Wenye ufahamu na soko la miwa Dar

Wenye ufahamu na soko la miwa Dar

Extrovert

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2016
Posts
72,433
Reaction score
191,695
Wadau kwema,
Nipo katika mchakato wa kufanya utafiti juu ya soko la miwa kwa hapa Dar es salaam. Kuna mambo ambayo ningependa kuyafahamu kwa wale wenye uzoefu na ufahamu mtakuwa msaada sana.
1.Mbegu gani ya miwa gani iko na demand sana sokoni.

2.Utokaji wa mzigo kwa muda, mfano ndani ya week mauzo yakoje kwa uuzaji wa jumla.

3.Bei halisi ya miwa kwa reja reja ina range katika shilingi ngapi kwa muwa mmoja?

4. Soko kuu la miwa liko wapi kwa jiji la Dar es salaam. Mf.Manzese ni soko kuu la ndizi, Ilala Boma soko kuu la nazi. je miwa ni wapi ambapo naweza shushia mzigo?
 
Sawa lakini kwa kuuliza hivyo hapa hutopata taarifa sahihi, watu wengi waliokuwa masokoni hawashindi mitandaonj
Nakubali nilionge na mtu wa sterio akasema wao hawana soko la miwa labda tandika. napo kucheki ikawa hola.Ndio maana nimekuja uliza huku
 
Wadau kwema,
Nipo katika mchakato wa kufanya utafiti juu ya soko la miwa kwa hapa Dar es salaam. Kuna mambo ambayo ningependa kuyafahamu kwa wale wenye uzoefu na ufahamu mtakuwa msaada sana.
1.Mbegu gani ya miwa gani iko na demand sana sokoni.

2.Utokaji wa mzigo kwa muda, mfano ndani ya week mauzo yakoje kwa uuzaji wa jumla.

3.Bei halisi ya miwa kwa reja reja ina range katika shilingi ngapi kwa muwa mmoja?

4. Soko kuu la miwa liko wapi kwa jiji la Dar es salaam. Mf.Manzese ni soko kuu la ndizi, Ilala Boma soko kuu la nazi. je miwa ni wapi ambapo naweza shushia mzigo?
4. Soko la Miwa kwa Dar lipo soko la Tandalee

Watu wote huchukulia hapo!!
 
Binafsi huwa nakutana na Changamoto kama zako nikiwa natafuta taarifa mbalimbali, na vile Waafrica sio kama Wazungu mambo mengi hayako wazi sana mtandaoni hats kwa watu wanaojua.....

Manzese hapo hapo kuna soko kubwa la Miwa, Wafanyabiashara wengi wanaoleta miwa toka Mikoani hushusha hapo, na wateja wakubwa wa miwa ni wale wanaokamua Juice.

Ni ngumu kujua Bei ya Muwa mmoja mmoja, binafsi najua bei ya jumla pale SOKONI ni 7,000 mpaka 10,000 kwa Mzigo wa Muwa, bei hupanda na kushuka kutegemea na Demand.

Mzigo mmoja wa Miwa unakua na Miwa 25 mpaka 40 ikitegemea na Ukubwa wa Miwa.

Kwa uchache hivyo ndo najua, na nilifanya research miezi michache ilopita coz nlikua interested na Biashara ya kuleta Miwa kwa jumla....
 
Back
Top Bottom