Wengi kanisani/msikitini hawatoi sadaka! Wanatoa michango

Wengi kanisani/msikitini hawatoi sadaka! Wanatoa michango

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,204
Sadaka ni ile hali ya kujitolea kitu chako cha thamani kubwa, ikiwemo uhai, kwa ajili ya upendo au imani fulani.

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu huu watu wamekuwa wakitoa sadaka kwa miungu wao. Mungu wa Israel alipojidhihirisha kwa wanadamu watu walimfanyia sadaka lakini ilisisitizwa sadaka itolewe kwa vitu bora na vyenye thamani sio vitu dhaifu.

Mwanzoni kabisa Mwenyezi Mungu alimjaribu nabii Ibrahim kwa kumtaka amtoe sadaka mwanae pekee, Isaka kwa kumchinja!!

Ilikuwa mtihani mkubwa lakini hii ilikuwa ujumbe kwamba sadaka lazima iume.
Sasa hatuwezi kutoa sadaka ya watoto wetu lakini wazee wetu walitakiwa wakitoa sadaka ya mazao basi yawe yale yaliyostawi. Sio kutoa mazao dhaifu. Hiyo sio sadaka kwa sababu hupotezi kitu kwa kutoa ngano mbovu!

Walitakiwa pia wakitoa sadaka ya wanyama watoe ndama walionona sio dhaifu, wazee na wagonjwa!!

Kumtoa ng'ombe mgonjwa sio sadaka kwani mtu hupotezi kitu kwa kutoa mnyama mgonjwa. Hupati dhawabu.

Siku hizi watu hutakiwa kutoa zaka kwa kutoa fedha ingawa hata kwa njia ya vitu inaruhusiwa.

Hata hivyo sadaka inayotolewa na baadhi ya waumini makanisani na misikitini siku hizi imepoteza hadhi ya kuitwa sadaka! Ni Michango!!

Kutoa nguo zilizochakaa kwa ajili ya masikini sio sadaka kwani mtu hupotezi kitu kwa kugawa nguo mbaya.

Ukitoa chakula kibovu vilevile hiyo sio sadaka. Ukitaka kutoa basi tenga sehemu ya kipato chako nunua nguo mpya wapelekee watoto yatima nk.
Tenga nusu ya akiba yako ya chakula kizuri wape masikini au nenda kanunue dukani kulingana na uwezo wako. Hiyo inaweza kufikiriwa kuwa sadaka.
Matajiri wanaojiita Wakristo au Waislamu wana mtihani mkubwa kukidhi viwango ya sadaka kwani yawapasa kutoa zaidi.

Tajiri anayemiliki mali kwa mfano za Sh bil. 5 hatumtegemei atoe laki mbili kama sadaka!! Labda aseme ametoa mchango.

Mtu mwenye utajiri huo hata akitoa laki tano haumii. Hivyo haikidhi viwango vya sadaka.

Hakuna mtu anayewaomba wala kuwalazimisha matajiri kutoa sadaka kwenye nyumba za ibada. Lakini wakijisikia kutoa basi watoe kiwango ambacho angalau kinachoakisi ukwasi wao.

Usitoe kanisani Sh 200 wakati mfukoni una Sh 5000 halafu ukaiita hiyo sadaka! Yesu alipomuona yule mama masikini ametoa pesa yake yote kama sadaka akasema "huyu ametoa sadaka kubwa kuliko wote"

Toa vyote ulivyonavyo kama unataka iitwe sadaka vinginevyo ni mchango tu.
Lazima sadaka iume. Ukiwa na laki moja mfukoni ukatoa kanisani Sh elfu moja hiyo walahi sio sadaka. Ili iweze kupanda ngazi kuwa sadaka angalau utoe elfu 90 na ubaki na 10!

Ukienda kanisani au msikitini hata kama umebakiwa na nauli tu ya kurudia nyumbani, toa yote sadaka.
Ni baraka kutembea kwa miguu kurudi nyumbani baada ya pesa yote uliyokuwa nayo kutoa sadaka.

Ukivuna magunia matatu ya mahindi usipeleke kibaba kanisani. Toa angalau gunia moja ili kutoa kwako kufanane na sadaka.

Ukipata pesa yeyote toa kiasi kinachoeleweka. Usipeleke mabaki na sarafu tu kanisani. Miaka yote tumekuwa tukitoa kamchango tu kwenye nyumba za ibada.

Sasa katika hizi 'siku za mwisho' tuanze kutoa kiwango kikubwa zaidi kanisani kuliko tunavyotumia kwenye mambo mengine.

Haiwezi kuitwa sadaka kama kwa mfano, msikitini unatoa Sh mia tano wakati kwenye mfuko wa nyuma una laki mbili. Tena pesa hiyo umepanga kunywea pombe au kujirusha.

Wengi hatuelewi sadaka ni nini. Utakuta mtu yuko radhi kutoa mchango wa harusi hadi laki tano, tena kwa marafiki wenye uwezo, lakini inapokuja sadaka kanisani anatoa Sh mia 2!

Wekeni hazina zenu mbinguni. Tuache kuhangaikia saaana maisha haya. Tunapita. Matajiri watayaacha mamilioni yao na akina yakhe wataziacha Sh mbilimbili zao. Tusipende sifa kwa mambo yasiyo ya kudumu.

Makanisa na misikiti yatajengwa na waumini wenye moyo wa dhati wa kutoa. Sio siasa au kutaka sifa. Mungu kwanza mengine yooooote, baadae....
 
thamani ya ninachotoa ni siri ya mimi na Mungu wangu, wengine hawatajua uthamani wake
 
Vyuma vimekaza mkuu

unaweza kutoa sadaka halafu baadae unamkuta padri au sheikh anaendesha Prado wewe una baiskeli



Nakumbuka sana kitabu cha THE TRIAL OF BROTHER JERO dah
 
mleta uzi wewe hua unatoa sadaka au mchango, usije ukawa na wewe ndo walewale
 
Hyo sadaka ya gunia 3 kwa moja ni sadaka ya aina gani?sadaka ya 9alfu ktk kumi alfu ikoje?yawezekana hujui hata maana ya sadaka
 
Hyo sadaka ya gunia 3 kwa moja ni sadaka ya aina gani?sadaka ya 9alfu ktk kumi alfu ikoje?yawezekana hujui hata maana ya sadaka
Itakuwa vizuri nawe ukatueleza maana ya sadaka kwa kadiri ya uelewa wako
 
Ukimsoma vizuri mtoa mada ameeleza maana ya sadaka kwa anavyojua yeye na kutoa mifano mingi na mpaka na mifano ya kutoka kwenye vitabu takatifu
 
Sadaka lazima ikuume. Uache starehe zako kwa sababu ya sadaka. Vinginevyo hiyo ni kitu kingine.
 
Back
Top Bottom