Nina wazo la kufanikisha 'project Y' mwishoni mwa mwaka huu. Katika hiyo project nahitaji vijana wenye vipaji katika ushonaji nguo, mabegi ya ngozi, viatu vya ngozi; au mwenye kipaji cha kutengeneza video za katuni.
Ningependa wapatikane wale ambao wako tayari kuanzia chini. Miezi 4 ya mwanzo hakutakuwa na malipo, ila utalipiwa unapoishi na huduma ya chakula itakuwepo. Wanatakiwa kama ifuatavyo; ushonaji nguo 1, ushonaji viatu 1, ushonaji mabegi 1, mtengeneza video za katuni 1.
Kama una hivyo vipaji au ujuzi,karibu tujadili