Weka porojo na misifa ya kijinga tujadili ukweli huu

Weka porojo na misifa ya kijinga tujadili ukweli huu

mtunzasiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
1,449
Reaction score
993
copy and paste Facebook

Kuna watu wamezoea porojo,
kuna watu hupenda kujadili changamoto na mambo ya msingi katika Nchi,
TANZANIA tuko kwenye Uchaguzi wa Rais, wabunge, na madiwani.
Tunao wagombea wengi wa Urais lakini tuzungumzie ,
EDWARD NGOYAI LOWASSA NA JOHN POMBE MAGUFULI,
Kati yao kwa utafiti na uchambuzi mbalimbali mmoja anaweza kuwa Rais wa Tanzania.
Sasa tuone baada ya uchaguzi,

hivi ni kweli JPM Ana uwezo wa kuleta mabadiliko na kuwageuka kina kikwete,mkapa,mwinyi,kinana,chenge,Nape, na wafia bendera wote ndani ya CCM na kubadili mambo kiutendaji kuondoa kulindana rushwa, na ufisadi ambao ndio kilio cha [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=mabadiliko2015]#mabadiliko2015 ??[/URL]

Au je ni kweli LOWASSA anaweza kuWageuka UKAWA na kuzalisha ufisadi kama ilivyo ccm leo na kuondoa ndoto ya #mabadiliko2015 wanayoyataka Watanzania wengi? Au tutaona neema mpya Tanzania tujadili...
 

Attachments

  • 1442327864139.jpg
    1442327864139.jpg
    68.2 KB · Views: 187
  • 1442327880402.jpg
    1442327880402.jpg
    42 KB · Views: 158
Fisadi ataendeleza ufisadi wake na atawashawishi wenyeji wake wawe kama yeye na asiye fisadi vivo hivyo!
 
Kumpa nchi Magufuli ni sawa na kumpa kazi kondoo alinde simba.
 
Dunia ya leo inahitaji kiongozi mwenye upeo unaoendana na mabadiliko ya kidunia kwa ujumla na si kiongozi mwenye upeo unaoishia ndani ya mipaka.Maendeleo ya leo hayatikani na ujenzi wa madaraja pekee bali ushirikiano kati ya taifa moja na jingine.Huwezi kuishi kwenye dunia ya Sayansi na Technologia ukitegemea kupata maendeleo wakati una maono Local na siyo Global.Tunahitaji Raisi mwenye upeo unaoendana na kasi ya maendeleo ya dunia hii ya leo na si maendeleo ya barabara na madaraja pasipokuwa na mipango ya kutuandaa kuwa watu wa kujitegemea na kutegemewa kiuchumi.Watu wanaongelea kuanzisha viwanda pasipo kufafanua soko la uhakika litapatikanaje.
 
Baada ya ushindi wa magufuli naona jinsi alivyoshindwa kuwageuka mafisadi umewakumbatia na amewahakikishia usalama wao alichofanya ni kuongeza jengo la mahakama na kuita mahakama ya ufisadi lakini mpaka sasa ufisadi uliosemwa kwa muda wote hakuna hata mmoja ulio kwenye mahakama hiyo.
 
Baada ya ushindi wa magufuli naona jinsi alivyoshindwa kuwageuka mafisadi umewakumbatia na amewahakikishia usalama wao alichofanya ni kuongeza jengo la mahakama na kuita mahakama ya ufisadi lakini mpaka sasa ufisadi uliosemwa kwa muda wote hakuna hata mmoja ulio kwenye mahakama hiyo.
1471861240873.jpg
 
Ikulu sio sehem ya kujifunza kuongoza. Mtu aliyeshindwa kuwa kiongoz bora awali hawez kuwa bora sasa. Tutajuta kumpa nchi
 
Back
Top Bottom