamu serikali si wao, hawa jamaa nao wana yao tu., waache wanaotakiwa kugonga hiyo mihuri wagonge, .
 
Kwani Kama hiyo mihuri inafanyiwa Dili na Wenye viti,hao makatibu kata wakipewa hawataifanyia dili?Hapa cha kujiuiliza nu Kwa nini Wenyeviti hawanaga mishahara wakati wabunge,madiwani wanajilipa.Hawa Wenyeviti hupata malipo yao Kwenye hizi mihuri.Shame.
 
Ni busara kwa hawa wenyeviti wa mitaa kunyang'anywa hiyo mihuri kwani ndio inawafanya wafanye maamuzi ya kitapeli yanayowaumiza wananchi!! Watendaji ndio wakae na mihuri kama wenyeviti wakigoma kuirudisha basi wajiuzuru na wengine watachukua nafasi zao!! Kazi wanayofanya ni ya kujitolea kuongoza jamii na haihitaji malipo ya mshahara; it is not a full time job!! Sheria pia iweke wazi kuwa wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa wawe ni wakazi wa mitaa hiyo ambao wanamiliki nyumba katika mitaa ; kwani baadhi ya wajumbe ni walinzi wa nyumba na sio wamiliki!!!
 
Kwani Kama hiyo mihuri inafanyiwa Dili na Wenye viti,hao makatibu kata wakipewa hawataifanyia dili?Hapa cha kujiuiliza nu Kwa nini Wenyeviti hawanaga mishahara wakati wabunge,madiwani wanajilipa.Hawa Wenyeviti hupata malipo yao Kwenye hizi mihuri.Shame.
Not shame anyhow, kwani wakati wanagombea nafasi hizo hawakujua kuwa hazina mishahara?na leo unanapowatetea wapate malipo nje ya kanuni yaani kiujanja ujanja kupitia mihuri hiyo atakayeumia ni nani kama sio mwananchi wa kawaida maana hakuna mwongozo wowote ulio rasmi wa tozo kwa huduma bali kila mmoja hutoza kwa mujibu wa njaa yake.
 
Back
Top Bottom