donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,258
- 22,140
Kwa wale wakuu ambao mlipita shule zetu zile za kawaida zamani, mtakumbuka kulikuaga na hii myth kwamba ukiweka nyoya la tausi katikati ya daftari au kitabu basi lile nyoya litakua. Nakumbuka kuna mdada nlisoma nae alikua anaamini kiasi kwamba eti analilisha lile nyoya yale ma left-overs ukishachonga penseli eti ndio chakula chake, mwisho wa siku watu wakamlia taimingi nakuliiba nyoya lake. Si akaenda kusema kwa mama yake ambae alikua ni mwalimu? Mama yake acha amnyuke bakora na kumuona mpuuzi kuamini such non living thing as a feather can actually grow!