Wenge ya Jay Melody: Muziki mzuri wa msanii mdogo

fineboy

Senior Member
Nov 7, 2017
122
250
Nasema haya baada ya siku mbili hivi kutoka kwa ngoma kali sana za wasanii wachanga ama unaweza kuwaita wadogo, wasaniii wenye uwezo halisi wa kutengeneza muziki na mashairi yalioshiba. Wanaopenda muziki mzuri najua mtaelewa nachosema.

Siku kama mbili zimepitaa msanii "JAY MELODY" ametoa ngoma kali sana yenye mashairi ya kutisha mpaka kunichukua hisia na kunipeleka mbali sana kutokana na hali yangu ya kimahusiano ilivyo kwasasa.

Msanii huyo ambaye pia ni mwandishi wa mashairi ya nyimbo, ameandika nyimbo mbali kama ule muziki aliyoimba Nandy unaoitwa Kivuruge. Pia aliandika wimbo wa msanii mwezake, nyimbo ya maarufu ya Hauzimi wa msanii Benson.

Baadhi ya mashairi yaliopooo kwenye wimbo wa JAY MELODY, wimbo unaitwa Wenge.

Muinjoy wikiendi na mziki mzuri wakuu.

Oooooh ooh vile moyo unavuta najionea sana huruma
Nakaa chini nalia najiangalia sijitamani

Chini nachimba aaah, natafuta mzizi ooh
Najitafutiaa dawa kusinga kwa hirizi najiitaa mjingaa aaaah
Jay acha utoto, najiona mjinga wenge kimtindo

Hata tusiwee wapenzi mama jua naumia umeeondoaa mchuma
Mama ngazi inaaachia, wewe una-enjoy upendo mimi nachezewa hisia,
Penzi langu mama natamani urudi zamani
 

Attachments

  • File size
    9.9 MB
    Views
    0

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom