Wenye tabia ya ku flash vifaa vya mawasiliano watahadharishwa mara moja

Jay Gees

Member
May 8, 2016
29
16
Serikali imewataka wauzaji wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi (mobile devices) kuacha mara moja tabia ya kubadilisha namba tambulishi (‘kuflash’) za vifaa hivyo kwani watakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 au faini isiyopungua Sh. milioni 30 au vyote viwili.

tcra.jpg


Kauli hiyo imetolewa na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

“Namba tambulishi (IMEI) za vifaa vyote vya mawasiliano ya mkononi ambavyo vimeibiwa,vimeharibika,kupotea au visivyokidhi viwango vya matumizi katika soko la mawasiliano havitaruhusiwa kuunganishwa kwenye mitandao ya watoa huduma ifikapo tarehe 16 June 2016, “alisema Mungy.

Akizungumzia kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya simu zote zisizokidhi viwango, Mungy alibainisha kuwa idadi ya simu hizo imeshuka kutokana na elimu ambayo wameitoa katika mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema lengo la elimu hiyo kwa umma ni kujenga uwezo kwa wananchi kutambua simu zisizokidhi vigezo kabla ya kufika ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.

Mungy alifafanua kuwa uchambuzi wa IMEI unaonyesha kuwa hadi Februari,2016 idadi ya namba tambulishi ambazo zilikuwa hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia tatu ambapo namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 18 na simu halisi zilikuwa sawa na asilimia 79.

“Kwa mwezi Machi 2016 ulionyesha kuwa Idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango ni asilimia nne, na idadi ya zile zilizonakiliwa zilikuwa sawa na asilimia 13 ambapo uchambuzi huu umehusisha taarifa za kampuni zote za simu nchini,’’. alifafanua Mungy.

Aliongeza kuwa matokeo hayo mazuri ni matunda ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya mamlaka hiyo, Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Tume ya Ushindani (FCC),kampuni za simu, pamoja na wadau wengine katika kuelimisha umma juu ya uhakiki wa simu walizonazo ikiwa ni pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua simu ikiwemo kuzihakiki ubora wake.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Usimamizi wa Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Injinia Gabriel Mruma amesema kuwa ni vyema Watanzania wakajenga utamaduni wa kununua simu zenye ubora kuepuka usumbufu wakati Tanzania inapoelekea ukomo wa matumizi ya simu bandia.

TCRA ina dhamana ya kusimamia shughuli za mawasiliano ya Kielektroniki na Posta hapa nchini.

Kuwepo kwa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2011 kumewezesha kutekelezwa kwa mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano vya mkononi.

Mfumo huu wa kielektroniki ulizinduliwa tarehe 17, Desemba 2015 na unahifadhi kumbukumbu za namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano vya mkononi kwa lengo la kufuatilia namba tambulishi za vifaa vilivyoibiwa,kuharibika au kupotea,
 
Hapa nionacho ni wamezidiwa kete na wajanja, simu FEKI zinarudishwa sokono na zinapiga kazi kama kawa.
 
Oyoo vile visimu vyetu feki ni mwendo wa kuflash tu sasa au ndo taanza kutaftana na tcra kwa tochi GottoloveU wahi hapa uskie siri ya urembo
 
Kwa hyo tukaibe au &*&$$#%&*&&

Hili linchi linakuwaje aisee
 
Huyu nae katuchosha bana,Imei imeia...
Kila ninapomuangalia huyu meneja mawasiliano wa TCRA bwana Innocent Mungy uwa namfananisha sana na yule Mohammed Saeed al-Sahhaf almaarufu kwa jina la "Comical Ali" aliyekuwa waziri wa habari wa Iraq kipindi kile cha uvamizi wa Marekani mwaka 2003.

Mungy amekuwa akijitahidi sana kwenye vyombo vya habari kutetea unga wake na mwajiri wake TCRA tangu kipindi kile cha kuhamia ving'amuzi vya digitali na sasa simu feki lakini matokeo yake asilimia fulani isiyobezwa uwa ni kinyume na alichokuwa anaaminisha watu wakati wa kampeni za kuhamasisha. Ni aibu kwake binafsi na mwajiri wake. Je anastahili kuitwa Comical Mungy?
 
Mjomba kabugi... Maana halis ya kuflash co kubadil imei.. Ni kuweka system files nyngine zenye uzima ili kufufua simu... Yan design kuflash choo. Suala la kubadili
Imei ni internationally illegal (so kwenye hili naunga mkono hoja) ila wasichojua ni kwamba wahuni wana njia za kubadili imei ambazo ni un-traceable... By d way naunga mkono tcra
 
Kila ninapomuangalia huyu meneja mawasiliano wa TCRA bwana Innocent Mungy uwa namfananisha sana na yule Mohammed Saeed al-Sahhaf almaarufu kwa jina la "Comical Ali" aliyekuwa waziri wa habari wa Iraq kipindi kile cha uvamizi wa Marekani mwaka 2003.

Mungy amekuwa akijitahidi sana kwenye vyombo vya habari kutetea unga wake na mwajiri wake TCRA tangu kipindi kile cha kuhamia ving'amuzi vya digitali na sasa simu feki lakini matokeo yake asilimia fulani isiyobezwa uwa ni kinyume na alichokuwa anaaminisha watu wakati wa kampeni za kuhamasisha. Ni aibu kwake binafsi na mwajiri wake. Je anastahili kuitwa Comical Mungy?

Mkuu umenikumbusha Waziri wa Sadam Hussein, alikuwa jasiri na kiburudisho tosha - ndege za vita za adui zinadondosha mabom kwenye viunga vya mji wa Bagadad yeye anasema hizo ni radi tu ni ngurumo ya mvua! Bahati nzuri nasikia alipata kazi huko Quatar kama mtangazaji wa TV.

Linapo kuja suala la Mungy wa TCRA nafikiri ni vyema ajihusishe zaidi na masuala ya PR lakini katika hoja za kiufundi awachie Technical Guru wa TCRA wawe wasemaji wakuu siyo yeye - siyo vizuri kujifanya a jack of all trade.
 
Miaka yote mlikuwaga wapi kuanzisha huu utaratibu msituchoshe hili zoezi ni gumu hata upande wenu vilivile si unaona mnavyotisha watu.Mtazima simu chache sana na mpaka usawa huu nyingi zinafanya kazi na ni feki.
 
Hawajui maana ya kuflash simu, imei nyingi za simu origal hasa samsung zime/zina corrupt, pia imei za simu zenye mtk cpu uki restore simu yako ama factory reset zina ondoka hapa nataka kuongelea kuhusu imei repair/rebuild and change ni kosa kisheria dunian kote kubadili imei ila una ruhusiwa ku repair ama rebuild imei
 
Back
Top Bottom