Wenye watoto kutoruhusiwa kufunga ndoa kanisani wakiwa wamevaa Shela

HII SASAI TASABABISHA MIGOGORO MAKANISANI.

KWANI NI MSTARI WA NGAPI UNAOSEMA HIVYO KUHUSU SAKRAMENT YA NDOA??????

"NIMEFUNUA VITABU VYOTE, NIMEPEKUA KURASA ZOTE, KULITAFUTA ANDIKO MIMI SIKULIONA.
NI WAPI PALIPO ANDIKWA, TAMKO HILI LA KKKT, MIMI SIKUPAONA.

FUNGUA MACHO EE NDUGU, FUNGUA MACHO. GIZA NENE LINATANDA, FUNGUA MACHO.
SHERIA YA UPANDE MMOJA, FUNGUA MACHO. MBONA MWANAUME HATAJWI, FUNGUA MACHO.
JE, MWANAUME AKIWA NA MTOTO WA NJE, FUNGUA MACHO, HAPO SHERIA YASEMAJE, FUNGUA MACHO.
............................."


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ningeelewa zaid kama wangesema 'washirika waliozaa pamoja' maana je kama mwanamke aliwahi kuzaa na mtoto yuko kijijini, au mwanaume naye ana mtoto tayari, wakakutana kila mmoja ana mtoto, wtakataliwa kwenda madhabahuni, najaribu kutafakari, dhana ni kuishi kinyumba au kuzini maana kuzini si lazima uzae, kuna watakaowakubalia waende madhabahuni kumbe na wao kila weekend huishi kinyumba, comes weekday kila mmoja karudi kwake. Au tafsiri ni kuwa waliozaa wamezini zaidi au wameonesha ushahidi wa kuzini...nawaza kwa maandishi! nisaidieni!
 
Kwa hili itabidi muinvent "electronic virginity test" kwa genda zote, uzinzi si uzazi, bikira hamna kabla ya ndoa usipande madhabahuni. Only then mtakuwa fair!..tufafanulie pia 'kitubio' au 'maungamo' yanaplay part gani kwenye mchakati huu kimaandiko tafadhali!
 

JE NA MWANAUME NAYE ATAPIMWAJE??? AU NI SHSERIA INAYOHUSU WANWAKE TU AMBAO WANAZINI KABLA YA NDOA.

NDIO MAANA HATA YESU ALISEMA "....ANAYEJIONA KUWA HANA DHAMBI NA AWE WA KWANZA KURUSHA JIWE KWA HUYU MWANAMKE...."; " ....USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA...";

KWA MTAZAMO WANGU BADO KUNA DOSARI KATIKA TAMKO ILI AU LABDA KAMA MLETA MADA HAJAIWEKA KAMA ILIVYO TANGAZWA.
 
Soma vizuri, nimetumia 'invent' na pia nimesema genda zote!..tafakari!
 
Soma vizuri, nimetumia 'invent' na pia nimesema genda zote!..tafakari!

Wewe upo vizuri hakuna shaka; hofu kwa hilo tamko ambalo limetaja mwanamke tu. je, na sisi wanaume tunaruhusiwa endapo tuna mtoto????

Au mleta mada amelinukuu tamko vibaya???
 
Wewe upo vizuri hakuna shaka; hofu kwa hilo tamko ambalo limetaja mwanamke tu. je, na sisi wanaume tunaruhusiwa endapo tuna mtoto????

Au mleta mada amelinukuu tamko vibaya???
Nahisi hii mada ni mtambuka..aliyeileta angeidetail zaidi na kuweka wazi vipengele vyote ikiwemo 'maungamo/kitubio'
 




Mwanamke anazaa peke yake?? Hapo wamechemka , kwa maoni yangu Kanisa kama kanisa halitakiwi kuhukumu badala yake linatakiwa kuwarudisha waumini kwa Mungu anaye toa hukumu ni MWENYEZI MUNGU PEKEE... huyo alietoa hilo tamko akajitathmini vizuri.
Kupata ujauzito sio dhambi ni Baraka toka kwa Mungu, ikitokea mwanamke ni mjamzito inatakiw arudishwe kundini ili asipotee.

Ukiangalia kwa kina ndoa nyingi za siku hizi zinafungwa tu na sio Harusi, ninavyofahamu harusi inafungwa kwa watu ambao hawajawai kukutana kimwili kwa wote wawili (wawe mabikira) je ndoa zetu za sasa zinafungwa na mabikira watupu???

Labda waseme kuanzia sasa hatutafungisha tena harusi bali "TUNABARIKI NDOA ZA WAUMINI" maana wote walisha shake well before use.
 
huu uzi unanichanganya kweli nimegundua kuwa mchumba wangu ni mama wa mtoto mmoja yeye na familia yake wakati nachumbia hawakuniambia kuwa mwenzangu anamtoto afu bimkubwa wangu ndo kajua ukweli kabla yangu
 
sio kudanganyana, nimetaka kuonyesha tu thinking capacity yao ilivyo ndogo kwa ku base kwenye mambo yanayoonekana kwa macho na kusahau yasioonekana kwa macho ya kibinadamu
Nikuhurumia hiyo unayoona ndio busara zako ni upumbavu mbele.Neno linasema hekima ya mwanadamu ni upumbafu mbele za Mungu.

Hawafanyi hayo kushindana na mtu lengo ni kutuhimiza tuache uasherati na uzinzi, Mimi na wewe kama upo huko tuache nafai zipone.

Huuuu nani uwakejeli na kuwaita watumishi wa BWANA akili ndogo? . Kwanini uliye na akili Kubwa usiende kanisani Kufundiaha.

Chunga kauli zako unajiona mwenye hekima mpaka kuwadharau watumiahi .

Neno linasema ni heri kufingiwa jiwe LA kusagia nafaka na kutoswa baharini kuliko...........

Neno la
 
Hao wachache kwa uchache wao hata hawajulikani...i was devoted Christian tokea utotoni ila kadiri nilivyozidi kukua kiumri na kujua reality ya kinachofanyika na hawa viongozi wa kiroho kwa kivuli cha kanisa basi nikakataa kuwa mnafiki...
Nikusaidie kitu kimoja kama unaona kuna sehemu wapo unaoita makanjanja Mimi na wewe ndio tunajukumu LA kuifundisha Kweli.

Neno linasema enendeni duniani mkawafanye kuwa wanafunzi wangu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.
Hii ndio kazi yetu kaka usikwepe hilo
 
Kueneza dini siku hizi ni kazi kama kazi zingine...hatukuitwa wote kuifanya kazi hiyo!
 
Hapo watasababisha wimbi la watoto wanaopelekwa kwa bibi kufichwa kuongezeka ili watu wafunge ndoa kwa raha zao
 
Makanisa mengine na yenyewe ni wanga tu.

Kama watu walipendana hadi kufikia hatua ya kuzaa pamoja, kanisa linawakatalia nini?

Ndio maana huwa nafikiri dini si muhimu kwa maisha ya watu.
Mkuu hujalazimishwa waweza kwenda "bomani" hakuna tabu kabisa.
 
Kueneza dini siku hizi ni kazi kama kazi zingine...hatukuitwa wote kuifanya kazi hiyo!
Kwani wewe unadhani kueneza mpaka uwe Mch. ? Hata katika eneo lako la kazi matendo yako tu yatawaponya wengine na kumtukuza Mungu alie hai.
 
huu uzi unanichanganya kweli nimegundua kuwa mchumba wangu ni mama wa mtoto mmoja yeye na familia yake wakati nachumbia hawakuniambia kuwa mwenzangu anamtoto afu bimkubwa wangu ndo kajua ukweli kabla yangu
Piga chini huyo fasta atakuja kukuzingua!!!
 
Kanisa limekurupuka, wanawake wengi hawapendi kupata watoto nje ya ndoa lakini wanarubuniwa kwa namna mbali mbali na wanaume. Cha kushangaza Kanisa limeamua kuwabagua wanawake pekee yao na kuwa kimya kuhusu wanaume wenye watoto nje ya ndoa.

Kwa mjane ndiyo rahisi zaidi, ndoa inabarikiwa tu, kwa sababu tayari alishakuwa na ndoa ila mwenza kafariki...
 

Basi ndoa zote zitakuwa za kubariki tu sio kufunga maana asilimia kubwa wameshakutana kimwili....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…