Wenye watoto kutoruhusiwa kufunga ndoa kanisani wakiwa wamevaa Shela

Kanisa limekurupuka, wanawake wengi hawapendi kupata watoto nje ya ndoa lakini wanarubuniwa kwa namna mbali mbali na wanaume. Cha kushangaza Kanisa limeamua kuwabagua wanawake pekee yao na kuwa kimya kuhusu wanaume wenye watoto nje ya ndoa.

Ndiyo maana nikasema... iwekwe sheria kwamba mwanamke atakayepata mimba kabla ya ndoa ni lazima afungishwe na huyo huyo aliyemtia mimba... kuwakamta wanaume wanaokataa mimba...
 
Mbona mnaosali mnapelekeshwa sana kama ng'ombe.
Wachungaji wengine wanasema hivi na wengine wanasema vile lakini unakuta swala ni moja.
 
Nikusaidie kitu kimoja kama unaona kuna sehemu wapo unaoita makanjanja Mimi na wewe ndio tunajukumu LA kuifundisha Kweli.

Neno linasema enendeni duniani mkawafanye kuwa wanafunzi wangu na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.
Hii ndio kazi yetu kaka usikwepe hilo
Direct question; wewe umeoa ukiwa bikra? kama sivyo, je hapo ulipo wewe ni bikra? na kama sio na hujaoa uko kundi gani siku ya harusi yako!?
Majibu honest tafadhali!
 
Wapime na bikra kabisa
Sio wanawaonea watenda dhambi wachache na kuwaacha wazinifu wengi wakifunga ndoa
 
Nikuhurumia hiyo unayoona ndio busara zako ni upumbavu mbele.Neno linasema hekima ya mwanadamu ni upumbafu mbele za Mungu.
Hawafanyi hayo kushindana na mtu lengo ni kutuhimiza tuache uasherati na uzinzi, Mimi na wewe kama upo huko tuache nafai zipone.
Huuuu nani uwakejeli na kuwaita watumishi wa BWANA akili ndogo? . Kwanini uliye na akili Kubwa usiende kanisani Kufundiaha.
Chunga kauli zako unajiona mwenye hekima mpaka kuwadharau watumiahi .
Neno linasema ni heri kufingiwa jiwe LA kusagia nafaka na kutoswa baharini kuliko...........
Neno la
tehe tehe tehe YES akili zao ndogo tena sana, kuna njia zingine za busara zaidi za kuhimiza kuacha uasherati/uzinzi than hiyo waliyoitumia IQ zao ndogo sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Mkuu hujalazimishwa waweza kwenda "bomani" hakuna tabu kabisa.
Mademu wanaotoa mimba wanafungishwa ndoa maana hawajazaa........Walioleta uhai duniani wanakataliwa,..........we unaona ni sawa hivyo?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
tehe tehe tehe YES akili zao ndogo tena sana, kuna njia zingine za busara zaidi za kuhimiza kuacha uasherati/uzinzi than hiyo waliyoitumia IQ zao ndogo sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Ubarikiwe
 
Lakini kiuhalisia... Siyo poa kabisa mnakaa miaka kumi uchumbi watoto wanne mnazaa alafu mnaenda kufunga ndoa kwa mwbwembwe kabisa... Siyo poa.. Mkiamua kuzaa maana yake mshajihalalisha wenyewe... Ndiyo iwe imetoka hiyo...

Naona ingeongezwa kabisa na kama ukitaka kufungishwa ndoa.. Lazima iwe na mtu uliye zaa nae...
*Tumechoka na michango ya harusi za wenye watoto eti haruc wakati mmebanjuana weeeee sasa mnataka kitchen part na haruc ya nn? Simwendelee tu kukunjana hivo hivo*
 
Nadhani tatizo hapa si shela kwa sababu shela ni nguo tu cha msingi ni maadili ya kanisa! Wafuate maandiko kwenye Biblia yanasemaje kuhusu hilo jambo.
 
hapo wameleta ubaguzi, wangesema hawafungishi ndoa kwa wanawake wasio bikira hapo ningeona sawa. kwasababu kuna wengine wamefanya uzinzi na kuishi pamoja muda mrefu sana kwa siri lakini bahati tu mbaya hawakulengesha mimba na kuzaa. ajuaye kipimo cha wingi wa dhambi ni Mungu, na jambo hilo lipo sirini. wanaenda kimwili sana hawa jamaa.

pia, hawajui maana ya kufunga ndoa, hiyo ni civil issue, issue ya kiserikali, yule mchungaji anapofungisha anakuwa amevaa mikoba ya msajili wa ndoa ambaye ni mfanyakazi wa serikali, hivyo kufungisha katikati ya ibada si sahihi sana pamoja na kwamba ni uamuzi wao. ujue mchungaji hafungishi ndoa hadi awe delegated power na msajil, la sivyo ndoa zote zilitakiwa zifungwe na msajili wa ndoa kule RITA.

Ni kweli kabisa , ndoa ni za kiserikali na wale ni mawakala wa serikali, ndio maana sio kila shekhe au mchungaji au padre anaweza kufungisha ndoa. Watu watahamia kufunga ndoa wilayani sababu ya vikwazo visivyuokuwa na kichwa wala miguu.
 
kipind hiki tumekuwa na tatizo kubwa sana la usingle mam.Tabia hii ya kuzaa watoto nje ya ndoa ndio hupelekea usingle mama.nahis kkt wameamua kubuni kitu kinachoweza kuwapa pressure waumin wake ili wawe makini na ngono zembe.
USINGLE MAM N JANGA NA UNAFFECT SANA WANAWAKE BCZ SINGLE MAMS EVERYWHERE.mwanamme anatia mimba af anaoa mwanamke mwingine.
 
Back
Top Bottom