Weekend story! BEN 10

Bora ya kr na kyle yalivyoparanganyika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
For once in my lifei was helpless! Lost and in pain! Maumivu ya moyo hayapoi kwa ganzi! Kama moyo kupata jeraha ulipasuka vipande vipande! Ghost ashanipa maumivu ila hayaingiii hata robo kwa haya! Hata robooo! Mpaka maji nayaona kama shubiri!

Niliona Mozah anavo lia mpaka anaishiwa nguvu anajilegeza nilikuwa sijui maumivu ya moyo kiboko! Mifupa ilio pondeka pondeka ! Jeraha la moyo ni jeraha baya sanaa! Usiku sina hamu ya kulala kabisaaaa kabisaaa! Nilikaa siku 3 hata kusinzia!

Mwanangu akaona kuniguza peke yake hawezi ikabidi Hans aje! Nikaenda chumbani kwa Hans kupekua unga wake alipouficha nipanguse japo kidogo tu! Nilielewa kqabini Hans hafanyi jitihada za kupona! Amejeruhiwa moyo! Sikuupata unga!

Nikaanza kumuomba Hans naomba basi hata ukucha, nateseka mwenzio, nitakuja kufa nikuachie mtoto uleee mwenyewe bila msaada kisa kuninyima ukucha! Akakomaa sina unga mimi! Nimeacha! Nikaenda kununua kwa Cookie akaninyima! Unga ukiutafuta huupati! Ikabidi niende kuchoma valium ndo nilale!

Nimbembeleza hans chukua basi hata papa unipe huo unga! Hatakii! Ananiambia nenda kwe ye maombi! Namwambia sitaki! Ananikumbusha unakumbuka mnavonilazimishia rehab? Namwambia kaliwe kiboga achana na mimi! Nilimuone huruma mwanangu sanaa maana wazazi wote nati zimekatika!

Akaja Mozah kuniomba niende kanisani! Nikaenda sura imenishupaaa! Mda wa maombi watu wanajimimina mi nimekaa tu naangalia angalia wanavojimaliza! Naanzia wapi kuomba? Naishia wapi! Moyo wangu ulikuwa umejeruhiwa vipande vipande! Ningesema niende mbele za bwana nisingejizuia kuporosha mitusi nikajikuta nalaabiwa bure! Wacha tu nijeruhiwe moyo!

Nikakuta Hans kaniletea bangi! Nikamwambia badala unipe mambo ya konki mambo ya m colombia unanipa m jamaica! Maumivu nayosikia moyoni mwangu naweza kumla huyo mjamaica na ugali kama mboga! Niacheeee bwana!

Kila nikijitahidi kumsahau yule bwege nashindwa mwenzenu! Nashindwa kabisaaa! Sijui alikiwa kaniloga na kama kaniloga kweli mganga wake basi ni mamba kabisaa sio kiboko! Na hivi navomkumbuka nashikwa na uchungu usio na uzazi!

Kanisani nikaacha kabisa kwenda wala kusali wala kuomba wala kuamini! Nikawa nipo nipo kama mpagani tu! Naanzaje kupanda madhabahuni na kiwaambia watu Mungu anaishi, ana nguvu na uweza wakati mimi kunitendea maajabu kagoma? Nawaombea watu wanafanikiwa sanaa! Nikijiombea mwenyewe holaaa! Seriously? Basi sijiombei wala simuombei yoyote! Tukose wote!

Kila nikijitahidi kumsahau nazhindwaa kabisaa! Naanzaje kwa mfanooo? Mwanaume anajua kupenda yuleeee! Sijawahi kupendwa maishani mwangi kama nilivo pendwa na huyu mpuuzi! I didnt have to try hard! Situmii nguvu, sifosiiiii! It was true love! Raha sanaa ukimpenda mtu akakupenda!

Kukawa na kitchen party ya mdada mmoja kanisani! Mozah kanikeraaa nikaamua kwenda nae! Kukawa na mchungaji akasema wale wote ambao hawajaolewa wasimame niwape upako mwaka huu haushi wataolewa! Na maneno yangu hayatonirudia kinywani kwangu!

Sikusimama! Mozah ananifinya finya! Nikachana pakti ya konyagi na kuinywa dry! Mozah akasimama! Nikaona kichekesho anataka kuolewa tena khaaaaa! Akaomba pale mahubiri mazuri! Mistari ile ile who finda a wige finds favor from God! Akatumia na ya Abraham kumtuma kijakazi akamtafutie Isaka mke! Ile ile ya kila siku! Sikusikiliza! Baadae Mozah ananiambia nilisimama kwa niaba yako! Khaaaaaa! Nikamwambia sababu miguu ni yako next time chuchumaa kabisaa kwa niaba yangu!

Kila navojitahidi kujipa moyo nime msurvive Ghost kweli huyu anishinde kabisaa? Hana jeuri hioo! Nikowaza hana jeuri nakumbuka mara ya kwanza namuona nikasema kaka mzuri huyuuu! Ila mimi sina bahati hizi! Akaanza kunichatisha chatisha! Nikasema jamani mimi huyu huyu au? Nikajua labda anataka kunidanga!

Akanikaribisha ofisini kwake Standard Chattered Bank! Nilashangaa kwamba he actualy have a life! Ndo nikadata kabisaa! Nikataka kumshirikisha Mozah ila nikaona hataaa! Asije kuniharibia mimi! Let me handle him alone! Hana papara na papuchi kabisaa!

Nikawa nalala na Ghost kimazoea tu, ila moyo kama moyo ushahama! Ishahamia huku! Kenny anakua!sha na good morning text! Mchana atakitafuta kokote mle wote lunch! Akitoka kazini lazima akutoe out! Mpaka kesho yake tena hio! Ndo ratiba!

Hakuwa msemaji kabisaa! Yeye ni nani anatokea wapi wala nini! Ila anapenda kunijua zaidi na mie tena kwa kujimimina najimaliza kabisaa! Hata ukienda kununua nguo atakupeleka! Yuko radhi atoroke kazini akupeleke kununua nguo! Akanikubusha sanaa mapenzi yangu na Sam wakati bado wadogo!

Mwanaume mpole yuleee sijawahi kuona! Kila kitu anakuuliza wewe unaonaje? Kyle tunafanya vipi! ***** kweli kweli kama angenioa ningekuwa nimepata bonge moja ya mume! Bonge moja ya mume! Nawaambiaje ndugu wasomaji mngekomaaa! Mngepata tabu sanaaaa! He is everything i ever wished for a husband! Nasemajeee mna bahati!

Siku ya kwanza anavua shati oooh my God! Alinivuruga sio kidogo! Siku zote anavaaga long sleeves! Iwe shati hata v neck hata tshirt lazima iwe longsleeves! Siku hio anavua naona body ina tatoo kama zote! Afu zimepangiliwa zimekuwa kama nakshi hazi chushiii! Mpaka na mimi nikatamani nikaongeze tatooo! Nina tatoo ya kipepeo mguuni Sam huyooo!

Kavua shati hivi nikasema Mungu kweli ananipenda! Na ananipenda kweli kweli! Kichelewa kote kuolewa for this man namsameheee! The wait is worth every second! Of all tatoos my favorite was Dragon! Hio dragon ni tatoo maybe kubwa kuliko zote na ipo mkononi mwake! Hii tatoonilikiwa naweza kuiangalia siku nzima na nisichoke!

Mpaka nikamwambia i want to get a tatooo! Ananiambia this shit is painful siwezi kukuruhusu! Nikamuonesha mguuni! Akawa anagoma goma! Nikamwambia nipeleke nikachore! Akawa hataki! Nikangangania sanaa mpaka akakubali mpole sanaa! Nilikuwa namkalia kichwani! Akanipeleka! Nikachora dragon wa kike! Hakumpatia sanaa kama wa Kenny! Wa Kenny alikuwa piece of work sio kidogo! KaI moja imefanywa into perfection! The shit is painful kweli kweli!

Baada ya kutibuana vuzinikaenda amfute kwa kuchora juu yake aweke kopa aandike Linda! Bora nimkumbuke shoga angu na mwanangu! Akasema haiwezekani! Dragon ni mrefu, tatoo ni kubwa afu nyembamba kuirekebisha atachafua chafua mgongo wangu pakubwa sanaa! Bora nimuache! Kwanza yupo mgongoni simuoni kwa hio hatakiwi kunikera!

Mozah akasema i should try to see other people! I never know naweza kubahatisha mkali zaidi! Sikutaka! Ila kumpa moyo nikasema ngoja nijaribu huenda jeraha likapona jumla jumla! Nikaanza kutoka out! Kila mtu naona ananiboa tuu! Seriously!

Wengine vitambi ndindi mi nishazoea kupapasa body la mazoezi lile! Wengine njaa kali! Maana mtu unamkuta siku ya kwanza antangaza njaaa! Puuuuuuu! Unamsikiliza unaona ni ushenzi mtupu! Sikufanikiwa sababu nilikuwa sitaki kufanikiwa kabisaa!

Ada ikatushinda na Hans,nikamwambia sasa Hans tunafanyaje baba mtoto! Akasema mimi hapa sina msaada mama mtoto! Tumuamishe tu shule! Nikamwambia hapana! Cha kufanya yule demu wako, main chick wako baba ake si ana hela kama zote, muombe hio pesa tuone itakuwa vipi! Hans akasema mimi sitaki anione hivi! Nikamwambia nenda bwana mimi na mwanao tunakuona hivi yeye nani asikuone hivi? Akaenda akakosa!

Nikamfata Ghost, nikamwambia mwanangu hana ada, sasa beach plot yako nakurudishia nipe ada manake nimewaza kuiuza kwa mtu mwingine nimeona sio fair! Akaniambia Linda ni mwanabgu si nilikwambiaga! Kesho naenda kumlipia ada! You dont have to give back anything sweetie!

MiGhost namjuaaaa kuliko nyie wasomaji! Hio kesho atataka uchi! Anyway nitampa show moja goli zake 3 kwani nina hasara gani? Na kweli kesho kanipigia yupo hotelini njoo chukua risiti! Nikaenda!

Kwanza mwili wake ulinikeraa! Makovu kovu kama katoka vitani! Hio mikovu anayo siku zote! Ila siku hio ilinikera zaidi! Ana mshawasha kama wote! Mimi rohoni kanitokaa sio kidogo! Ila natoa ushirikiano hivo nifanyaje ndugu msomaji? Nifanye vipi? Najiliza uongo uongo! Akojoe tu, anipishe zangu! Nikajishangaa kabisaa kilichonitoa roho kwake ni nini haswaa?

Badojeraha za moyo wangu zilikiwa kubwa sanaaa! Nikaenda kumuuliza mke wa Cookie Kenny kaenda wapi na anafanya nini? Akasema hajui! Nikamtuma mpeleleze Cookie! Akasema nauhakika hajui angeniambia! Ndp zake kupotea miaka kadhaa na kuja kuibuka tena kivingine!

Baada ya miezi mi tatu nikaanza kusikia kichefu chefu,homa, nikajua tu kitu na box! Mimba! Ya nani exactly sina uhakika! Mbona aibuuuu! Nawaambiaje watu! Naanzia wapi! Nikauza uza vitu vyangu vichache nilivo navo!

Nika apply masters Sweeden, nikamuaga Hans na kumwambia inabidi twende wote tupeane zamu mtoto! Nilijua nikimuacha takufa mapema! And somehow even if he waa a deas beat dady i juat wanted him arround my daughter! Nikamwambia naenda kusoma!

Ulaya no gharama mnoo mnoo! Nikampanga Ghost mi nataka niende Sweeden mwaka moja kwanza nikapumzike na kutuliza kichwa nisapoti! Akakubali! Tena anasema kama Ulfat atangangana kukakaka huku tuanzishe famiia kule! Mimi kukutunza sio issue! Moyoni nayajua mie!

Akatutengenezea karatasi muhimu, tukaondoka na mwanangu! Sweeden nalea tumbo langu kwa raha sanaa! Japo sijui toto hili baba yake nani ila nachojua ni toto langu na nitalipenda mpakana pumzi yanguya mwisho! Ghost anatuma pesa ya uhakika, tuna bebishana kwenye simu hatari! Ila sikumwambia na mimba wala nini! Akitaka picha za uso tu! Au nimekaaa na kuvaaa koti kubwa sanaaa!

Siku moja jioni nikiwa jogging ikapita gari kali sanaa! Kali ana ya ulaya mjue ni lamborgin! Ikapunguza mwendo kama kusimama kwa mda! Dereva akaniangaliaa kama akataka kunisemesha akaghairi na kuondoka zake! Dereva ni mzungu kabisaa and i was positive simfahamu kabisaa!

Jioni Ghost kapiga simu, ananiambia nimetoka kuchukua visa ubalozin huku nakuja na flight ya kesho! Utumbo ulinitetemeka! Na!wambia sawa baby! Nimekuhamuu kweli! Anaguma mmmhhhh! Kesho kutwa tutakuwa wote hapo kujiachia!
 
Duh!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwiiii..kyle nini lakini??!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jioni Ghost kapiga simu, ananiambia nimetoka kuchukua visa ubalozin huku nakuja na flight ya kesho! Utumbo ulinitetemeka! Na!wambia sawa baby! Nimekuhamuu kweli! Anaguma mmmhhhh! Kesho kutwa tutakuwa wote hapo kujiachia!

ITAENDELEA
 
Duuu ,t sound Kama Kyle anamimba ya konkii kr...... Amtafute tu then akubaliane na ukweli pengine drug dealers ndo fungu lake maana mabwana za wote wanahistoria ya madawa!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Konky!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…