Wazo la kutengeneza kikundi cha vijana wajasiliamali

fabianmalaba

JF-Expert Member
Feb 21, 2017
280
183
Ndugu zangu,
Kwa jina naitwa Fabian,umri wangu ni miaka 30 nipo mkoa wa Dar es salaam,elimu yangu ni taaluma ya teknolojia ya habari ngazi ya cheti tu,kutokana na kukosekana kwa ajira hapa kwetu, mimi kama kijana mwenzenu nimekuja na wazo dogo sana la ujasiliamali,

Wazo langu ni hili,

Tuungane vijana 15 jinsia mchanganyiko,tukutane mahala popote tutakapo kubaliana kukutana tujadiri wazo langu hili

TUKIWA WATU 15 JINSIA YOYOTE,KATIKA HAO KUMI NA TANO NAAMINI TUNAWEZA KUANZISHA GENGE LA CHAKULA MAHALI POPOTE KWA KUCHANGIA KILA MMOJA ELFU 20 ILI TUTENGENEZE BANDA NA KUNUNUA VIFAA VYA SHUGHULI NZIMA HALAFU TUTAPEANA ZAMU YA KUHUDUMIA KATIKA SHUGHULI YETU MRADI KUWEPO NA UONGOZI NA TUTAIWEKA KATIKA NGAZI ZA SERIKALI ILI KUSIWEPO NA UJANJA UJANJA,BAADA YA MWEZI MMOJA TUNAJUMLISHA MAUZO YOTE TUNAKAA CHINI NA KUJADILI NINI TUFANYE ILI KUBORESHA ZAIDI

natanguliza shukrani zangu za dhati,

kwa atakaekuwa tayari basi tuwasiliane hapa au tunaweza kutengeneza kikundi cha mawasiliano kwanza ili tujue tumefika wangapi ndipo tukutane na kujadiri suala hili pengine kukawa na fursa nyingine tofauti na hii

tutafutane hapa +255765325644 (whatsapp)
 
Hongera sana mkuu kwa wazo hili..
Ila kwa ushauri ungeanza na wale vijana ambao mlisoma nao na bado hawajapata kazi kama wewe au pia wale wa mtaani kwako/kijiweni ingekuwa rahisi kwenu kuendesha hiyo biahsara sababu mnajuana vizuri kuliko hapa utapata mwingine yupo namtumbo mwingine uchira mwengine.
 
Wazo zuri sana mkuu tena isiwe genge iwe ufugaji wa kuku kama tunajikusanya ata kumi to tunaanzisha mrad mnzuri sana kwa mm nipo teyari ukiwapata wengine ni pm
 
Watanzania hususani Vijana porojo kibao, hawawezi kufanya kazi kwa vikundi

- Vipi kwenu ni hapa hapa Dar na eneo vipi la kufanyia business vipi ?
 
MRADI HUU UNALENGA HASA WATU WALIOPO MKOA WA DAR ES SALAAM SIO MIKOA MINGINE

(kuna mtu katoa maoni kwamba nianze na watu niliosoma nao hapana ndugu yangu sijapenda kufanya hivyo maana najua kama itakuwepo mikakati madhubuti na watu walio tayari kufanya kazi haijalishi mnajuana tangu lini, cha muhimu ni kufanya kazi basi,then mambo yetu yataenda kwa maandishi ya kiserikali sio kiholela, naamini tutapata watu wazima wenye akili timamu,kazi sio lazima mjuane background au mmesoma wote.

Ndugu zangu Watanzania wenzangu

Hili jambo si la masihara hata kidogo,hivyo tunahitaji watu walio committed katika kazi na si ubabaishaji, lengo ni kutaka kujikwamua kimaisha na najua hakuna kitu kinachokua rahisi kukianzisha lazima kuna vikwazo, wengine watatukatisha tamaa lakini tujue nini tunakifanya naamini tutasonga mbele,

mpaka sasa nimeshafuatwa na watu wanne tu inbox walio tayari katika hili,

Niliona niweke kiwango hiki kidogo cha kuanzia maana ningeweka pesa nyingi watu wasingejitokeza lakini tukikutana tujadili itakua vyema maana tutafikia muafaka na tutajua ni kiasi gani cha kuanzia,pengine tutapata mawazo mengine mazuri zaidi,

nazidi kusubiri watu kufikia kesho kutwa nitakua nimepata idadi kamili ya watu tutakaokutana na kikundi cha mawasiliano kitatengenezwa ila tuwe na subira tuone tutakua wangapi

Ahsanteni..
 
Watanzania hususani porojo kibao, hawawezi kufanya kazi kwa vikundi

- Vipi kwenu ni hapa hapa Dar na eneo vipi la kufanyia business vipi ?
.

Usiwakatishe tamaa waliodhamiria.Ni wazo zuri na hatua nzuri kuanzia,ninawashauri kuwa msilazimishe kuwa muwe vijana tu.Ruhusuni na wengine bila kujali umri wao.Toeni nafasi siku ya kwanza mtakayokutana kila mmoja wenu apendekeze wazo lake.Jadilini kwa utulivu na busara kisha amueni kwa pamoja muanze na lipi miongoni mwa mawazo mengi yatakayotolewa.

Wekeni kanuni za kujisimamia na hatua za kuchukua kwa wakosaji,itawalipa mno.
 
Watanzania hususani porojo kibao, hawawezi kufanya kazi kwa vikundi

- Vipi kwenu ni hapa hapa Dar na eneo vipi la kufanyia business vipi ?
ndugu yangu,siwezi kukushawishi hata kidogo maana jambo hili ni hiari ya mtu, hapa hakuna porojo hata kidogo na kila mmoja lazima awajibike kufanya kazi, kama unafikiri watu hawawezi kujiunga katika vikundi basi subiri tumalize kikao tutakachokifanya hapo mbeleni tutakupa mrejesho
 
Bas tufanyeni kitu kimoja tutengeneze ka group cha wsp tukifika kama 10 ivi alaf tupange iyo kitu ila tuwe wa dar tupu me naandaa ilo group
hilo wazo lipo akilini mwangu hata kabla ya kuweka wazo hapa, kwaiyo usipate tabu najaribu kusubiri nione response ya watu ndipo nitengeneze hilo kundi la mawasiliano la whatsapp
 
Kumbe message niliianzia katikati nami nipo Dar es Salaam na tupo tayari, mimi na Wife maana wote ni wahanga wa ajira za serikali ya awamu ya tano
sawa kaka naomba tuwe wavumilivu tu ili tuwe angalau kumi na zaidi ndipo tukutane nadhani ndio jambo la busara zaidi au unasemaje mkuu
 
Ni wazo zuri sana. Upo wapi mkuu mi nipo tayari na tayari ninaye kijana mwingine hapa yupo tayari pia.
nashukuru kwa mwitikio wako naamini tutakua wapiganaji wote, tuvute subira kufikia kesho kutwa tujue tupo wangapi ili tupange namna ya kukutana na kujadiriana,cha msingi mjaribu kunitafuta kwa namba yangu iliyopo huko juu nijue tumefika wangapi
 
ndugu yangu,siwezi kukushawishi hata kidogo maana jambo hili ni hiari ya mtu, hapa hakuna porojo hata kidogo na kila mmoja lazima awajibike kufanya kazi, kama unafikiri watu hawawezi kujiunga katika vikundi basi subiri tumalize kikao tutakachokifanya hapo mbeleni tutakupa mrejesho
Sikukatishi tamaa ila ukifanikiwa kuwaweka kikundi na mkafanya jambo hususani la kiuchumi mimi nitajitoa JF - Labda lingekuwa WAZO LA MAANDAMANO YA KISIASA, Ungefanikiwa kwa 100%
 
Hongera sana mkuu kwa wazo hili..
Ila kwa ushauri ungeanza na wale vijana ambao mlisoma nao na bado hawajapata kazi kama wewe au pia wale wa mtaani kwako/kijiweni ingekuwa rahisi kwenu kuendesha hiyo biahsara sababu mnajuana vizuri kuliko hapa utapata mwingine yupo namtumbo mwingine uchira mwengine.
nashukuru sn kaka, lakini nimejaribu kutolea ufafanuzi katika maoni yako kwa maelezo marefu huko juu kwahiyo hakuna shaka juu ya hili.
 
Mtoa mada ameweka namba yake. Kama upo serious mfuate whatsapp ili iwe njia rahisi ya kuunda Group la whatsapp. Tuwe serious! Hili linaweza kuwa na tija kubwa sana kwetu. Ningependa ikibidi J5 tarehe 1 tukutane kwa ajili ya uasisi wa shughuli yetu hii.
 
Back
Top Bottom