Website designer anahitajika

Website designer anahitajika

Barakaeli174

Senior Member
Joined
Aug 2, 2015
Posts
171
Reaction score
142
Tunahitaji professional web designer kwa ajili ya website ya chuo, financial services na NGO. Mzoefu awe ana uwezo wa ku design website na database ndani yake kwa ajili ya watumiaji wa huduma za ofisi hizo.

Maombi yote yaambatanishwe na gharama za kutengeneza tovuti. Maombi yatumwe kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu, ATL P.O.Box 9300 Dar es salaam
 
Dunia ya leo mnapokea maombi kwa njia ya Posta! Barua za Maombi kutoka Ngara, Malinyi, Kasulu, Tandahimba, Simiyu na pembe zote za nchi, zitatumia muda gani kuwafikia? Na wakati huo huo mkongo wa taifa ushaenea sehemu kubwa ya nchi, huku ofisi nyingi za Posta na Halmashauri zina Access ya Internet!

Haya bwana, nawatakia kila la kheri!
 
Tunahitaji professional web designer kwa ajili ya website ya chuo, financial services na NGO. Mzoefu awe ana uwezo wa ku design website na database ndani yake kwa ajili ya watumiaji wa huduma za ofisi hizo. Maombi yote yaambatanishwe na gharama za kutengeneza tovuti. Maombi yatumwe kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu, ATL P.O.Box 9300 Dar es salaam

Yaani mtu ambaye atakuja kuomba kazi hiyo kwenu lazima afikirie kupanga bei mara mbili maana kama ni professional ambaye hashuki chini ya milioni alafu unamwambia atume barua kwa sanduku la posta karne ya 21 mwaka 2015, ni utani huu. Labda niwakumbushe kua mwaka huu 2015 kufungua email kama huna custom domain basi gmail ni bure.
 
Hahahaha,Nimecheka mpaka basi.
Hii Post sijui kama aliepost sio yule Mzee wa Kipindi cha Malumbano ya Hoja cha ITV Askari Mstaafu.

Enzi za Mwalimm

kweli Technology imekimbia kwa kasi sana kuja kwetu huku tukiwa hata hatujaamka.
Mungu nusuru kizazi hiki kijitambue.

Halafu Gharama za Kutengeneza Website zinategemea na Ukubwa wake na trees structures(wataalam mtaweka sawa hapa).
Kwa hiyo mtu hawezi kutuma Maombi akaweka na gharama zakutengeneza,Ndio hapo mtakuta **** mmoja anawez kusema anaweza kutengeneza hata kwa Laki sita tu,ahalfu hapo hapo akaibuka mwingine akasema kwamba anaweza kutengeneza kwa Milioni tatu au nne.Sasa mnaweza kumkimbia huyu wa pesa nyingi bila kujua kwamba ni vitu gani amevijumuisha ili website iwe ya kisasa.

Nayway,naimani designers lazima watakupiga maswali hadi ushike adabu ndio wakutumie Quotation
 
Cc:Bakulutu

Dunia ya leo mnapokea maombi kwa njia ya Posta! Barua za Maombi kutoka Ngara, Malinyi, Kasulu, Tandahimba, Simiyu na pembe zote za nchi, zitatumia muda gani kuwafikia? Na wakati huo huo mkongo wa taifa ushaenea sehemu kubwa ya nchi, huku ofisi nyingi za Posta na Halmashauri zina Access ya Internet!

Haya bwana, nawatakia kila la kheri!
 
Tunahitaji professional web designer kwa ajili ya website ya chuo, financial services na NGO. Mzoefu awe ana uwezo wa ku design website na database ndani yake kwa ajili ya watumiaji wa huduma za ofisi hizo.

Maombi yote yaambatanishwe na gharama za kutengeneza tovuti. Maombi yatumwe kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu, ATL P.O.Box 9300 Dar es salaam

Ni pm inbox mimi ni mtaalamu wa dynamic website with databases, bei tutaelewana natengeneza kazi nzuri na zinazokidhi viwango
 
Back
Top Bottom