Wenger aponda hali ya dimba la Old Trafford

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ameuponda Uwanja wa Old Trafford kwamba si mzuri na haufai kuchezea soka ya kuvutia.

Kauli hiyo ilitolewa mufa mfupi baada ya kuishuhudia timu yake ikifungwa 1-0 juzi usiku na Manchester United na kuondolewa kileleni mwa Ligi Kuu ya England.

Katika mchezo huo, klabu hiyo ya London ilishindwa kuonyesha cheche na soka yake ya kitabuni ya kushambulia zaidi na kwa muda mrefu.

“Tumeona makosa ya kiufundi kwenye timu zote mbili, lakini hayo ni matokeo ya uduni wa uwanja ambao umetuzuia kucheza soka ya kuvutia,” alieleza Wenger baada ya mchezo huo . “ Umejaa mabonde, yanaufanya mpira usitulie na pia ulikuwa na utelezi.”

Wenger, ambaye mara kadhaa ameshindwa kuonana uso kwa uso na mpinzani wake wa Man United, Alex Ferguson, alikataa kuingia katika vita ya maneno kabla ya mchezo huo, ingawa alieleza kuwa matokeo hayo hayakuwa ya kukatisha tamaa.

“Kiufundi, uchezaji wa timu zote mbili ulikuwa wa wastani kwa sababu ya hali ya dimba ambayo kwa mtazamo wangu si nzuri, kiasi kwamba imeathiri mchezo kwa kiasi kikubwa,” alisema.

“Kama nitaulizwa kama dimba ni mzuri au mbaya, unataka niseme nini?”

Alisema watumishi wa uwanja huo waliumwagia maji kabla ya mchezo na wachezaji kadhaa walianguka, ingawa ukuta na sehemu imara ya kiungo ya Man United iliyoundwa na watu watano na wepesi wa chipukizi Rafael aliyezuia krosi zetu wamechangia kushindwa kwetu.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo, beki wa United Patrice Evra aliwaita wachezaji wa Arsenal kuwa ni “kituo cha mafunzo”, akieleza kuwa wanachezea mpira kwa kiasi kikubwa, lakini si miongoni mwa timu zinazowania taji la ubingwa.

Kwa jumla, mchezo wa kuvutia uliozoeleka wa Arsenal ulikosekana juzi usiku, lakini Wenger alieleza kuwa hana hakika matokeo hayo yana maana gani kwa timu yake ambayo haijashinda taji tangu mwaka 2004.

“Ni matokeo ya kukatisha tamaa, tumekata tamaa sana, lakini kitu muhimu kwetu ni kwenye mchezo ujao tupate matokeo mazuri ,” alisema kocha huyo Mfaransa. “Kwa jumla, kutokana na hiki nilichokiona leo, hakuna sababu ya kutojiamini . Tumeonyesha kuwa imara kwa jumla.”

Naye Ferguson alieleza kuwa walistahili kushinda kwa mabao zaidi, kama si kukosa nafasi nyingi za kufanya hivyo.

Alisifu safu yake ya ulinzi kwa kuweza kuwazima washambuliaji wa Arsenal na sehemu ya kiungo kwa kuwazuia kucheza mchezo wao wa kawaida wa pasi za haraka, kasi.

Wakati huohuo, beki chipukizi wa England, Kerrea Gilbert amefuata nyayo za David Beckham kwa kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS), Portland Timbers.

Gilbert, 23, ambaye ameichezea Arsenal kwa miaka mitano amekulia England akiwa katika shule ya soka ya klabu hiyo.
Alicheza kwa mkopo kwenye klabu kadhaa za madaraja tofauti nchini mwake.

Klabu hiyo ya Timbers, ambayo itacheza MLS msimu ujao, imemsajili beki huyo kwa lengo la kujiimarisha na kumpa mkataba wa miaka minne.
 
wenger anamatatizo makubwa sana naomba mumsameheeeeeeeee tu,mara nyingi akifungwa anatoa vizingizio vya ajabu sanaaaaa
 

Attachments

  • gunners.jpg
    gunners.jpg
    8.2 KB · Views: 45
....Kweli uwanja haukua ktk hali nzuri siku ile lazivyo ya Barca na Madrid yangemkuta pale OT
 
Alibanwa maswali na waandishi wa habari ikabidi asingizie uwanja huyu mzee bana utafikiri ndio mara ya kwanza arsenal kucheza hapo cheap comments from him
 
siku moja atakuja kusema mpira haukuwa wa mviringo au majani siyo ya kijani sana!sipendi sana waalimu ambao hawawezi kukubali kushindwa na ubora wa wapinzani wao.:angry:
 
Back
Top Bottom