Website za Bongo:Tulikuwa tayari au tulilazimishwa?

Website za Bongo:Tulikuwa tayari au tulilazimishwa?

Aqua

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2012
Posts
1,657
Reaction score
1,237
Habari wadau
Kuna kitu kimeshanikuta kama mara mbili,kuna kipindi nilitaka niulizie hapa jf baadaya nikaamua kwenda kwenye ofisi za hao wahusika.Walichonieleza ni aibu.
Baadhi ya makampuni(wizara/watu) yamekuwa na website ila kitu ambacho kinashangaza utakuta kile walichoandika kwenye website zao ni tofauti na khali halisi iliyopo ofisini kwao.
Kwa mfano kuna chuo kimoja maarufu hapa Tz kwa kutoa mafunzo hasa ya computer,kuna course zinawekwakwenye website say course itaanza tarehe 15May2013 ukienda ofisini kwao ukichukua form zinasema kitu tofuti.Bora hilli labda hawakupata wanafunzi wa kutosha.
Je inakuaje namba ya simu waliyoweka au e-mail address ikiwa haifanyi kazi na wao wanajua na bado wameiacha kwenye website yao?
Ushauri kwa wenye website au wanaoupdate website,tuweke numba za simu zinazopatikana au e-mail address zinazofanya kazi.Na website ziwe updated hiyo ndiyo maana halisi ya website,website ni ofisi yenu inayopatikana kwenye web.Au online business bongo bado sanaa eeh?Tunaiga iga tu.

Kama wewe mnawebsite jiulize,contact information zenu zinafanya kazi na mnapata e-mail au simu?
Aqua:Kaka habari yako,unafanya kazi hapa ....... maeneo ya Mussa's son.
Mshikaje:ndiyo,sema nikusaidie nini?
Aqua:Hivi ile e-mail yenu ya info@...go.tz inafanyakazi?Kwani nimewaandikia e-mail kama mara 3 hivi lakini zinafail.Na contact form yenu je vipi kuna mtu huwa anasoma tunachowatumia?
Mshikaji:Aaah,hiyo e-mail haifanyi kazi achana nayo kabisa,jamaa wa ICT wanafanyia kazi.
Aqua:Ok,lakini si unajua website yenu inawawakilisha nyie?Kwa hiyo kama kuna madudu kwenye web site yenu hii inaonyesha hamko...... na kuna mtu analipwa kwa ajili ya hiyo website!

NB:Kuna website nyingi tu contact information zao ni vimeo na huwezi amini ni za sehemu nyeti au makapuni makubwa.
 
Website zimekaa kama blog sasa cjui wenye blog wafanyaje??
 
Back
Top Bottom