Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 1,339
- 1,493
Heshima kwako muhusika!
Napendekeza wazo la ajira ambalo litasaidia wazee, walemavu na watu wasiojiweza kiuchumi kusaidika na kuwa fursa kwa vijana wahitimu wa ngazi tofauti za elimu hapa nchini.
Napendekeza Wizara ya Afya + Wizara ya Ulinzi washirikiane kwa pamoja katika kutekeleza hili swala kibajeti na vitendea kazi.
Zijengwe "Kata House" zenye uwezo wa kuchukua watu 200 - 500 kila kata ambazo watakaa watu wenye ulemavu wote (wasio na uwezo kujihudumia), wazee wasiojiweza, watu masikini kabisa na watoto wasio na makazi.
FAIDA
1. Tutaondoa tatizo la watu masikini na wasiojiweza nchi nzima.
2. Sera ya ustawi wa Taifa itafanyika na kutimilika vizuri.
3. Tutatengeneza ajira zisizopungua 20-30 kwa kila kata nchini (Vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali)
4. Tutachochea mpangilio mzuri wa maendeleo ktk mji/ mijini na maendeleo ya watu kiuchumi.
5. Tutakuwa tunaona muelekeo mzuri ktk kufikia uchumi wa kati.
GHARAMA ZA UENDESHAJI "KATA HOUSE"
1. Wizara tajwa zitawajibika ktk kutoa bajeti ya kuendesha hizo program zikisaidiana na wananchi husika wa KATA husika kuchangia gharama ndogo ndogo ili kuchochea maendeleo ya kituo.
2. Serikali kuu inaweza kuazimia kuziombea fedha hizi program na kuzifadhili kwa namna inavyoona inafaa.
3. Kila kituo ktk KATA lazima kianzishe mradi wa kujiendeleza wenyewe usiojihusisha na kodi za moja kwa moja, mfano ufugaji ng'ombe maziwa, mbuzi wa nyama, kuku mayai au nyama, kilimo biashara nk
MWISHO
Kuhusu hili wazo Serikali itaweza kutengeneza ajira kubwa kwa vijana na upande mwingine ikiondoa changamoto za watu wasio na makazi kuzagaa mitaani, omba omba wa mijini, umasikini wa vipato na walemavu wa aina zote wasiojiweza.
Nakumbusha hili, Serikali ina wajibu kwa wananchi kuwapa ustawi bora wa maendeleo kimaisha na kiuchumi.