Wenye nyumba na kutolipa bili za umeme na maji

Apr 3, 2016
67
26
jamani kuna tabia imejitokeza sasa wenye nyumba wengi hawalipi bill za umeme yaani anachangisha hela kama chumba uwepo usiwepo utalazimika kulipia kwa mwezi, yaani unalipa kama mkataba wa nyumba.

Pili ukiangalia mzunguko wa mwezi unakuta mpaka wote muishe yeye huwa hatoi hela maana tarehe moja hudai hela, juzi kuna rafiki yangu alifukuzwa saa sita mchana kisa alikuwa kasafiri kama siku 28 hivi akapigiwa simu na mwenye nyumba kuwa anatakiwa atume hela ya umeme ya mwezi yule rafiki akahoji mbona sipo nalipia nini na huyo rafiki alikuwa na kitanda tuu na pasi, baada ya hilo swali akajibiwa kuwa anatakiwa alipe kama kodi ya nyumba shilingi 25000 kwa mwezi yule rafiki akarudi, akaenda kukaa kwa ndugu yake ili amalizie hizo siku mbili ili mwezi uishe aje alipe mpya.

Alivyorudi tarehe moja mwenye nyumba kaja na mjumbe kuwa unatakiwa uondoke ufungashe sasa ivi na hela yako iliyobaki ya miezi mitatu akapewa na mjumbe akamkata hela ya mjumbe ishirini, na hela ya umeme ya mwezi ambao hakuwepo, na mwingine wa anaouanza upya ilikuwa saa sita mchana kwa bahati nzuri akaahangaika siku hiyohiyo akapata nyumba nzuri sinza, umeme elfu kumi pia unachangwa ukiisha tu.

Tatu tanesco wametoa punguzo la service charge kwa ajili ya kusaidia ugumu wa maisha lakini hiyo imekuwa tofauti kwa wale wanaokusanya hela kwa mwenye nyumba kwa kweli hii ni kero kubwa wenye nyumba wengi kutumia mabavu wakishirikiana na wajumbe tunaomba serikali isaidie hili kuwe na ki bylaw cha kuregulate hii mikataba maana wapangaji wanaonewa saana kwa kile cha kusingizia ujenzi gharama, kama ni hivyo hata madereva wa madaladala nao wangekuwa wanaweka nauli kubwa maana na yenyewe ni gharama kununua wenye nyumba acheni huo unyapapaa.

Lingine wenye nyumba kufatilia maisha ya mpangaji, hasa ukikuta nyumba ana miliki mmama atataka ajue vitu ulivyonavyo, unaishije, una hela kiasi gani yanakuhusu nini wee umempangisha mtu nyumba iweje uanze kupepeleza tena wengi hufanya kuchonganyisha mpangaji na mpangaji ili ipate informamation za wote tuacheni hizi kero tubadilike
amini unamfanyia mtu unyama hujui kesho itakuwaje au wanao utawaachaje dunia hugeuka kila mtu anapenda kukaa kwake lakini shinda ni kipato
 
Sheria ya kuhamishwa ulipo panga notice ni siku 90 hata kama umerudishiwa pesa yako uliyolipa kodi
 
ni kweli lakini naona haina haja ya kuanza kulumbana na mwenye nacho nyumba ziko nyingi bora kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima
 
Na yeye akahama?
Yaani hela yake angechukua na asingekubali kubama hadi notice ya siku 90 iishe
 
Hizo ni changamoto tu na ukiona mwenye nyumba anakunyanyasa ujue anakupa akili na wewe ujenge nyumba yako.
Ila ukitaka kulijua hilo inabidi uwe na akili ya ziada.
 
Sheria ya kuhamishwa ulipo panga notice ni siku 90 hata kama umerudishiwa pesa yako uliyolipa kodi
Kama umehamia kwa mkataba kinachofuatwa ni mkataba tu mkuu,labda kama ulihamia bila mkataba
 
Dah kweli ni shida....mimi chumbani kwangu nina taa tu na kiredio....na muda mwingi nashinda mihangaikoni....lakini nalipia elfu kumi na tano.....
Mwenye nyumba akipata tatizo kumchangia ni lazima sio hiyari....
Mtoto wa mwenye nyumba ni deputy mwenye nyumba na anatoa amri halali.......
Siku mwenye nyumba akiamka vibaya na umeme anauzima siku nzima......
Matumizi ya choo mwisho saa nne usiku.......

Mnaokaa kwenye majumba yenu inabidi mumshukuru muumba kwa kuwapa neema hiyo....lakini nyumba za kupanga ni masimango tu.....unadharauliwa na kitoto kidogo kwa kuwa baba yake ndio mwenye nyumba......inauma sana...

Nikifanikiwa kununua kiwanja changu....nakwenda kukaa hata juu ya miti....
 
Back
Top Bottom