Wazo la mapato mapya kwa Serikali

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,092
Naitaka Serikali ya Jamuhuri itunge sheria itakayotoa kibari kwa kila kijana aliye na umri wa miaka 18-35 na kuendelea (awe tajiri au masikini, awe na ajira au hana) kuchangia kwa lazima Tsh.6,000 kila mwaka.
Napendekeza fedha zitumike ktk eneo moja ambalo ni viwanda tu.
Naomba utaratibu uwe kama ifuatavyo;
1. Ujenzi wa kiwanda kikubwa kimoja kila wilaya ambacho kitatoa ajira kwa hao vijana.
2. Serikali mmnaweza fanya mapendekezo ni wilaya ipi inafaa kiwanda kikubwa cha watu wa Jamhuri kijengwe.
3. Viwanda vijengwe vitano (5) kwa mwaka.
4. Hivyo viwanda viwe na uwezo wa kutoa ajira zisizopungua idadi ya watu 250-450.
5. Wasimamizi wa hivyo viwanda wawe vijana wenyewe.
6. Utaratibu wa ajira ni kila kijana kujisajiri kupitia serikali ya mtaa wake.
7. Pawe na akaunti maalumu ya kuweka hizo pesa. Napendekeza ziende moja kwa moja BOT.
8. Vijana wa mkoa husika ambapo kiwanda kinajengwa ktk wilaya yao ndio wapewe ajira.
 
HII SI NDO ILE WALIKUWA WANAITA KODI YA KICHWA AU??
Ndo I arudi kwa sura mpya nini
 
Kichwa chako kimejaa kamasi badala ya ubongo
Toa wazo au mawazo yako kwa Serikali ya Jamhuri huzuiwi. Usipe kuwaza ubaya waza na mema kwa wingi.
Hii nchi ni yetu sote.
"Vijana watapata maono, wazee wataota ndoto"
In Tanzania no one is above the law.
 
Wazo zuri ila haliendani na nchi yetu na wakati tuliopo hayo ni mambo yalikuwa ya wakoloni
Hapo ili wazo liwebora, serikali wanaweza kutengeneza kanzi data ya kila mtaa kwa kata kwa wilaya kwa mkoa.
Itasaidia sana.
Pia tusiwe na mambo ya interview ktk hizo ajira bali kama mtu unataaluma fulani (semi & skilled labor) au afya yako inakizi kufanya kazi unafanya (unskilled labor).
 
Pia tuwe wabunifu wa mambo yetu wenyewe. Hata ikitokea tumeiga basi tuboreshe hayo mawazo yaendane na mahitaji yetu.
 
Naitaka Serikali ya Jamuhuri itunge sheria itakayotoa kibari kwa kila kijana aliye na umri wa miaka 18-35 na kuendelea (awe tajiri au masikini, awe na ajira au hana) kuchangia kwa lazima Tsh.6,000 kila mwaka.
Napendekeza fedha zitumike ktk eneo moja ambalo ni viwanda tu.
Naomba utaratibu uwe kama ifuatavyo;
1. Ujenzi wa kiwanda kikubwa kimoja kila wilaya ambacho kitatoa ajira kwa hao vijana.
2. Serikali mmnaweza fanya mapendekezo ni wilaya ipi inafaa kiwanda kikubwa cha watu wa Jamhuri kijengwe.
3. Viwanda vijengwe vitano (5) kwa mwaka.
4. Hivyo viwanda viwe na uwezo wa kutoa ajira zisizopungua idadi ya watu 250-450.
5. Wasimamizi wa hivyo viwanda wawe vijana wenyewe.
6. Utaratibu wa ajira ni kila kijana kujisajiri kupitia serikali ya mtaa wake.
7. Pawe na akaunti maalumu ya kuweka hizo pesa. Napendekeza ziende moja kwa moja BOT.
8. Vijana wa mkoa husika ambapo kiwanda kinajengwa ktk wilaya yao ndio wapewe ajira.
Waambie wanasiasa wajipunguzie marupurupu, ruzuku na mishahara ya kifisadi. Hamuwagusi wao, kila siku kuwakamua walala hoi!
 
Hi hi hi hivi umeeanda shule kweli? Yan njia zilizotumika na wakoloni na Nyerere, Mwinyi alafu dunia ikaziacha wewe ndio unakuja nazo na unaona una wazo bora.

Umezaliwa mwaka gani? Umesoma mpk level ipi? Maana ni ajabu hujui vitu vidogo hivi. Na mfumo wa kodi wa kisasa huujui hata tafuta maarifa kwanza ili uweze ishauri sarikali upo nyuma sana hata ubalozi wa mtaa uwezi pata.
 
Kodi ya kichwa, kodi tunalipa nyingi sana, hizi hizi tunazolipa zinatosha zikitumika vizuri, hakuna haja ya kuumiza watu zaidi.
 
Hii sio kodi ya kichwa. Pia huo mfano ulioutoa wa kodi ya kichwa kipindi cha wakoloni na awamu ya uongozi wa nyerere hayo mapato yalijenga viwanda?
Serikali imekuwa na sera nzuri ya viwanda ila imeshindwa kuja na njia ya wapi mitaji itapatikana na pia kuondoa changamoto ya ajira kwa vijana.
Uzuri viwanda hivyo vikianzishwa nyinyi vijana wenye taalumu na mnaoishi mkoa husika ndio mtaviendesha kwa weledi wenu huku kukiwa na muongozo wa kisera kutoka Serikalini.
 
Kodi ya kichwa, kodi tunalipa nyingi sana, hizi hizi tunazolipa zinatosha zikitumika vizuri, hakuna haja ya kuumiza watu zaidi.
Acha kuogopa, unataka nchi ujengewe na nani?
Yaani kutoa Tsh.500 kwa kila mwezi kwa miezi 12 ushindwe kweli? Mbona mnapenda kulalamika na hamna majibu ya njia ya nini kifanyike?
Je, unafurahia vijana wenzako kukosa elimu bora, ajira na maisha mazuri? Mimi na wewe tunajukumu la kulitengeneza taifa letu kwa njia zote.
 
Naitaka Serikali ya Jamuhuri itunge sheria itakayotoa kibari kwa kila kijana aliye na umri wa miaka 18-35 na kuendelea (awe tajiri au masikini, awe na ajira au hana) kuchangia kwa lazima Tsh.6,000 kila mwaka.
Napendekeza fedha zitumike ktk eneo moja ambalo ni viwanda tu.
Naomba utaratibu uwe kama ifuatavyo;
1. Ujenzi wa kiwanda kikubwa kimoja kila wilaya ambacho kitatoa ajira kwa hao vijana.
2. Serikali mmnaweza fanya mapendekezo ni wilaya ipi inafaa kiwanda kikubwa cha watu wa Jamhuri kijengwe.
3. Viwanda vijengwe vitano (5) kwa mwaka.
4. Hivyo viwanda viwe na uwezo wa kutoa ajira zisizopungua idadi ya watu 250-450.
5. Wasimamizi wa hivyo viwanda wawe vijana wenyewe.
6. Utaratibu wa ajira ni kila kijana kujisajiri kupitia serikali ya mtaa wake.
7. Pawe na akaunti maalumu ya kuweka hizo pesa. Napendekeza ziende moja kwa moja BOT.
8. Vijana wa mkoa husika ambapo kiwanda kinajengwa ktk wilaya yao ndio wapewe ajira.
Sasa wewe unafikiria hio 6000 watatoa wapi kama hakuna ajira kwao?au watu wanachapisha hela majumbani kwao?
 
Acha kuogopa, unataka nchi ujengewe na nani?
Yaani kutoa Tsh.500 kwa kila mwezi kwa miezi 12 ushindwe kweli? Mbona mnapenda kulalamika na hamna majibu ya njia ya nini kifanyike?
Je, unafurahia vijana wenzako kukosa elimu bora, ajira na maisha mazuri? Mimi na wewe tunajukumu la kulitengeneza taifa letu kwa njia zote.
Shida siyo kutoa hiyo 500/=, hata 10,000/= tunaweza kutoa, shida ni kwamba unatuomba tuongeze kijiko cha maji kwenye bwawa la kuogelea la olimpiki halafu uone tangible effect katika uhalisia, hayo matrillion wanayokusanya kila mwaka washindwe kifanya hicho unachosema halafu tutegemee hizi 500/= ndio zifanye? Zitalowa tu na hata usione faida yake
 
Naitaka Serikali ya Jamuhuri itunge sheria itakayotoa kibari kwa kila kijana aliye na umri wa miaka 18-35 na kuendelea (awe tajiri au masikini, awe na ajira au hana) kuchangia kwa lazima Tsh.6,000 kila mwaka.
Napendekeza fedha zitumike ktk eneo moja ambalo ni viwanda tu.
Naomba utaratibu uwe kama ifuatavyo;
1. Ujenzi wa kiwanda kikubwa kimoja kila wilaya ambacho kitatoa ajira kwa hao vijana.
2. Serikali mmnaweza fanya mapendekezo ni wilaya ipi inafaa kiwanda kikubwa cha watu wa Jamhuri kijengwe.
3. Viwanda vijengwe vitano (5) kwa mwaka.
4. Hivyo viwanda viwe na uwezo wa kutoa ajira zisizopungua idadi ya watu 250-450.
5. Wasimamizi wa hivyo viwanda wawe vijana wenyewe.
6. Utaratibu wa ajira ni kila kijana kujisajiri kupitia serikali ya mtaa wake.
7. Pawe na akaunti maalumu ya kuweka hizo pesa. Napendekeza ziende moja kwa moja BOT.
8. Vijana wa mkoa husika ambapo kiwanda kinajengwa ktk wilaya yao ndio wapewe ajira.
Ntaafiki wazo lako iwapo tu ukusanyaji huo wa mapato utaendana na mfumo mzuri wa kuwajibishana na uhuru wa kuhoji matumizi hovyo ya fedha.
 
Back
Top Bottom