Micheweni Pemba
JF-Expert Member
- Jul 13, 2010
- 351
- 179
SEHEMU YA KWANZA: KUTOKA UWANJA WA VITA – TEHRAN 1985
Mwezi Machi 1985, Tehran ulikuwa ni uwanja wa vita. Makombora ya Iraq yalikuwa yakidondoshwa kila usiku na kuwaweka wakazi wa jiji hilo katika hali ya taharuki. Raia wa kigeni wakaanza kuhama. Walihaha kutafuta tiketi za ndege kutoka shirika moja hadi jengine.
Tarehe 17 Machi, Saddam Hussein wa Iraq akatangaza kuzitungua ndege zote zikiwemo za kiraia baada ya masaa 48 kumalizika. Kuanzia hapo tiketi zikageuka kuwa vipande vya karatasi, kwani mashirika ya ndege yalilazimika kuhamisha raia wa nchi zao kabla ya muda uliotangazwa.
Japan ilikuwa na raia 216 Iran na shirika lake halikuwa na safari za Iran. Japan iliomba kuhakikishiwa usalama na Iran na kukubaliwa, lakini Iraq haikujibu ombi kama hilo. Ikawa ni vigumu kwa Japan kupeleka ndege Iran, hasa kutokana na masafa, upande wa kutokea na uzoefu. Wajapani wakawa wamechanganyikiwa.
Uturuki ilikuwa na raia takriban elfu sita nchini Iran. Nao wakihaha kutaka kurudi kwao, shirika lao la ndege lilikuwa na ndege moja tu kwa siku. Watu wengi walikusanyika kuwahi tiketi za ndege, kwani safari ya gari nayo haikuwa salama.
Katika hali kama hiyo, usiku wa tarehe 18 Machi wajapani wakapata mawasiliano kutoka kwa balozi wao kuwa wafike shirika la ndege la uturuki kukata tiketi. Walipofika wakakutana na misururu mirefu ya waturuki, lakini wakajikuta wao wamepewa kipaumbele!
Saa mbili usiku wa tarehe 19, ndege 2 za uturuki zikatua katika uwanja wa kimataifa wa Mehrabad, masaa 2 kabla ya muda wa mwisho uliotolewa na Iraq. Ndege ya kwanza ya kawaida na ya pili ni maalum. Ndege ya kwanza wakapanda Wajapani 215, na ya pili Waturuki na Mjapani 1 aliebaki. Wakati huo mji wa Tehran ukihanikizwa na sauti za ving’ora kuashiria makombora yaliyokuwa yakikaribia kutoka Iraq.
Ndege maalum ya kuwaokoa Wajapani ilipelekwa baada ya ombi la Waziri Mkuu wa Japani kwa Waziri Mkuu wa Uturuki Turgut Ozal (marehemu). Ozal alikubali ombi hilo na kuliamuru shirika la ndege la Uturuki (Turk Hava Yollari – THY) kupeleka ndege ya ziada. Inasemekana shirika liliwaita marubani wake na wahudumu wazoefu kwa safari hizo za mwisho, na kuulizwa walio tayari kujitolea. Wote walinyoosha mikono kutaka nafasi hizo!
Kuna masuali mengi ya kuuliza:
Ni kwa nini Japan ilipeleka ombi Uturuki?
Kwa nini Waziri Mkuu alikubali ombi hilo?
Kwa nini waturuki waliokuwa wakihaha kupata tiketi waliridhia nafasi chache zilizopo wapewe Wajapani?
Kwa nini wananchi wa Uturuki waliridhia uamuzi huo?
Nini kiliwapa ujasiri marubani na wahudumu wa THY?
Waturuki walikuwa wakitaraji nini au wakilipa nini kwa Wajapani?
(Picha kutoka Wikipedia)