weekend yangu ilijaa kumbukumbu za ahadi tele za uchaguzi wa 2015.

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Baada ya Timu yangu ya Simba kufungwa, Chelsea kufungwa nikaamua nijikumbushe tu ahadi za wagombea wetu wa uraisi wa 2015. Mheshimiwa Edward Lowassa na John pombe magufuli.

Edward Lowassa kipaombele cha kwanza elimu, chapili Elimu na cha tatu Elimu, Elimu bure mpk chuo kikuu, maji yatapatikana, Anayekula mlo mmoja atakula milo miwili nk. Lakini kwa mujibu wa matokeo yaTume Ya uchaguzi hakufanikiwa kushinda hivyo ahadi zake hazitekelezeki.

John pombe magufuli Serikali ya magufuli mikopo ya elimu ya juu itatoka kwa wakati, mwanza itakuwa kama Geniva, kila kijiji kitapata shilingi milion 50 kwa mwaka, Kodi ndogondogo ambazo kero kwa wananchi nitaziondoa, Tanzania nchi Tajiri haiwezi kuwa maskini nk. Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yalivyotangazwa na tume ndiye alishinda sasa ndo anatekeleza ahadi zake.

Kwangu kila nikimpigia babu kijijini kumwuliza kama milion 50 wamezipata anacheka tu, nina rafiki yangu ndugu Rafael wa mwanza nikimpigia vipi huko mwanza kama geniva mmmh anasema hakuna chochote kilichobadilika sasa sijui kama wenzangu huko kwenu ahadi zinatekelezeka.
 
Back
Top Bottom