Wee Dada! Lote hilo lakoo?

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,805
Reaction score
43,230
Habari za uzima kila mmoja pale alipo kutoka pembe nne za dunia.

Binafsi yangu ni buheri wa afya tele mwenye changamoto kiasi cha mboga, zilizo ndani ya uwezo wangu nazitatua kwa wakati na zilizo nje ya uwezo wangu napishana nazo kama bodaboda barabarani.

Twende kwenye mada kuu kabla sijachakachua hapo kwenye salamu. Leo nawaletea kisa kilichonitokea sokoni alfajiri wakati naenda kununua bidhaa kwa ajili ya kuziuza kwa wateja wangu wa huko kitongojini ninakokaa. Utangulizi kidogo, tangu mwezi wa saba mwaka huu, niliamua kufungua genge la matunda hapa mtaani ninapokaa maana magenge yako mbali kidogo na yaliyo karibu hayakuwa na matunda mengi na ukiyakuta basi yamesinyaa kwa kukaa sana gengeni.

Baada ya kuona uhitaji wa watu pale mtaani na kusikia wamama wawili watatu wakilalamika siku wakiwa na uvivu wa kwenda sokoni kufata matunda au wakihitaji matunda na muda wa kwenda sokoni ni hafifu. Basi nikakamatia fursa na kufungua kigenge pale mtaani, bi Kasinde nikakinakshi na mbaombao na makreti ya plastiki.

Ili kukidhi haja ya wateja wapate matunda fresh yaliyotoka sokoni siku hiyohiyo, nikaamua niwe naenda sokoni kila siku na gharama ya usafiri na hadi kuuza tunda nna faida yangu ya kujaza kibaba. Nikajiongeza kuweka baadhi ya bidhaa mbalimbali za gengeni zinazohitajika mara kwa mara majumbani.

Namshukuru Maulana kigenge kikazoeleka na kinawateja hadi wa mtaa wa pili na watatu kwa huduma bora, tabasamu na utani wa hapa na pale. Mteja akija gengeni kwangu si mtoto, kijana mzee lazima ataondoka na tabasamu na kesho atarudi tena. Mziki wa taratibu haukosekani gengeni kwangu kuniliwaza kipindi nasubiri wateja na saa ingine hunyanyuka na kucheza basi wateja burudaani ahahahaaa. Huo ni utangulizi looh, somo la muhtahsari wa habari sijui ntafaulu lini walaahi…. Najikuta tuu nashindwa kufupisha habari. Haya tuendelee kabla sijasahau nlichotaka kusimulia hehe





Kisa cha leo kwanza wakati natoka nyumbani Mbagala nilichelewa maana matunda mazuri kwa bei ya mkulima lazima niyadamkie alfajiri, hivo na zile haraka nikatoka bila vuvaa dera kwa juu badala yake nikaliweka kwenye mfuko wangu ambao huwa naweka kiroba cha kubebea matunda baada ya kununua, na nikasema nikifika sokoni ndo ntalivaa kwa juu ili kupunguza tafrani sokoni na kujihakikishia usalama wangu. Nilitoka nimevaa kaboka mchizi na blauzi ili nikifika sokoni nitupie dera niwe huru kuinama kuchagua matunda bila kuhofia kukaa vibaya.

Ile nimeshuka kwenye daladala natembea kwa haraka nikiwa naelekea sokoni nafungua mfuko wangu nitoke dera nivae, heeee..!! nakutana na mtandio wa dera….. Nikasimama ghafla na kujiuliza, sasa na hii kaboka mchizi na kiblauzi ntachaguaje matunda??? Si watu wataanza kuhesabu pingili kwenye mbavu looh!! Nikaishiwa pozi, nikasema nikienda hivihivi na kaboka mchizi masaburi yataleta za mbwatambwata, bora nusu shari kuliko shari kamili.

Kama askari hachagui bunduki kwenda vitani mradi ina risasi, basi nikajifunga mtandio wa dera nikaingia sokoni. Ile naingia nasikia sauti ya mwanaume inaita, weee dada…!! Wee dada…!! Weee dada weeweeee…!! Sikugeuka ila nikapiga jicho mbele sikuona mwanamke, piga jicho la kishushushu kulia na kushoto kwangu huku nikiwa naendelea kupiga hatua kuingia sokoni waapii sioni mwanadada yeyote. Sauti inayoita ilikuwa inatokea kwa nyuma upande wa kushoto, nikageuka nyuma upande wa kulia nione anayeitwa pia hakukuwa na mwanamke karibu zaidi yangu. Nikiendelea kupiga hatua ile sauti ikaita tena, weee dada weeweee… lote hilo lakoo…!!??

Nikajiuliza ni mimi itakuwa maana hakukuwa na mwanamke jirani, ila…….. lote hilo lako ni nini? Mmhhh!! Nikapuuzia nikafanya manunuzi yangu. Wakati natoka napita palepale nilipoingilia huku nikiwa nimejitwisha kiroba cha matunda kadhaa nikasikia tena sauti, huyo anaondoka. Safari hii sikuweza kugeuka maana nilikuwa nahawahi daladala nifikishe mzigo mapema, biashara asubuhi jioni mahesabu.

Kilichonifanya nilete huu uzi, ile sauti nimeendelea kuisikia siku nzima leo, wee dada, weedada weeweee….!! Lote hilo lako…!!?? Bado najiuliza lote hilo nini? Likichwa? Limikono? Litumbo? Mmmhhh kila nikijikagua sioni nina linini…!!

Najua kuna wataosema kesho nikamuulize, hapana sitomuuliza japo sokoni naenda kila siku, nimeona nisimulie hapa labda hiyo sauti itaacha kujirudia rudia.

Ahsanteni kwa kunisikiliza, Alamsiki.



NB: Picha ni mfano, si uhalisia wa genge la Kasinde.



Kasinde Matata.
 
[emoji16][emoji16] my dada utakuwa ns mzigo wa kiwango gani hadi watu wakushangae...maana ta.ko sio habari tena siku hizi, asilimia 60 ya wanawake nimaokutana nao wamefungasha
 
Sijaona Cha ajabu ila nimeona ni simulizi ya kitoto kabisa...hivi unafikiri tako ni ishu Sana?kila mtu siku hizi anatako
 
Unaweza kukuta unatiti titi Kama kibuyu Cha bi mwenda....Sasa jamaa alitaka ugeuke alione.
 

Buu G,

Hapa mwendhio nshalowa ndembendembe nasubiri kukaushwa nirejee kwenye mstari.

Aahahahahahahhaaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…