Wengi bado wanampenda Al Assad huko Syria! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wengi bado wanampenda Al Assad huko Syria!

Discussion in 'International Forum' started by jmushi1, Sep 29, 2012.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Hii article inaonyesha sura ya tofauti kabisa na ile tunayoiona kwenye media...

  Wanadai taifa lao linaharibiwa na kwamba walikuwa wakiishi vizuri tu,inanikumbushia stori za walibya...

  Wanasema unyama mwingi unafanywa na hao wanaojiita revolutionaries...Lakini wengine wanasema wote serikali na revolutionaries ni wa kulaumu...
  Na kwahiyo wanajiuliza kama hawa ni wanamapinduzi kweli ama wahuni tu wenye kuharibu taifa lao?
  Kwamba jeshi lilikuwa likiwalinda kiukweli lakini sasa ni tofauti,pia wanamapinduzi wanawatumia watoto...

  Pia wanalaumu propaganda za kuonyesha kuwa serikali ndiyo yenye kufanya mauwaji,na pia mara nyingine ni uzushi...
  Na wakati mwingine wanauwa wananchi na huku waki chant kwenye video kuonyesha kwamba ni serikali imeuwa kumbe ni wao...Pia kuna aliyekufa kwa kansa,lakini wakati wa maziko,walipoona camera ya mwandishi,wakawa wanachant as if mtu huyo aliuwawa na serikali!
  Not Everyone Hates Syrian President Bashar al-Assad | PBS NewsHour | July 20, 2012 | PBS

  Very sad kwa kweli,those are the stories of true Syrian families ambao hata sauti zao hazipewi kipaumbele.
   
 2. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii Arab Spring kiboko! tuamini lipi sasa, western media/rebels/syrian government?
  Wananchi ndio wanaokufa na sio wapiganaji both rebels/government troops, very sad, rebels sasa hivi wamefungua kiwanda chao wanatengeneza silaha wanadai silaha wanazopewa na saudia arabia/quarter/turkey hazitoshelezi mahitaji, taifa linawaka moto, wananchi wapo katikati ya mapambano hawana pa kwenda, uku vifaru uku mizinga juu ndege za kivita. duuuuhhh
   
 3. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kila lenye mwanzo halikosi mwisho kwahiyo magaidi mwisho wake wataondoka tu.Kuna mengi ya kushangaza ktk hii dunia kwa mfano...Hawa wa magharibi wao huwa wanajitangaza kama wanapigana na magaidi lakini hivi sasa imegeuka wao wanaungana na magaidi kupigana na serikali za nchi za watu ambazo zipo kihalali.Sababu kubwa ni kwamba serikali hizo hazikubali siasa za wamagharibi kwahiyo lazima wazitafutie sababu kwa gharama yoyote ile haijalishi watu au watoto wangapi watapoteza maisha ila isitokee ktk nchi zao kwasababu wao ndio wanaroho wengine hawana roho.
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu,wananchi ndiyo wanaokufa,lakini kinachoonyeshwa ni miili yao tu wakiwa wameshakufa,lakini siyo maoni yao wakiwa hai!

  Camera ziko kwa hao wanaoitwa wanamapinduzi,na wakati mwingine jeshi.Laiti kama media zisingekuwa bias,basi tungeona mengi sana.Na hii habari ni ya pbs,a very credible source.

  Kwenye mgogoro huu,inategemea ni serikali gani itaingia madarakani,lakini kama wakiingia hao sunni ambao ndo wanaoitwa wahabi/salafi,basi ujuwe Iran hawana lao,na hao minorities watakuwa kwenye wakati mgumu sana.Inasemekana asilimia 60 ya wasyria wanamsapoti huyo Assad.

  Ila wakishamwondoa,watakuwa wameimaliza ile connection ya Iran na Hizbolah,na kwahiyo Iran itakuwa isolated,hilo linawafanya wairan wamsadie Assad kwa hali na mali,na inavyosemeakana,tayari wanafanya hivyo.

  Tatizo ni kwamba hata Suadi na Qatar ambao ni sunni,wanasapoti hao rebels kumwondoa Assad kwasababu hiyohiyo ya kuwadhibiti Iran,ila vita hivi vinaweza kuwasha moto mkubwa sana hapo middle east na kuuzima inaweza kuchukuwa decades.Na kama ikatokea Iran kuwa attacked,basi ndo itakuwa moto mkubwa zaidi.

  Yote hayo hata hivyo ni maisha mengi sana ya wananchi,wamama na watoto yanapotea bila mtu yoyote kujali.That is how this world is.
   
 5. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unajua serikali ya Syria ilikataa kushirikiana na western kwahiyo hawana dili ya peace na Israel kama walivofanya Egypt na Jordan.Na wananchi wa Syria kiukweli wako wanaompenda Assad na wengine wamegawanyika kutoka ktk vyama tofauti isipokuwa vyama vya upinzani vingine vimeungana na serikali kutokana na jinsi propaganda zinavofanywa na western.Na chama kingine ndio ngangari ambacho kinasapotiwa na Western wakishirikiana na Saudi pamoja na Qatar.Na sababu kubwa ya kuichukua Syria ni kuilinda Israel ambayo ni kama kambi ya kijeshi kwa Western.Kwahiyo kama wataweza kumuondoa Assad basi inamaana Hezbullah watakuwa nguvu yao imepungua kwasababu ni tishio kwa Israel.Na Iran inaitumia Hezbullah kama kambi yake ndogo ya kijeshi ikiwemo Syria yenyewe.Kwahiyo silaha zote za Hezbullah zinatoka Iran kupitia Syria na ikiwemo Syria yenyewe vilevile inaisaidia Hezbullah kwa silaha.Ndio maana tukaona ile vita ya Lebanon na Israel ilikuwa hakuna alieshinda hata hivo kwa muelekeo mwingine inaeleza kama Israel ilishindwa kwasababu nia yao ilikuwa kuiangusha Hezbullah lakini haikufanikiwa kwani walipewa suprise.Walidhani wataingia kirahisi kuipiga na kuichukua nchi na matokeo yake walikufa wanajeshi wengi na vifaru vingi viliharibiwa.Kwasababu Rusia waliwapa Syria silaha ambayo inauwezo wa kuviangamiza vifaru vya Israel ambavyo vilijulikana kama ndio best ktk vifaru vinavotengenezwa hapa duniani.Na hao waandishi wa habari waliokuwepo huko kwakweli ni mtihani mkubwa kwasababu wengi wao wamepelekwa na nchi za western au zile zinazo sapoti western.Kwahiyo wanaweza kwenda sehemu ya rebels na wakachukua watu waliouliwa na wapinzani na kutoa taarifa za uongo ili waisingizie jeshi la nchi.Kwasababu western wanachofanya ni kuongeza maafa Syria ili ipewe sapoti ya kuingia kijeshi na sio rahisi Urusi na China kukubali.
   
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu,lakini huko middle east kuna vituko sana,nadhani the bottomline ni ubinafsi.Kwamfano Hamas walikuwa wakisaidiwa na Assad,lakini sasa hivi wako against naye.Wote wanataka uhuru wa Palestine,lakini bado wote wamegawanyika,hilo ndo litawacost maisha yao yote kwasababu ni rahisi sana kugawanya base on sects(Shia,Sunni,Alawite,suffi nk).

  Ila mashaka makubwa sana yatakuwepo baada ya Assad kuondolewa,kwasababu nina uhakika kuwa hao wanaotaka kumwondoa ni sunni(wakisaidiwa na Saudi na Qatar)ili kumdhibiti Iran(ShiaAlawite,na sufi),na hao kina Assad ni minorities watakuwa na wakati mgumu sana,pamoja na ukweli kwamba silaha za kikemikali zinaweza kuingia mikononi mwa watu wabaya.Situation ya maeneo yale siyo nzuri kabisa.

  Kitu kinamweka Assad madarakani hadi sasa ni msimamo wa China na Urusi.Hata hivyo,juzi wamekutana "friends of Syria" waliongozwa na marekani na Saudi,wamepitisha maazimio ya kuendelea kuwasadia waasi.Na vile vile raia wa marekani wameruhusiwa kuchangia mamilioni kwa ajili ya waasi,wakati huohuo marekani anamwonya Iran aache kuendelea kumsaidia Assad kwa silaha.The overall situation is extremelly fragile.
   
 7. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni sawa kwa mtazamo wako ila Hamass hawawezi kuachana na Syria wale msimamo wao ni wa uhakika.Na hii vita ya ushia na usunni vilevile ni ya kuchonganishwa na western ila inaelekea kushindwa kwasababu wafuasi wa sunni wengi wanaipendelea Iran isipokuwa ni hawa viongozi wa Saudi na Qatar. Kwahiyo kila miaka inavozidi kwenda mioyo ya watu inabadilika kutokana kwa kubaini ukweli ulipo na hata media zinachangia kuongopa.Mfano Al-Jazira zamani ilikuwa ni tishio kwa western lakini sasa hivi wamewekwa chini na wanaifanyia kazi western na ndio maana kuna wanahabari wao baadhi wamejiuzulu kwasababu wanasambaza habari za uongo kutoka Syria.Na sasa hivi Iran anayo steshen yake Press TV ambayo na yenyewe inatoa habari tofauti na nyingine.Kwahiyo wengi wao sasa wanajua kama TV zinatoa false information kwa kutaka sapoti.Itakavokua lazima kutachafuka zaidi ya hapo na tutarajie vilevile huko Saudi wananchi lazima watacharuka.Kwani tayari wameshaanza baadhi ya miji japo ulinzi mkali na sio rahisi kusikia ktk TV ni Press Tv tu ndio anaonyesha kwasababu lazima na wao wapate wafuasi kutoka maeneo hayo.Kiukweli hii vita USA inawakosti sana na walitegemea watafanya kama Libya kumaliza muda mfupi lakini hatimae mambo yamekwama.Mikutano yote waliyofanya wameshindwa kwahiyo inabidi waendelee kuwadhamini wapinzani.
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Ndiyo mkuu,Hamas wanawasapoti Syria,lakini wanawasapoti wapinzani na siyo Al Assad ambaye aliwasaidia sana huko nyuma.Ndo hapo shukran ya punda ni mateke.

  Kuhusu hilo la kubadilika,inawezekana,lakini it will take time kwasababu ya balance of power.Ni kweli sunni wengi wa Syria licha ya kwamba wao ni majority,lakini hawana shida na Al assad,ila kuna wachache wenye connection na wahabi wa saudi.

  US vita hii haimcost kihivyo,sanasana wanauza silaha ambazo saudi na qatar wanatumia pesa kuzinunua na kuwapelekea waasi.Syria ikianguka,hapatakaa kuwe na amani hata kidogo.

  Upande mmoja wako Iran,na mwingine wako Lebanon na Hizbolah.Kumbuka ni Al Assad alituhumiwa kwenye yale mauwaji ya waziri mkuu wa Lebanon Rafiq Hariri.

  Kutawaka moto kwasababu kila mmoja anataka kuwa more influential.Halafu bado kuna the Iraki factor,ambapo Iran ana influence kubwa kwasababu majority pale ni shia.Watavurugana sana na sioni mwisho wake.Sana sana watu wanapoteza maisha na wenzao wanauza silaha tu.
   
 9. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi bado siamini kama Hamas wanaweza kuwakubali wapinzani kwasababu wapinzani wameungana na western ambao sapoti kubwa pia inatoka Israel pamoja na Uturuki.Hamas na Israel hawawezi wakawa pamoja hata siku moja.Kwasababu Saudi inajulikana kama kingdom inasapoti Israel na ndio maana Saudi kingdom hawaelewani sana na Hamas ila wanaelewana na Mahmud Abbas.Kwasababu kawekwa ili awasaidie Israel kuendelea kukaa na kuweka usalama wa muisraeli.Hamass hivi sasa wamebanwa kiasi kwamba hawasikiki sana ktk media kwahiyo alie tangaza kama Hamas hawataki serikali ya Assad ni Israel na hii ilikuwa ni propaganda ili wajijengee sapoti.Niliwahi kuona speech kipindi cha nyuma kwa kiongozi wa Hamas nchini Syria hajatamka maneno hayo ila alikuwa analaani mauaji yanayofanywa na wapinzani.Kwasababu wakiikataa serikali ya Assad hawawezi kukubalika na wapinzani ambao watakuwa chini ya Israel na wao vita yao kubwa ni Israel hawaitambui.
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Haya soma hii...
  http://www.nytimes.com/2012/02/25/world/middleeast/hamas-leader-supports-syrian-opposition.html
   
 11. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I think Putin knew it well, the so called FSA they are RAG-HEAD Arab-thugs,Thief's, and Idiot from all corner of the ARAB WORLD,all the way from SOMALI-AFGHAN connection. The west have failed in this.. The battle for Syria have been lost with it the war for Iran. Shame on them. NANI ANAITAJI SHARIA LAW.
   
 12. n

  nsanu Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Assad kama hatang'olewa basi Syria hapatakuja kuwa na amani kwa muongo mrefu, kila nikiiangalia Syria aftr Assad naiona is a new Iraq
   
 13. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hakuna maneno yeyote yanayoweza kusemwa na binadamu yatakayoniaminisha kuwa fulani anapedwa na kusapotiwa na wananchi wake ikiwa huyo fulani ni mwoga wa kitu kinachoitwa kura.

  Kama 60% inampenda, basi uchaguzi huru utaamua hilo.

  Kudhania China na Russia wana maana ni kujidanganya. Hawa ndio wauza silaha namba 1 kwa matendo yote machafu ya dunia hii. Wataalam wa migomo bubu wasiojua kumsaidia mtu kitu.

  Tatizo la waarabu ni UFALME. Viongozi wana hulka za KITAWALA na hawajui kuwa nchi ni ya Wananchi zaidi ya kuona ni ya familia zao na wengine ni wapangaji.

  KIla kitu huko ni kulazimisha. Kufuga ndevu lazima, kuvaa miguo myeusi lazima, kufungia wanawake ndani lazima ili mradi kila kitu ni shuruti. Sasa katika dunia ya leo, kazi ipo.
   
 14. TZ biashara

  TZ biashara JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 523
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hizo habari walizitoa Waisrael hata mimi niliwahi kuona station yao moja vilevile lakini hiyo habari haina ukweli.Unajua Israel ili apate sapoti inabidi atumie mbinu zote mkuu na yupo tayari kusema uongo wa aina yoyote.Mimi ninazo stesheni nyingi za TV mpaka za kiarabu kwahiyo najua jinsi hawa wanavofanya.Na hiyo habari uliyo weka ipo chini ya muyahudi kwasababu ni "New york times"kwahiyo usitegemee kupata habari ya ukweli.Media karibu zote zilizopo USA n Europe zipo chini ya mayahudi na kikubwa zaidi ni kutembeza propaganda ili kuwakosanisha.Lakini waarabu sasa hivi baadhi yao wanatumia mbinu tofauti na sio rahisi kuwagonganisha vichwa waliweza kuwagombanisha Hamas na Fatah lakini huku kwengine hawa mitandao yao ipo pamoja na wanamsimamo mkuu hiyo ni kweli tupu.Na ukisoma habari za hawa jamaa zita ku confuse sana.Uwezi amini nimekutana na muingereza ananiambia hana muda wa kuangalia chanel za kwao kwasababu ni waongo na anajua kinachoendelea na wapo wengi kama hao.Wazungu wamezifungia chanel ya Press TV kwasababu inawaumbua.serious mkuu
   
 15. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani unadhani Iraki kuna amani?

  Pia hata kama simshabikii Al Assad,lakini ninaamini akiangushwa hakutakaa kuwe na amani.Si tupo?Tuombe uzima.
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,924
  Trophy Points: 280
  Daah!mkuu wewe ni mbishi kweli kweli,haya nimekuletea ya waarabu basi kama ndo utaiamini...
  Loading...
   
Loading...