We mbaba unaacha ngapi ya mezani?

Pesa inayoachwa mezani ni Kwa ajili ya dharura ndogo ndogo, baada ya kuhakikisha chakula kimo ndani, mboga nk nk.
embu acheni unafiki wa isidingo

mtzania wa kawaida hana maisha hayo mnayosema ya kuacha pesa ya dharura.

kwanza ni kwa kipato gani?
 
hayo ni maisha ya isidingo

sio ya mtzania wa kawaida maana hana iyo pesa ya dharura.

ukitaka kuamini haya nayosema pale inapokaribia na mwisho wa mwezi we pita kwenye atm uone watu wanavohaha kuingiza na kutoka kadi zao kwenye
maana yake mshahara haukutani
 
Mwanamke wa namna hii ndio namtafuta
 
embu acheni unafiki wa isidingo

mtzania wa kawaida hana maisha hayo mnayosema ya kuacha pesa ya dharura.

kwanza ni kwa kipato gani?
Vipato vya Watz havilingani, mipango hailingani, matumizi pia hayalingani.
 
Ukiona mshahara haukutani, wewe ni Mwizi wa ZAKA!!

Lipa ZAKA Kwa Mungu uone kama utapungukiwa.
 
Mi siachi kitu kila kitu kipo ndani labda hela ya vocha na emergency.
 
Kwa maisha ya mjini wewe kula tu chochote utakachokikuta bila kujali umeacha ngapi...... wanaume kusaidiana
 
Mboga na viungo 150,000\month haipungui na haijawahi kutosha.
 
mkuu jiandae kuto.mbe.wa
Mkuu,
Mimi siishi dasilama nipo huku katavi ndani ndani Kijiji kinaitwa nsenda huku mahindi,maharage, viazi, mihogo + mbogamboda zipo za kujichumia shambani kwangu ,kisamvu,mchicha,majani ya maboga,kabeji,spinach,matembele buku jero inatosha huku kijijini na inabakia..

Kuacha home Buku jero (1500) Ni kwa majir 😊 wachache mnoo hapa kijijini maana Mimi kijijini ndio nakiduka Cha mahitaji muhimu

NB.
Huku Kodi ya nyumba unapata hata kwa 3000,7000,10,000 mkuu Tanzania Ni pana Sanaa sanaaa mkuu tembea ujionee
 
duh umetisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…