Kwa sababu hatujui kesho tutakutana na nani basi fanya wema kwa yeyote bila kujali cheo chake, rangi, kabila na hata dini.
Imepita kama mwezi hivi Siku Moja niko maeneo flani natembea nikaiona simu aina ya sumsung pembezoni mwa njia ikiashiria kuwa imedondoshwa, simu ile ilikuwa mpya kabisa na nzuri hasaaa.
Nikaiokota nikaendelea na safari zangu ikapita kama nusu saa ikapigwa nikapokea, akaongea kaka mmoja kwa unyenyekevu sana akinisihi kwamba yeye ndiye aliyedondosha simu akiwa kwa boda boda hivyo ananiomba sana nimrudishie na atanipa kiasi flani cha pesa.
Basi moyo ukaanza kubishana nizime nitoe laini nitokomee au nimpe tu, dah shetani mbaya, roho wa Mungu akaniambia mpe, mabishano yakawa makali kati ya roho ya shetani na ile ya Mungu, mwisho wa siku nikaamua nisikilize la Mungu la kumpa simu mwenye simu.
Nikamwelekeza nilipo akaja nikampatia na kunipatia kiasi cha ela, dah nikakataa nikamwambia hana sababu ya kunilipa chochote kwani ile simu ni haki yake na mali yake, akanilazimisha sana nikagoma,.
Yule kaka hakuamini kama kuna binadamu anaweza okota sumsung akarudisha na akapewa hela akaikataa.
Basi juzi nikawa naenda mahali na nilikuwa nje ya muda so ili kuwahi ilinibidi nichukue boda, nikaongea na boda boda wa kwanza akasema huko nakoenda ni mbali na barabara ni mbaya na ni usiku so akanitajia bei kubwa sana, dah nikamshindwa akaja mwingine naye,hivyo hivyo
Wakati nawaza nifanyeje akaja yule niliyeokotaga simu yake kumbe kilikuwa ndo kijiwe chake na alishaniona na akanikumbuka akaja a kaniambia dada wewe si ndo uliokotaga simu yangu nikamwambia ndo mimi ujakosea, akasema twende dadangu, nikapanda akanipeleka bure akanisubiri akanirudisha hadi nyumbani bure kabisaaaa.
Jamani nilifurahi sana si kwa sababu nimepelekwa bure bali kwa sababu Mungu aliamua kunidhihirishia kuwa wema hauozi, nilifundishwa kwa matendo.
Nawewe msomaji wangu ebu tenda wema kuna siku tu Mungu atakulipa tena unaweza usijue wakati ukilipwa.
Epuka kutendea mtu mambo ya hiyani kuna machozi ya watu ambayo huwa hatari yanapodondoka.
Jioni. Njema