Wenye Ulimwengu

Wenye Ulimwengu

josephdeo

Member
Joined
Nov 23, 2015
Posts
96
Reaction score
208
"Joseph mwanangu tumenzingirwa na watu nje ya nyumba yetu wakiwa na lengo la kutuua!".

"Wanataka kuwaaua...kivipi!...kwanini?!. Nini sababu?..". Maswali yalinitoka mfulilizo kwenda kwa baba yangu. Aliyenipigia simu usiku wa manane.

"Ni lile lile la kila siku. Naona sasa wamedhamiria kabisa kutekeleza yaliyokuwa maneno kwa vitendo".

Usingizi ukakata na kukumbuka kuwa takribani wiki mbili mzee wangu alikuwa akiniambia ya kuwa. Kuna watu wanamtuhumu ni mchawi.

Yalikuwa maneno tu ambayo wote tuliyapuuza na kamwe sikutarajia ya kuwa bado jamii yetu ilihudumu kwenye mila za kizamani. Ukuaji wa teknolojia na kasi ya maisha ilinifanya niamini kuwa mambo yale yangesalia kuwa kama tetesi tu na sikujua yangefikia huko.

Nikanyanyuka toka kitandani na kuangalia saa iliyokuwa ubavuni mwa kitanda changu. Ilikuwa saa saba na dakika arobaini na tano usiku. Sikuwa nimekata simu na nilimsikia kwa mbali baba akizivuta pumzi nyingi kwa nguvu kisha kuzitoa nje.

Kisha kwa sauti ya chini akaniambia. "Nasikia harufu ya petroli nje ya nyumba mwanangu inaonekana wanataka kutuunguza ndani!".

Mapigo ya moyo yalianza kwenda nje ya mpangilio, pupa nazo zikanijaa na mwili ukaanza kunitetemeka kwa woga.
 
Unawezakupata muendelezo wa riwaya hii kupitia group hili la WhatsApp bure kabisa...

Au tuma ujumbe kwenye namba hii ili iwe tukuunge... +255 655 500 516
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom