Weka hapa nyimbo ya underground unayoikubali (Uzi kwa ajili ya undergrounds wanaofanya vizuri)

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,816
11,541
Hello wakuu, mara nyingi wasanii wanaohit ndio tunaamini wanajua, kumbe wengine wanabebwa na labels, marketing, algorithms, nk. Nk.

Makampuni kama Universal, Sony, nk. Nk. Yanaweza kupush mimbo ihit kumbe yana agenda zao kama za LGBTQ kina Lil nasX, Cardi b na wengineo.

Mda huo huo kumbe kuna undergrounds wanafanya vizuri kuliko hata baadhi ya mainstream artists. Na hii ni kote USA, Nigeria, hata Bongo.

Naanza na Mimi list ya undergrounds naowakubali ni;
1.JID (USA)-Sidhani kama saivi ni underground ila sio mainstream pia. Huyu jamaa anajua zaidi ya kujua, yupo chini ya dreamville ya J.cole. Album yake ya forever story ndo album yangu ya mwaka huu.

2.Little simz (UK):
Huyu nampenda anavyomix UK slang hiphop na Afrobeats.

3.Sampa the great(zambia)-
Huyu napenda anavyorap na pia ana zile sound za natural African vibes fulani, ukisikia ndo utaelewa.

4.Tobe Nwigwe (USA but originally Nigerian)
Huyu jamaa ni genius aisee, ukicheki video zake utaona jinsi alivyo creative.

5.Buju (Nigeria)
Huyu jamaa nlimjia kwenye kibao cha cold outside ft. timaya. Mistari imekaa, melody kali, inshort anajua.

6.Dizasta (Tanzania)
Huyu haitaji introduction..labda muulizeni Scars

7.Weston estate (USA)- Hii ni Boyband ila wanajua na wanastahili more attention kuliko waliyonayo sasa hivi.
 
Back
Top Bottom